Waziri Tizeba analala hoteli mpaka leo kwa kodi zetu

saimon111

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
1,736
1,351
naomba niwashirikishe hili ndugu zanguni maana sidhani kama watanzania wanatendewa haki na kodi zao.

naibu waziri wa usafirishaji, Bwana. CHARLES TIZEBA, mpaka juzi ilikua ni siku yake ya 247 anaishi hotel ya NEW AFRICA HOTEL & CASSINO iliyopo posta tangu alipopewa uwaziri 4 may 2012.

katika hotel hiyo kuna vyumba vya $160, $180, na $300 kwa usiku mmoja tu. waziri huyu analala chumba cha $300 ambacho kapewa kupunguzo na anakilipia $250 kwa kuwa ni mteja wao wa kila siku sasa, gharama hiyo anayolipiwa na serikali ni nje ya chakula cha mchana na usiku.....

sijaishia hapo pia familia yake ikija kumtembelea ambayo huwa inakuja mara kwa mara na inakaa hotelini hapo sio chini ya wiki moja tena kwenye vyumba vya $160 (discounted $150) hapa pia huwa serikali ndio inalipa hizo gharama.

mpaka juzi gharama za chumba tu zimefikia $61,750 ambayo ni sawa na millioni 98 za kitanzania.

CONCERNS
hivi nyumba zote hapa dar es salaam serikali imekosa kabisa kumpangishia huyu bwana mpaka akalale hotel ya kifahari as if ni nyumbani kwake....?

source: The Guardian, on sunday january 13
 
Kosa ni kuuza nyumba za Serikali bila kujali mambo kesho.Vinginevyo nyumba zijengwe zingine kila mwaka kwa zaidi ya idadi iliyouzwa kwa Watumishi wa Serikali .

Nyumba ziliuzwa kwa watumishi ambao wala hawakuwa na shida ya nyumba.,sasa wengine wanapata tabu kwa sababu ya maamuzi mabovu ya watawala.
 
We una uhakika jamaa analala hapo kila siku? Isije ikawa jamaa amepangisha nyumba anaishi ila anaendelea kula pesa za wadanganyika.

Mpaka tushtuke hii nchi itakuwa imebaki matobo matobo tu.
 
Hayo ndo matunda ya Magufuri, Mkapa na chama cha Majambazi CCM OYEEEEEEEEEEEEEEE. Na hii dhambi haitawatoka jadi kizazi cha mwisho katika uzao wenu magamba.
 
Ndio maana watanzania tunatakiwa kuikataa kwa nguvu zote hii serikali ya CCM. Wao hawana mpango na COSTS wanazotumia, no costs control at all. Tunaolipa kodi inatuuma sana, hatuna sauti na hela yetu ya kodi na wanaotakiwa kututetea ndio watafunaji wakubwa. Tena hapo unaweza ukakuta Hotel haijalipwa hata senti tano hela yote hiyo ni deni, na hii serikali inadaiwa Trillion 22 zingine kwa matumizi haya ya kipumbavu. Hivi kweli hakuna muda specific wa mtu kukaa hotelini anapoanza kazi?
Je mawaziri wangapi wanaokaa hotelini?

Anafanya matumizi hayo yote lakini pale jimboni kwake Nyakaliro kituo cha afya hakina hata Panadol wananchi wanaambiwa wakanunue. Please mtanzania say no to CCM, this is too much.
 
Mambo kama haya ndiyo tunataka akina Mwigulu na Nape watupe majibu na sio issue ndogo ndogo na nyepesi kama za nani anamiliki kadi ya chama kipi! huu ni ufisadi tu sasa huyu ni mmoja wapo wengi sana yaani kwa ujumla kunamatumizi yasiyo ya lazima katika serikali hii. tukiweza kudhibiti matumizi haya tunaweza kutoa huduma za elimu na afya bure tena za kiwango cha juu tu.
 
Sijui mtu usingizi unampata vipi kwa ufujaji wa jinsi hii wa fedha za umma! Dar yote hiyo kweli hakuna nyumba ya hadhi yake ikapangishwa? Haiwezekani!.
 
Hivi walipata wapi wazo la kuuza nyumba za serikali kama mahitaji bado yanaonekana hata na asiyeona kuwa yapo? Na juzi juzi tu si mheshimiwa kazindua ujenzi wa nyumba za serikali? Kwa hiyo ndio mwondoko wa kula matapishi yao wenyewe?

Ama wanatuchosha.....
 
Nyie mnaolipwa ujira kwa kutetea chama cha mabwepande! a.k.a ccm hapa jamvini njooni basi mkamilishe kazi ya siku!Alah! ngoja ni PM Nepi hasionekane mtu rumumba leo jion.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom