Waziri Mwakyembe tizama na huku pia

FILOMBE

Member
Mar 2, 2012
27
0
Habari wana JF. Nimekuwa nikifuatilia utendaji wa mawaziri katika serikali ya Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, ni ukweli usiopingika kwamba waziri mwenye dhamana ya uchukuzi Mh. Dk Harison Mwakyembe ni miongoni mwa watendaji bora kabisa wenye uwezo wa kuchukua maamuzi pale inapohitajika. Ni ukweli uliodhahiri kwamba mzee huyu anachapa kazi.

Kwa leo naomba nimkumbushe Mh. Waziri Mwakyembe kutizama pia upande wa uchukuzi wa abiria hasa katika miji mikubwa kama DSM, Arusha, Mbeya na Mwanza.

Ukutizama wakati wa asubuhi na jioni katika vituo vya daladala utatambua kwamba bado upande huu haujatizamwa vema, kwani wananchi na umma wa Watanzania una pata taabu na adha ya usafiri. Abiria ni wengi sana katika vituo wakati wa asubuhi na jioni kutokana na uhaba wa huduma ya usafiri wa umma.

Hivo rai yangu kwa Mh. Waziri afanye maamuzi mengine magumu na mazuri yenye manufaa kwa Watanzania kama alivofanya kwa kufufua Reli kusafirisha wakazi wa maeneo mbali mbali Dsm. Tengenezeni mazingira yatakayochochea wawekezaji wengi kujitokeza na kuwekeza katika usafiri wa umma.

Ahsanteni.
 
Back
Top Bottom