Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,549
SOMO/USHAURI KWA WIZARA YA AFYA NA WAFAMASIA NCHINI KUHUSU OPOTOSHWAJI UNAOFANYWA MAKUSUDI NA BAADHI YA WATAALAM WASIOKUA WAMINIFU.
Na Prof Patrick Koboko(MD,MMED,MPH,MBA, PhD in Human Anatomy)
Wasalaam!
Kwanza nitoe pongezi kwa serikali yangu inavyojitahidi katika kulinda usalama wa afya za wananchi wake hususani waziri wa Afya Ummy Mwalimu kwa jinsi anavyopambana ndani ya wizara ya Afya ingawa bado kuna watu wanaomzunguka wanampotosha kwa makusudi ili kulinda maslahi yao binafsi. Kupitia somo hili, naamini serikali itachukua maoni yangu na kuyafanyia kazi, wataalam wa dawa nao watajifunza hususani wale wanaopotosha umma wa watanzania kwa makusudi kulinda maslahi yao binafsi.
UPOTOSHWAJI WA MAKUSUDI UNAOFANYWA KWA WANANCHI.
Kwanza ifahamike kwamba hakuna chuki baina ya taaluma moja dhidi ya nyingine kwenye kada ya Afya, tatizo kubwa ni baadhi ya Wataalam kwa sababu ya njaa zao au ubinafsi usiokua sababu kutaka kufanya kila kitu kisiasa na kuipotosha jamii kitu ambacho huenda baadaye kikaleta madhara makubwa nchini kwa baadaye.
Nimetoa ushauri sana kwa kuandika humu ndani kama moja ya mtandao pendwa pamoja na mitandao mingine maarufu ya kijamii ambako ujumbe unaweza kuifikia jamii na mamlaka kwa haraka zaidi. Kama nilivyosema siku moja humu kwamba tuna tatizo kubwa sana la mifumo ya elimu yetu nchini, uelewa ni tatizo kubwa sana kwa baadhi ya wataalamu (siyo wote), mfumo tuliojengewa ni ule wa watu kupenda kujipatia vipato kwa njia za mkato na kujitapa kwa sababu wamesoma badala ya kuzalisha, mtu anamaliza shule badala ya kwenda kuzalisha, anafikiria cheti chake kikakae dukani kwa mwenzake ili alipwe pesa anayotaka yeye,hafikirii kwenda kuanzisha hata kiwanda kidogo za kuzalisha dawa ndogo ndogo za baridi au kuingia porini kufanya utafiti wa dawa za kutibu maradhi mbali mbali ili kulinusuru taifa na uagizaji wa dawa kutoka nje. Tunazalisha wanataaluma wazembe wanaowaza kukaa ofisini kupulizwa na viyoyozi badala ya kwenda porini kwenye Magome ya miti huko kutafuta suluhisho la maradhi ambayo yamekua yakiibuka kila uchwao. Hapa ndiko tatizo liliko.
Niwaombe wanataaluma wenzangu hasa wanazuoni wa kada hizi za Afya, tuzalishe wanataaluma wenye kujitegemea na siyo wanaowaza kukaa maofisini kuwaza vyeti vyao kutumika kufungulia maduka ya dawa au vituo vya afya na mahospitali. Tuwe na wataalam wenye tija wanaowaza kuzalisha na kuleta mapinduzi katika sekta ya Afya nchini. Mifumo ya Wanavyofanya kazi watanzania katika sekta ya Afya ni tofauti kabisa na ninayoiona hapa Afrika Kusini na hata Egypt nilikokaa takribani miaka 7 nikiwa mwalimu wa chuo kikuu na mwanafunzi huko.
Wenzetu wamejikita zaidi katika kuzalisha zaidi na siyo kukaa maofisini tu kubishana na kulalama na ndiyo maana dawa nyingi tunaingiza kutoka kwao.
HAKUNA UKWELI WOWOTE WALA HOJA YA KISAYANSI KUA MFAMASIA PEKEE NDIYE ANAYETAKIWA KUUZA AU KUTOA DAWA.
Kama nilivyosema awali ni kweli ndio uhalisia wenyewe ya kwamba Mfamasia anafanya kazi Hosptalini, Kwenye tafiti mbali mbali za dawa, Kiwandani, kua Mwalimu wa chuo kama mimi, Kwenye Godowns na stoo za kuhifadhia Dawa, maduka ya dawa na kwenye jamii pia . Daktari pia anafanya kazi Hosptalini, kua mwalimu wa chuo, Kiwandani, kwenye tafiti mbali mbali mbali, Godowns za kuhifadhia dawa, maduka ya kuuzia dawa na kwenye jamii pia, Muuguzi hali kadhalika. Katika maeneo haya kila mmoja ana jukumu lake kulingana na kuhitajika kwake.
Juzi tu tulikua kwenye utafiti wa Chanjo ya ugonjwa wa Corona, utakubaliana nami kua kulikua na madaktari wengi ndio na Wafamasia ndio wanaohangaika sana kwenye ugunduzi wa dawa na chanjo na dawa ya gonjwa hili, jiulize ni kwanini timu za madaktari na wafamasia ndizo zilikua mstari wa mbele kuhangaika juu ya dawa na chanjo ya gonjwa hili? Na bado utafiti unaendelea. Kwahiyo kazi bila team work haiwezi kwenda.
Nilisema ni ubinafsi mkubwa na ni upotoshwaji mkubwa unaofanywa na wachumia tumbo wachache katika taaluma ya Famasia nchini na wamefanikiwa kumpotosha hata waziri kua Wafamasia pekee ndio wanaopaswa kuuza dawa.
Kwanini wao tu ndio wanaotaka wakae madukani wauze dawa wakati hata mahospitalini tunafanya kazi na wao pamoja? Kwanini kwenye maduka nako tusifanye kazi as a team? Kuna sababu yeyote kimsingi au kisayansi kumzuia daktari au nesi kuuza dawa ikiwa yeye ndio amechagua kukaa kwenye duka la dawa badala ya kufanya kazi hospitani. Kila mtu anafanya kazi kwa choice yake, kuna Mfamasia anapenda afanye kazi hospitalini na mwingine kiwandani au kwenye maduka ya dawa, hali kadhalika kwa daktari na nesi hivyo hivyo, kuna shida pia kufanya kazi kama team kufanya kazi kwenye maduka?
Mnajua kua kwenye viwanda vya dawa wanafanya kazi as a team kama ilivyo kwa hospitali kama ambavyo mimi niliwahi kufanya kazi kwenye kiwanda kimoja cha dawa huko Tanzania nikiwa daktari? Wafamasia wachache waache ubinafsi na shida zao binafsi kuipotosha serikali na umma kwa ujumla.
NI MADUKA MANGAPI YANATOA DAWA ZINAZOHITAJI VYETI VYA MADAKTARI NCHINI?
Labda nimwambie Mhe Waziri Ummy kama alikua hajui, ni 99% ya maduka ya famasi nchini ambayo sheria inayataka yatoe dawa zinazohitaji maelekezo ya daktari (Dr's Prescriptions) hayafanyi hivyo. Kama ninadanganya atume timu yake ya siri kufanya uchunguzi huo kama hawatafungia maduka yote nchini. Kulaumu kua wauza dawa wasiokua wafamasia ndio wanaoharibu utaratibu huu na kuingiza afya za watanzania matatatani siyo kweli, Zile video clips zilizokua zikisambazwa mitandaoni kuonesha kuna watoa dawa hawana taaluma zilikua ni propaganda zilizoanzishwa na Wakaguzi wachache wachumia tumbo na ndiyo maana utaona hazikuowaonesha waliokua wakihoji maswali, wafanye uchunguzi wajionnee waache kupotoshwa na wachumia matumbo wachache, kabla sijaja kuandika humu nikiwa nchini nilifanya utafiti huu na hata sasa kuna vijana wangu walioko huko Tanzania wakifanya uchunguzi juu ya hili ili ninapotoa ushauri niseme vitu vya ukweli na uhakika.
SWALI1). Kama kwenye famasi mgonjwa ameenda kununua dawa kali yenye uhitaji wa cheti cha daktari na hana cheti hicho, atamhudumia au atamrudisha hospitali akaandikiwe na daktari kisha arudi dukani? Atawezaje kumhudumia wakati yeye siyo daktari na hawezi kuandika prescription?
Maana kuna hoja ya Kijinga hapa kua Mfamasia anaweza kuandika prescription kwa sababu anaweza kuisoma ile ya daktari eti kwa sababu amesoma Anatomy, Physiology, Pathology na Pharmacology na dio Upotoshaji mkubwa inakoanzia hapa.
Daktari ama tabibu Pathophysiology au history taking kwake ni masomo yanayojitegemea na yana principles na utaratibu wake achilia mbali Physiology na Anatomy au Pathology. Mfamasia anajua maana ya Main Complain, HPI na SOCRATES? amesomea wapi kama kuna mwenye kuthibisha hili aseme humu humu.
(2) .Kama waziri anashauriwa Wafamasia ndio wanaotakiwa kukaa mpaka kwenye maduka ya dawa muhimu ama DLDM ambayo hayahitaji cheti cha Mfamasia wala cheti cha daktari, ni kwa msingi upi sasa wakati dawa zenyewe hazihitaji Mfamasia wala cheti cha daktari?
Kama daktari au muuguzi aliyesomea kozi yake akafuzu vyema anauza DLDM, tatizo liko wapi hasa?
Kwanini tunaweka urasimu na siasa kwenye mambo muhimu kiasi hiki?
NI MADUKA MANGAPI YA DAWA TANZANIA WAFAMASIA HUBAKIA DUKANI MUDA WOTE WA KAZI?
Toka awali nilisema kwamba upotoshaji wa makusudi ukiendelea, kuna mambo yasiyosemwa tutaweka hadharani ili kusudi watanzania wajue nini kinajiri kwenye maduka haya ya dawa na ni kwa nia njema wala hakuna chuki hapa. Kila mtanzania ana haki ya kukinda afya ya mwenzake....
Ni 99.99% Tanzania ya maduka ya dawa ambayo yanatakiwa kusimamiwa na wataalam wa dawa wenye viwango vya elimu kuanzia na shahada ya kwanza hawakai kwenye maduka hayo kama sheria inavyowataka. Wanalipwa pesa nyingi ambazo hazikatwi Kodi kuanzia na milioni moja(1,000,000+) na kuendelea. Kama wizara ilikua hailijui hili basi wafanye uchunguzi wataelewa tu. Nchi inalia na mapato lakini kuna watu wanapokea pesa taslim bila makato ya kodi wakati kila mfanyakazi nchini, ni lazima na ni sheria kwa kila mfanyakazi kukatwa kodi. TRA na wizara ya fedha waliangalie hili serikali inapoteza pesa nyingi sana. Hata kama wanalipia leseni zao lakini taaluma zingine zinalipa vile vile na linapokuja suala kulipwa kwa kufanya kazi kodi ni lazima kwa taratibu za nchi yetu.
Ukaguzi wa kina wa Wizara ya Afya, Wizara ya Fedha na TRA kwa ujumla.
Kama nchi nzima ina wafamasia zaidi ya 1000 wenye level ya degree wanaosimamia maduka ya dawa na wanalipwa mishahara yao bila kukatwa kodi, ni kiasi gani taifa linapoteza kwa mwaka badala ya kuhangaika na tozo hizi ambazo zinaumiza zaidi watu wa chini?
KATI YA BARAZA LA WAFAMASIA NA TMDA NI NANI ANATAKIWA KUKAGUA DAWA NCHINI?
Huu nao ni mkanganyiko mkubwa sana Tanzania na Waziri anapotoshwa makusudi tu kwa vile labda siyo Mtaalam wa Afya maana wakati Wizara inaongozwa na Waziri mtaalam hatukuona haya, sijajua kazi ya Naibu waziri na Katibu mkuu ambao ni wataalam kwanini hawatoi ushauri huu kwa waziri.
Duniani kote, FDA au TMDA kwa kwetu Tanzania hizi ndizo taasisi pekee zinazotakiwa kukagua usalama wa dawa kisheria na taasisi hizi ndani yake utakuta kuna Wafamasia, Madaktari, Wauguzi, Wakemia, wataalam wa lishe na wataalam wengineo mpaka wanasheria kila mtu na eneo lake katika utendaji wake, and this is according to international standards, kwa Tz sijui kuna tatizo gani ndugu zangu hii kazi wanapewa Baraza la Wafamasia (Pharmacy council) ambalo hili ni baraza la kitaaluma ambalo kimsingi kazi yake ni kusajili wataalam na kuwapatia leseni za kazi, yaani sawa na kusema MCT au TANNA wafanye kazi za kukagua mahospitali ili hali haya ni mabaraza ya kitaaluma na yana kazi zake za msingi, labda wapitie kukagua leseni na vyeti vya wataalam wao waliowasajili. Sasa huku Tanzania Baraza la Wafamasia ndio wanakagua dawa, wanasajili Maduka ya dawa, huku wanasajili wataalam, yaani mambo Changanyikeni. Kama watapita kwenye kwenye maduka ya dawa na mahospitalini au viwandani kukagua leseni za wataalam hapo sawa maana kuna zinazogushiwa na ziingine kumalizika muda wake.
USAHURI wangu kwenye hili ni kwamba kazi ya kutoa vibali vya kufungua maduka ya dawa pamoja na ukaguzi wa madawa na maduka waachiwe TMDA ambao ndio kazi zao kimsingi na kama wataalam hawatoshi Wizara iajiri tu taasisi itimie na ifanye kazi kwa weledi waache kufanya mambo kienyeji. Baraza la Wafamasia ni Baraza la kitaaluma liachwe lifanye kazi zake za kimsingi ambazo ni kusajili wataalam, kuwapima na kuwapatia leseni za taaluma hiyo, wakague pia lesini zao ikiwa ni za kweli au bado ni valid.
HITIMISHO: Naiomba sana Wizara ya Afya na Mamlaka zizingatie za serikali ushauri huu ni muhimu sana, kuna upotoshwaji mkubwa unaofanywa na baadhi ya wataalam wanaokiuka maadili yao ya kazi. Tunapoteza pesa nyingi sana na umakini katika eneo hili muhimu ambalo liliachwa nyuma muda mrefu.
Ni ushauri pia kwa wataalam wa kada za Afya zaidi Wafamasia wazingatie, tuache kufanya kazi kwa mazoea, tuzingatie maadili ya kitaaluma. Tuzalishe ili taifa letu kidonge mbele.
Mimi sijikwezi na wala sina tatizo na taaluma ya mtu, naziheshimu taaluma za watu wengine na ndio tunaofanya kazi kwa pamoja kama timu ili kulinda afya ya jamii kama viapo vyetu vinavyotaka.
Ahsanteni!
Prof Partick Koboko(MD,MMED,MPH,MBA, PhD in Human Anatomy)
kobokopatricdr@gmail.com