Waziri wa JK ampinga Karamangi...

haya kayasema yeye au kasemewa au spinning yeye hajui ni vipi kukutana na waziri husika kulizungumza, jee vikao vya mawaziri hamna?

mie nnahofia ni udaku tu

Hilo baraza la mawaziri litakaa saa ngapi wakati kila mmoja yuko kiguu na njia?
Labda wafanye Video Conference, ili kila waziri alipo ashiriki.
 
huenda mama kombani alifanya hizo juhudi zote mnazozisema humu
na akagonga ukuta. hivyo ameamua kutoka hadharani.
 
Ukiwa waziri Tanzania ni wazi umewauza wananchi walio kuchagua kinyemela.

Bunge ni nguzo moja ya serikali inayojengwa na wananchi na Baraza la mawaziri ni nguzo nyingine ya serikali inajengwa na rais kwa niaba ya serikali.

Kuukubali uwaziri ni kusaliti uwakirishi wako bungeni. Kwa kuukubali uwaziri unalazimika kuziba masikio na mdomo usikiapo kilio cha wananchi wako.

Ujanja wa kutetea wananchi huku ukiwa waziri ulimshinda Mrema siku nyingi sana akiwa SISIEMU huyu Celina ataweza??
 
Ni kweli junior ministers hawaingii, kwenye full cabinet meetings, lakini still sio sababu ya huyu waziri, kukimbilia kwenye public,

ni kutafuta umaarufu wa short term kwa mgongo wa orodha ya mafisadi!
 
Ukiwa waziri Tanzania ni wazi umewauza wananchi walio kuchagua kinyemela.

Kabisa! Kombani lazima atetee waliomuajiri (wananchi), sio kwa sbabu ni waziri basi akae kimya wananchi wake wakipokonywa mali zao. Huu ndio wajibu wake yeye kama mbunge.
 
Kumbukumbu nzuri sana ..
Humu jf kitu hakipiti ndio raha yake.
Asante kwa kutukumbusha japo kunakundi halitataka kukubali ukweli ndio maana wanapinga mpaka kauli za na kura zao za ndiooooooooooo
 
Karamaghi alitumia hela nyingi sana kwenye kampen za kumwingiza jk 2005 ikulu kwa hiyo kila DILI alikuwa anafukuzia ili kurudisha pesa yake na SAFARI YAKE kwenda kusain kule uingereza ulikuwa uamuzi wake na na hakumuaga mtu isipokuwa LOWASA tu kumbuka waziri ana mamlaka kamili ya kusaini mkataba kadiri anavyoona inafaa
 
Waziri wa JK ampinga Karamagi

2007-10-23 15:55:27
Na Emmanuel Lengwa, Jijini


Wakati Wizara ya Nishati na Madini inayoongwa na Waziri Nazir Karamagi ikidaiwa kutoa uamuzi kuwa mgodi wa Epanko ulioko wilayani Ulanga Morogoro umilikiwe na kampuni moja ya uwekezaji, Waziri mwenzie wa Serikali ya sasa, amepinga uamuzi huo.

Aliyepinga maamuzi yanayodaiwa kutolewa na Wizara ya Bw. Karamagi, ni Bi. Celina Kombani ambaye ni Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Akizungumza na Alasiri kwa njia ya simu leo asubuhi, Bi. Kombani ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki kuliko na mgodi huo wa Epanko, amesema kama kuna uamuzi wa kuipa uhalali wa umiliki kampuni binafsi na kuwaacha wachimbaji wadogo, yeye kamwe haungi mkono jambo hilo.

Akasema Bi. Kombani kuwa msimamo wake, kama mbunge wa wapiga kura wake hao, ni kwamba sheria za nchi zitumike ipasavyo katika kutoa uamuzi kuhusu eneo hilo ambalo limekuwa na mgogoro kwa muda mrefu.

`Msimamo wangu kama Mbunge wa eneo hilo, ni kwamba sheria itumike kumaliza mgogoro huo ? na mwishoni mwa yote, wananchi lazima wapewe haki yao,` akasema Bi. Kombani.

Akifafanua zaidi, Waziri Kombani akasema kuwa yeye yupo upande wa Serikali lakini, wakati huohuo, hawezi kuunga mkono maamuzi yanayowaumiza wapiga kura wake kwa sababu anapaswa kuwajibika kwao.

`Mimi nipo Serikalini na pia nipo kwa wananchi ambao ndio wapiga kura wangu? siwezi kupendelea upande wowote. Ninachoweza kusema ni kwamba hapo inabidi sheria itumike,` akasema.

Akifafanua zaidi, Bi. Kombani amesema wachimbaji wadogo walikuwapo katika eneo hilo tangu zamani na hivyo, anaamini kuwa sheria zikifuatwa vyema, mgodi huo utaangukia mikononi mwao.

Hata hivyo, wakati Bi. Kombani akitoa msimamo huo, inadaiwa kuwa Wizara ya Nishati na Madini imetoa umauzi wa kuumilikisha mgodi huo kwa kampuni moja ya uwekezaji.

Inaelezwa zaidi kuwa, kutokana na uamuzi huo wa Wizara ya Nishati na Madini, wananachi wa eneo hilo wamejikuta wakiwa kwenye mapambano ya mara kwa mara na walinzi wa kampuni husika.

Hatahivyo, imeelezwa zaidi kuwa juzi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Meja Mstaafu Said Kalembo, alilazimika kuufunga mgodi huo kutokana na hali ya eneo hilo kuashiria vurugu na uvunjifu wa amani.

Meja Jenerali Kalembo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya Mkoa huo, alisema mgodi huo utaendelea kufungwa hadi hapo Wizara ya Nishati na Madini itakapotoa ufafanuzi zaidi juu ya mgogoro uliopo



mi nafukua tu
 
Back
Top Bottom