Waziri Ummy: Deni kubwa la matibabu ya nje lililoibuliwa na CAG halihusu Serikali ya Magufuli tu,ni malimbikizo ya nyuma

Maana kuna uwezekano mtu akaondoka hapa kama kiongozi wa serikali,anasema anakwenda kutibiwa moyo,lakini kumbe anakwenda kupata huduma ya kupandikiziwa mimba sababu ya matatizo ya uzazi,kitu ambacho katika "packages" ya matibabu yanayofadhiliwa na serikali nje ya nchi,hili la kupandikizwa mimba sio sehemu ya "packages" hizo.
Baada ya kupokwa majukumu yake ustawi wa jamii na kusimamia watoto na kina mama waliotelekezwa naona sasa ni payback time..
 
Kupandikizwa mimba hili si deni la yule mkuu wa mkoa?


Ukisoma maneno ya waziri kama kweli wamemnukuu sahihi, ni kama serikali ya Tanzania ya sasa ni mpya haihusiani na serikali zilizopita.

Wafanyakazi karibu wote waliwakuta, magari na vyote vilivyomo wamevikuta iweje leo wanaanza ubaguzi haya ya kwetu tuulizwe yale ya waliopita,

Kuwepo kwa deni sio kosa mkakati wa ulipaji ndio shida au na huku mmeshindwa kuhakiki. Maana tumezoea kusikia madeni ya walimu na wafanyakazi wa umma tukimaliza kuhakiki tutalipa.

Its time kwa serikali kufanya kazi kama serikali badala ya kunyooshea wengine vidole.

Kama kuna deni kubwa lilipwe mbona Bombadier ambayo ilishikiliwa kwa deni la watu wengine mmelipa?
 
Kuna wakati unapata hasira unatamani kutukana kabisaaa, hvi hii Serikali ishatuona sisi vilaza kama alivyotuita yule bwana, halaf pia CAG hajui kazi yake kiasi kwamba atuletee vitu vya enzi ya JK,nyambafu zenu nyie
 
Mbona umeshikia sana bango hili swala, hapa ndipo unapopatia ujira wako nini? Mbowe & Co. wanaiba Mabilioni wengine mmekalia kumpigia makofi, achaneni na Raisi na Serikali yetu, you can go hang!
ndugu yangu 1.5. trillion ni nyingi mno, usizibeze kauli ya kutaka kujua zilipo, zikipatikana zitatusaidia wote bila kujali itikadi ya vyama au dini, kumbuka bunge la MAMA makinda, lilivuka ukomo wa muda hadi saa tano usiku, tukipigania tsh bilioni 321, tena hazikua za hazina zilikua za TANESCO. Tutaachaje kutaka kujua trillion Moja na nusu, ambayo sawa na tsh billion 1500? Yani inaingia mara nne na nusu ya ile hela ya Tegeta escrow tsh Bilon 321
 
ii kujibujibu ni kutaka kusema hii serikali haina wezi??Kwanini wanavunja utaratibuuu?Halafu kila mtu akija anasema "Sehemu kubwa ya hii report ya CAG ni ya miaka ya nyuma,hadi July 2017,lakini baada ya hapo,serikali ya awamu ya tano imebadilisha sana mambo".Kwanini wanaitoa serikali ya Awamu ya Tano katika hizi tuhuma za CAG.
Ni upuuzi tu unaendelea .................!! Ila njia ya muongo ni fupi!!?

Kama hayo madeni yalikuwepo mbona hayakuonekana kwenye report ya CAG ya 2015/16!?

Anyway, tatizo kubwa ni zile 1.5 Trillion zilivyotumika au zilivyoyeyuka!!? Naona hakuna anayejitahidi kuzitolea maelezo. Mpango kaamua kumtumbia Home Boy Tumbili asaidie ku counter attack!!
 
ndugu yangu 1.5. trillion ni nyingi mno, usizibeze kauli ya kutaka kujua zilipo, zikipatikana zitatusaidia wote bila kujali itikadi ya vyama au dini, kumbuka bunge la MAMA makinda, lilivuka ukomo wa muda hadi saa tano usiku, tukipigania tsh bilioni 321, tena hazikua za hazina zilikua za TANESCO. Tutaachaje kutaka kujua trillion Moja na nusu, ambayo sawa na tsh billion 1500? Yani inaingia mara nne na nusu ya ile hela ya Tegeta escrow tsh Bilon 321


Hata iingie mara 1000, nchi yetu iko chini ya Raisi wetu makini hakuna kitakachoharibika!
 
Leo tena waziri wa Afya bi Ummy Mwalimu ameendelea "kujibu" report ya CAG.Waziri Ummy anasema eneo la deni la matibabu ya nje lililotajwa na CAG sio la awamu ya Tano,bali ni mrundikano wa madeni ya miaka ya nyuma,na hivyo serikali ya awamu ya tano isibebeshwe kana kwamba deni hilo limepatikani ndani ya miaka miwili ya uongozi wa awamu ya Tano.

Duh hawa mawaziri, hatari tupu... Hivi anataka kusema kuwa "Mkuu wa malaika" atalipa madeni yote anayokopa kabla hajatoka madarakani!!!??
 
Back
Top Bottom