Waziri Simbachawene: Tunapozungumzia kinga kwa Usalama wa Taifa, tunazungumzia kinga dhidi ya Ugaidi

HIMARS

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
69,366
94,547
Waziri George Simbachawene akitoa ufafanuzi kuhusu kinga kwa maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa kama ilivyoelezwa kwenye Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa wa Mwaka 2023.

Tayari Bunge limepitisha muswada huo na sasa utapelekwa kwa Rais kwa ajili ya kusainiwa. Kazi kwenu

NB: Hata wa bandari nao utapitishwa hivi hivi.


 
Kesho utaskia inapitishwa na sheria ya kinga kwa askari polisi, ili watumalize kabisa!

Hii nchi wabunge akili zao zipo makal*oni. Walikua wanalalamika huko huko bungeni kuwa wanafatiliwa na gari/watu wasiojulikana sambamba na wengine wakilalamika wanapigiwa simu za vitisho na watu wasiojulikana.

Halafu leo wanawapa kinga ya kisheria hao hao watu wasiojulikana?
 
Sasa hivi miili haitookotwa kwenye viroba tena. Itatupwa ovyo maana wana kinga. Mungu tusitiri na janga la uongozi wa hii nchi kwa sasa. Pitisha shani yako kwa kutuondolea kwa amani wale wote wenye nia ovu na taifa lako.

Warestishe in peace kila wenye mikono yao katika udhalimu na ukandamizaji wa nchi hii ikiwemo wauza bandari pia.
 
Kwani kwenye sheria iliyorekebishwa imefafanuliwa kama Waziri anavyofafanua? Ndugu zangu, utii wa Katiba ni mashakani sana kwa sababu nchi hii imekuwa sasa mtu mmoja ndiye Katiba na mamlaka juu ya katiba.

HIvi mmewahi kuwaamini CCM kiasi gani?

CCM lini imewahi kuwa na lengo zuri?

Mbowe alishtakiwa kwa ugaidi kumbe angeweza kufyatuliwa ikasemwa ni bahati mbaya.

Mungu aifute CCM tuanze upya kama nchi
 
kila mtu ana kinga, ili akitufanyia mabaya sheria imlinde, sijui tukimbilie wapi.

Watu wenyewe tunawaogopa tangia hapo, halafu wanajiwekea kinga, sa inakuwaje?
 
Sasa hivi miili haitookotwa kwenye viroba tena. Itatupwa ovyo maana wana kinga. Mungu tusitiri na janga la uongozi wa hii nchi kwa sasa. Pitisha shani yako kwa kutuondolea kwa amani wale wote wenye nia ovu na taifa lako.
Warestishe in peace kila wenye mikono yao katika udhalimu na ukandamizaji wa nchi hii ikiwemo wauza bandari pia.
amen
 
kila mtu ana kinga, ili akitufanyia mabaya sheria imlinde
sijui tukimbilie wapi
watu wenyewe tunawaogopa tangia hapo, halafu wanajiwekea kinga, sa inakuwaje
ofcourse, kila mtu ana kinga. sijajua specifically kinga hiyo ni kwenye suala gani hasa, manake hata polisi akipiga na kuua kama hajatumia excessive force na kama ilikuwa lazima kujilinda n.k, ana kinga, na raia pia hivyo hivyo. sasa hicho wanachokilinda kwa tiss sijui ni nini though najua pengine wanaweza kuwa na good intentions.
 
Back
Top Bottom