Waziri Mwigulu: Dola sio hela yetu kwani hatuizalishi wala Hatuprint. Tuna akiba ya Dola Bilioni 5.2

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba amezungumzia kuhusu Mjadala wa Dola kuadimika unaoendelea Nchi.

Amesema watu inabidi watambue kwamba Dola sio hela yetu bali tunaipata pale tunapopata Mkopo, Msaada, tunapouza bidhaa ama Huduma nje ya Nchi ndo tunapata Dola.

Sera za kifedha za Marekani kukabiliwa na mfumuko wa bei fedha wamezirudisha fedha ndani ya Central Bank yao Marekani.

Sababu za ndani zinazofanya dola ziadimike ni Matumizi. Matumizi yake yamekuwa makubwa.

Mitambo tunayojengea Bwawa la Mwalimu Nyerere vinanunuliwa kwa Dola, Ujenzi wa Reli Mitambo yake vinanunuliwa kwa Dola, Mikopo yetu tunalipa kwa Dola.

Kwahiyo Dola inatumika sana kuliko vitu vinavyotuletea Dola.

Wafanyabiashara wa hapa, wanapopeleka bidhaa nchi za jirani hawapewi dola. Kwa sasa Sisi tuna Dola Bil 5.2 kuwazidi wenzetu.

Ukame wa dola upo pote. Hii akiba hatuitoi sababu ndo tunalipia deni ili tusije tangazwa tumefilisika

Til 11 tunalipa kwa Mwaka deni la Taifa.

Watu wanadhani ni kazi ya benki kuu kutoa dola. Dola wanapatiana kwenye soko. Mara ya mwisho Benki kuu imetoa dola 2012 hadi 2022 baada ya Uviko. Baada ya Uviko Ilikuwa inatoa Mil 500.. Kwa Sasa tunatoa Milioni 10 na bado haitoshi sababu uhitaji ni mkubwa kila sehemu.

 
Majibu ya Mwigulu kuhusu dola kuadimika,
1. Dola sio hela yetu.
2. Marekani wamezirudisha kwenye central bank.
3. Matumizi yake ya ndani yamekuwa makubwa ndio maana zimeadimika.
4. Mitambo tunanunua kwa dola.
5. Mikopo yetu tunalipa kwa dola.
6. Wafanyabiashara wakiuza nje hawapewi dola.
Yaani hawa jamaa wameshaachana..ila muda utaendelea kusema.

Walivamia nchi kwa mbwembwe na mashauzi..wakataka kupendwa na kuonekana wao wazuri..wakataka kufurahisha kundi la wachache. Sasa wamebaki peke yao..wanazidi kuadhirika..sasa wanatafutana kila kona. Mugambo wanaruka na kukanyagana.
 
Kwani hatujuwi dola siyo yetu?! The guy is a twat and a prick!

Kuna vijiswali vidogo..

Royal Tour kumbe ilikuwa maigizo?

Alizoacha JPM mnadai zimelipa madeni au?

Madini, Tanzanite, Gold, etc etc hela zimeenda wapi?

Tuliwaasa muache mbwembwe za kusafiri, kununuwa ma V8, na ujinga mwingi wa kutumia hela kama vile tunazo, mkakataa kubana matumizi na kujifanya mama kafunguwa maakaunti na nchi mko wapi Sasa?

Jinga kabisa Hawa...
 
Sas si tuliambiwa mauzo ya nje yameongezeka?
Si tuliambiwa watalii wameongezeka?
Si tuliambiwa dola zimemwagika kutokana na watalii na utalii kuongezeka kwa kasi kutokana na royal tour?

Kwa hiyo sababu ya hela kupotea inatokana na kutoiprint? Kwa hiyo ingekuwa yetu tungeprint tuu?

Kwani ujenzi wa bwawa la umeme na hayo yote yameanza mwaka huu?
 
Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba amezungumzia kuhusu Mjadala wa Dola kuadimika unaoendelea Nchi.

Amesema watu inabidi watambue kwamba Dola sio hela yetu bali tunaipata pale tunapopata Mkopo, Msaada, tunapouza bidhaa ama Huduma nje ya Nchi ndo tunapata Dola...
Mwigulu anaongea porojo hana sababu zenye mantiki.

Hao wakubwa pesa zao ziko interms of dollars wanafurahia tu hata inapopanda.

Mabadiliko ya thamani ya shilling ya Tanzania kulinganisha na Dolla ya Marekani Toka Mwaka 1966
NYERERE
(1966-1972) 1 USD = 5 TZS,
(1973-1975) 1 USD =7 TZS,
1976,,1 USD=12 TZS
1977, 1 USD =12 TZS
(1978-82)-1USD-20TZS
1983- 1USD:22 TZS
1984-1 USD: 23TZS
1985- 1USD: 102 TZS
====================
MWINYI
1986- 1USD: 205 TZS
1987- 1USD: 207 TZS
1988- 1USD :220 TZS
1989- 1 USD: 226 TZS
1990- 1 USD: 265 TZS
1991- 1USD: 300 TZS
1992 - 1 USD: 385 TZS
1993- 1USD: 434 TZS
1994-1USD: 465 TZS
====================
MKAPA
1995 - 1USD: 500 TZS
1996- 1USD: 580 TZS
1997- 1USD : 665 TZS
1998- 1USD: 720 TZS
1999-1USD : 800 TZS
2000- 1USD: 820 TZS
2001- 1USD : 880 TZS
2002- 1USD : 900 TZS
2003- 1 USD: 900 TZS
2004- 1 USD: 910 TZS
2005-1USD : 1050 TZS
====================
KIKWETE
2006- 1 USD: 1100 TZS
2007-1 USD: 1150 TZS
2008- 1USD : 1200 TZS
2009 - 1USD: 1250 TZS
2010- 1 USD: 1260 TZS
2011- 1USD: 1300 TZS
2012- 1USD =1450 TZS
2013- 1USD=1620 TZS
2014- 1USD= 1650 TZS
2015- 1USD = 2210TZS
====================
MAGUFULI
2016- 1 USD= 2200TZS
2017- 1 USD= 2310 TZS
2018-1USD =. 2300 TZS
2019- 1USD = 2320 TZS
2020- 1USD= 2323 TZS
2021- 1USD= 2340 TZS
====================
SAMIA
2022- 1USD= 2410 TZS
2023- 1USD =2487 TZS
 
Waziri mwenyewe wa fedha hana ubunifu. Wenzake wanajipeleka karibu na brics kununua mafuta kwa hela zao urusi.

Kuna fursa ya kufanya biashara bila dola na mataifa kama Uchina India Urusi ila wanajikita kwenye mfumo chakavu wa kinyonyaji wa kutegemea dola maana vigogo ni wajinga au wana maslahi.
 
1. Amesahau ziara za Rais nje ya nchi zisoisha na wasaidizi wake wanaotumia dollar .

2. Magari ya kifahari ma v8 ya makatibu wizara, wabunge, Dcs, Rcs, Katiba tawala, wakurugenzi nk yanaagizwa Kwa dollar.

3. Petrol inaagizwa Kwa dollar.

4. Madini yetu yanatoroshwa Kila kukicha na watoroshaji hawalipi dollar nknk nk.
 
Majibu ya Mwigulu kuhusu dola kuadimika,
1. Dola sio hela yetu.
2. Marekani wamezirudisha kwenye central bank.
3. Matumizi yake ya ndani yamekuwa makubwa ndio maana zimeadimika.
4. Mitambo tunanunua kwa dola.
5. Mikopo yetu tunalipa kwa dola.
6. Wafanyabiashara wakiuza nje hawapewi dola.
Yaani hawa jamaa wameshaachana..ila muda utaendelea kusema.

Walivamia nchi kwa mbwembwe na mashauzi..wakataka kupendwa na kuonekana wao wazuri..wakataka kufurahisha kundi la wachache. Sasa wamebaki peke yao..wanazidi kuadhirika..sasa wanatafutana kila kona. Mugambo wanaruka na kukanyagana.
.bado ajasema😂😂😂😂 ana hoja nyepesi sana
 
Back
Top Bottom