Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba: Naagiza aliyemtolea bastola Nape Nnauye, achukuliwe hatua

Next is @Mwingulu nchemba jipange kisaikolojia bro

Mwingulu hajui saa wa dk atakapo kuja mwana wa Adam kuja kumtengua uwaziri

Mwigulu Nchemba kumbe haujamuelewa, kwa ujumbe huu sio kwamba anahitaji kujipanga kisaikolojia, ni kwamba tayari ameshaamua kueleza hisia zake za kuonyesha kutokuridhishwa na mambo yanavyoendeshwa na sio hivyo tu, ameonyesha kumuunga mkono Nape. Ni kitendo cha kijasiri kwa awamu hii kutuma ujumbe wa aina hiyo kama haujajipanga, anajua anachokifanya.
 
MIMI NADHANI MAWAZIRI AMBAO HAWANA FURAHA KUFANYA KAZI KTK NCHI HII YA KUSADIKIKA WATUMIE FURSA YA KULAANI ALICHOFANYIWA NAPE ILI WATUMBULIWE WABAKI NA UBUNGE WAO ILI MFALME HADI AMPANDISHE DAUD AMPE WIZARA KTK CCM MAWAZIRI 3, NAPE,JANUARY & MWIGULU WALIPIGANIA KWELI KWENYE LAST UCHAGUZI ILA KWA SASA HAWAAMINI LAZIMA KUNA KITU
Mlimsikia mwenyekiti anasema kuna waziri mmoja anasumbua anatoa siri,nimemshtaki Kwa baba yake. Huyo ni makamba
 
We Mwigulu wewe, unajipenda au hujipendi!!?? shauri yako, yasije yakakukuta yaliyomkuta mwenzio, usije ukasema hatujakuambia!??
 
Naomba unielewe hatuzuii mtu yeyote kukamatwa wala kuhojiwa wala kukatazwa jambo, nasemea utaratibu wa kuoneshwa bastola hadharani sio kitendo cha kiuaskari na sio kitendo cha Tanzania, hata Lema na Lisu hawajawahi kunyoshewa bunduki. Usichanganye sheria kuchukua mkondo na bunduki kuchukua mkondo
Ngoja nikusaidie mkuu kutoa Maelezo, askari kuwa na Silaha ya moto hadharani sio kosa, kosa ni kwamba alipointi bastola kwa nape huku akijua sio muharifu
 
Wanafik km kina nape, Mwigulu, makonda, makamba hawafai kuaminiwa wakapewa madaraka

Siku zote wanaangalia upande wenye maslahi
Hujui ulisemalo kwani hao unawadharau leo wakija kwenu mtawapokea kama watume na wafalme tena mtawasujudu kuliko ata Mwenyekiti wenu wa chama kwakuwa waliandaliwa kuwa viongozi bora na si kuwa watawala....
 
Mwigulu Nchemba kumbe haujamuelewa, kwa ujumbe huu sio kwamba anahitaji kujipanga kisaikolojia, ni kwamba tayari ameshaamua kueleza hisia zake za kuonyesha kutokuridhishwa na mambo yanavyoendeshwa na sio hivyo tu, ameonyesha kumuunga mkono Nape. Ni kitendo cha kijasiri kwa awamu hii kutuma ujumbe wa aina hiyo kama haujajipanga, anajua anachokifanya.
Ni bora utumbuliwe kwa kusimamia ukweli halisi wa jambo kuliko utumbuliwe kwa sababu isiyo na mashiko.
Kitendo cha yule askari chakupigwa na kila RAIA Jana imemtokea Nape next time inaweza kutokea kwa yoyote na kusababisha mauaji.
 
Nawale walio vamia clouds

MH. NAPE NDIYE NDIYE RAIA KWANI SIKU ILE WALIPOVAMIWA CLOUDS TENA MUDA WA USIKU WA MAJAMBAZI NA MBALAMWEZI PALE MH. MWIGULU HAKUSEMA NENO. TULIMUONA MH. NAPE PEKEE HADI IKASABABISHA KUACHISHWA NAFASI YA KUTEULIWA.

LEO MH. NAPE AMEONYESHWA BASTOLA MCHANA WA JUA, TUNASHUHUDIA TAMKO LA WAZIRI MWENYE DHAMANA.
 
View attachment 485970
Mwigulu Nchemba(Kushoto) akizungumza na Nape Nnauye katika ukumbi wa NEC kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma 10/15/2014(Maktaba)

Mh. Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu. Kitendo cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha kiasikari, sio cha kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini.

Nahusika na Usalama wa Raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni Askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake.
======

View attachment 485994
SWALI: KWA NINI WAZIRI AAGIZE NA ASIKAMATWE KWANZA,NDO ATOE TAARIFA KUWA YEYE NDO KAAGIZA LIFANYIKE?
 
View attachment 485970
Mwigulu Nchemba(Kushoto) akizungumza na Nape Nnauye katika ukumbi wa NEC kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma 10/15/2014(Maktaba)

Mh. Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu. Kitendo cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha kiasikari, sio cha kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini.

Nahusika na Usalama wa Raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni Askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake.
Naungana na ww kulaani pia nakupongeza kwa hatua ulizochukua kama kiongozi mwenye dhamana..........nakukumbusha tu clouds walivamiwa na bunduki usiku na watangazaji wakatishiwa kupelekwa jela na kupewa kesi za madawa ya kulevya
Kama kiongozi mwenye dhamana pia agiza jeshi lako likawakate wahusikaa kabla awajafanya kwelii..........la sivyo ulichoandikaa ni drama tuu na amna kitu maana kuna ambaoo uwez wanyooshea kidole japo una mamlaka iyoo
 
View attachment 485970
Mwigulu Nchemba(Kushoto) akizungumza na Nape Nnauye katika ukumbi wa NEC kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma 10/15/2014(Maktaba)

Mh. Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu. Kitendo cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha kiasikari, sio cha kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini.

Nahusika na Usalama wa Raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni Askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake.
======

View attachment 485994

NASHUKURU SANA, KWELI WALIMZALILISHA SANA NAPE, NIMEUMIA SANA KUONA VIDEO HII, HAKUWA NA WA KUMTETEA KABISA, KABAKI KAWEKA MIKONO YAKE MFUKONI NA KUSEMA "WEWE KAMA UNATAKA FANYA FUJO" HII SI HAKI KABISA. TENA BAADA YA KUTOA BASTOLA AKARUDI NYUMA, KUONYESHA YUKO TAYARI KUSHOOT, THIS IS WRONG AND HAS TO STOP!!!!!
 
Baada ya tukio la mtu ana anayedaiwa kuwa ni Askari kanzu kuonekana akimtishia Bastola Waziri za zamani wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo na Mbunge wa Mtama Nape Nnauye February 23, 2017 wakati alipotaka kuongea na Waandishi wa habari muda mchache baada ya taarifa ya Rais Magufuli kufanya mabadiliko ya Wizara aliyokuwa akiiongoza.

Leo March 24, 2017 Waziri wa Mambo ya Ndani, ya nchi Mwigulu Nchemba alitumia ukurasa wake wa Intagram na kusema..’Mh.Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu‘

‘Kitendo cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha kiaskari, sio cha kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini‘ –Mwigulu Nchemba

‘Nahusika na Usalama wa Raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni Askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake‘ –Mwigulu Nchemba
Sawa sawa Mwigulu. Hata kama ukitumbuliwa lakini umefanya kile kilichostahili, regardless of the consequences.
 
Naomba unielewe hatuzuii mtu yeyote kukamatwa wala kuhojiwa wala kukatazwa jambo, nasemea utaratibu wa kuoneshwa bastola hadharani sio kitendo cha kiuaskari na sio kitendo cha Tanzania, hata Lema na Lisu hawajawahi kunyoshewa bunduki. Usichanganye sheria kuchukua mkondo na bunduki kuchukua mkondo.
Mheshimiwa mbona tukio la clouds umepiga kimya sasa Raia tuna hofu na usalama wetu maana twaelekea Somalia sasa.
 
Nchemba hapo kama unajiosha tu.

Isiishie kwa kuwaagiza polisi, inatakiwa uwape masaa wakuletee ripoti, huyo ni nani na kwanini alifanya vile na kama ni askari nani alimpa amri ile, chain of command iliyofanya yale ijulikane, tuone hiyo chain ya command kama ilianzia tokea kwako au ilianzia kati kati.

Bila kufanya hivyo basi wewe ni Waziri husika wa usalama wetu na inabidi ufanye wajibu wako ili tuelewe kuwa na wewe huhusiki kwa Nape kuwa harassed namna ile.

Nnawaza tu, ikiwa mtu kama Nape anafanyiwa vile, sisi wenzangu na mie si tupo mashakani.

Mbwa wa polisi hakamati mtu bila ya kupewa amri, hali kadhalika kwa polisi mwenyewe kama ni polisi.

Tunataka mizizi ya huo ujinga ing'oke.

You can do much better than that kama hautaki nafsi yako ikusute. Otherwise utakuwa ni mnafik tu.
Heeeeh hadi wewe!!
 
Back
Top Bottom