Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,903
- 945
WAZIRI TABIA MWITA AMSHUKURU DKT. MWINYI KWA KOMBE LA CECAFA U15 KUTUA ZANZIBAR
Mabingwa wa CECAFA U15, Karume Boys wametua nyumbani Zanzibar wakitokea nchini Uganda na ubingwa wao walioupata kwenye michuano ya CECAFA U15 Boys Championship.
Karume Boys wamepokelewa na Makamu wa Pili wa Rais, Mhe. Hemed Suleiman, Waziri wa Michezo, Mhe. Tabia Mwita, Mkuu wa Mkoa, Mhe Idrisa, viongozi mbalimbali, Wazazi na wadau wa soka visiwani Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais, Mhe Hemed Suleiman, Waziri wa Michezo, Mhe Tabia Mwita, Mkuu wa Mkoa, Mhe. Idrisa wamepata bahati ya kuwa viongozi wa kwanza kubeba kikombe cha ubingwa wa CECAFA U15 kilicholetwa na vijana wa Karume Boys.
Karume Boys wameletwa na Ndege maalum iliyotolewa na Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambayo imewafikisha vijana wa Karume Boys nchini wakitokea Entebbe, Uganda.