Waziri Ummy: Nimeanza kuona uzembe kwa Watumishi wa Afya, Tutawawajibisha

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,413
8,199
Waziri wa Afya ametoa kauli hiyo baada ya Watumishi 2 wa Afya, Rose Shirima na James Getogo kutoka Zahanati ya Ishihimulwa, Tabora kuonekana wakijibizana kuhusu kutumia Vipimo vya #Malaria vinavyodaiwa kuisha muda wa Matumizi.

Ummy amesema “Nimeona clip Mtu anang’ang’ana kumpima Mgonjwa Malaria kwa kipimo ambacho kime-expire mwenzie anamkatalia, yeye anatoa majibu ya hovyo, mwaka huu tutawajibishana”.

“Nimetoka kumwambia #MgangaMkuu wa Serikali kuna ongezeko la Uzembe, Kutozingatia Maadili, Weledi na Miongozo ya Serikali kwa baadhi ya Watumishi wa Afya, hatutomfumbia macho Mtu, tunataka tuwapate wachache tuwaoneshe mfano ili iwe fundisho kwa wengine”.


 
Huyo Dada nesi ana mdomo mchafu sana, aachishwe kazi mara 1 tena haraka sana, haina haja ya uchunguzi.
 
Mbona kama anaangalia kamera kabisaaa
Au ndio usanii wenyewe?
Tuseme hajui kama anarekodiwa?
Hizi mbinu zimepitwa na wakati
 
Back
Top Bottom