Waziri wa Mambo ya Ndani, Uhamiaji wanakuhujumu!

Malilambwiga

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
485
296
Kuna gari T.435 AXE Toyota Rav4. Gari hii inatumiwa na maafisa wa uhamiaji kupita kila eneo walipo wageni hususani wenye asili ya Asia wanaoishi na kufanya kazi nchini kinyume cha sheria.

Wanachokifanya ni kuwatisha wahusika kisha wakishaonwa faragha biashara inaishia hapo.

Wiki moja iliyopita nimeshuhudia kwa macho yangu katika barabara ya Kilwa eneo la Mbagala wakiingia Yard mbili tofauti na mambo yalikuwa kama kawaida hawaogopi chochote wala hawana aibu.

Waziri tupia macho gari hili wanaoitumia wanakuhujumu.

Usiishie viwanja vya ndege tu na ukitaka kufanikiwa, idara hii igeuze badala ya kuwa idara inayojitegemea iwe ni kikosi cha Polisi na Kamishna wake awajibike kwa Inspekta Jenerali wa Polisi, hapo kazi zitaenda.
 
Kwani kuna ushahidi gani kwamba polisi hawapokei rushwa, Malilambwiga?.

Kwa taarifa yako, polisi ndio wanaochukua rushwa kutoka kwa watu wanaoishi kinyume cha sheria kuliko hao maofisa wa uhamiaji.
 
mawazo ya namna ya malilambwiga ,nchi haiwezi endelea. ukiangalia jeshi la polisi limeshindwa kutekeleza mambo mengi kwa weledi na kuna tatizo kubwa la rushwa pamoja na kuanzisha madawati mengi lakini bado hayajawasaidia wananchi .uhamiaji inahitaji kuboreshwa kwa kuweka kiongozi madhubuti atakayesimamia uwajibikaji kwa watumishi wa uhamiaji pia atakayesimamia stahiki za maofisa kulipwa kwa wakati,kupandishwa vyeo kwa wanaostahili kwa wakati. suala la maslahi ya maofisa uhamiaji na kupandishwa vyeo imekuwa ni changamoto kubwa.
 
Back
Top Bottom