Fidel80
JF-Expert Member
- May 3, 2008
- 21,947
- 4,446
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda leo(Ijumaa,Septemba 12,2008)anatarajiwa kuanza ziara ya siku 10 katika wilaya ya Mpanda,mkoani Rukwa ambako atakagua shughuli mbalimbali za maendeleo.
Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo,mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga,Waziri Mkuu atakwenda hospitali ya mkoa ambako atapokea vifaa mbalimbali vilivyotolewa na kampuni ya VODACOM na kisha kuelekea Mpanda.
Katika ziara hiyo,Waziri Mkuu atahutubia mikutano ya hadhara wilayani Mpanda katika maeneo ya Inyonga,Ilunde,Mapili, Nsekwa na Urwira.Maeneo mengine atakapohutubia wananchi ni Itenka A,Mamba,Igalukilo,Majimoto,Mwamapuli,Ilalangulu na Karema.
Kazi kubwa ambayo Waziri Mkuu atafanya katika ziara hiyo ni kukutana na kuzungumza na viongozi wa Kata katika kata zote za wilaya hiyo ili kuhimiza kilimo cha kisasa na ufugaji wa kisasa. Katika vikao hivyo,pia atakutana na wazee wa CCM wa kila kata.
Kazi nyingine za maendeleo atakazofanya Waziri Mkuu wakati wa ziara hiyo ni kukagua ujenzi wa sekondari za Ilunde na Utende,kupanda miti maeneo kadhaa,kuzindua bweni la wasichana sekondari ya Karema,bweni la wavulana sekondari ya Usevya na kuweka jiwe la msingi katika jengo la upasuaji kituo cha afya cha Mamba.
Vilevile atazindua Mradi wa Ugawaji wa Vyandarua huko Kashaulili kabla ya kwenda kuzindua nyumba za walimu Stalike.Atafanya majumuisho ya ziara hiyo Jumamosi,Septemba 20,2008 katika Ikulu ndogo wilayani Mpanda.Jumatatu Septemba 22,2008 anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Mkoa(CCM)utakaofanyika ukumbi wa Libori Centre, mjini Sumbawanga.Anatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam siku hiyohiyo.
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
DODOMA 11/09/2008