Breki sina
Member
- Jun 3, 2013
- 96
- 31
Bungeni Dodoma kupitia maswali ya papo kwa papo kutoka kwa Mh Ally mohamed ameuliza kuwa hivi karibuni viongozi wa kitaifa wameonekana wakilalamika kuwa Ufisadi ni tatizo kubwa,huku waziri mkuu akisema kuwa sio kulalamika kwa viongozi bali ni kuwakumbusha wananchi kuhusu tatizo hilo,huku akisema kuwa serikali haijamfunga mikono Dr.Hosea, hakika serikali hii haiwezi kupambana na ufisadi nchini nchi hii.
Soma sheria ya kitu
husika ndipo utoa hoja.Kwa
kukusaidia, Katika sheria namba
11 ya 2007 ya PCCB , Kifungu
cha 5 (2) sheria inatambulisha
kuwa PCCB ni chombo huru. Ukisoma kifungu cha 15 (1), (a)
& (b) utakuta panaelezewa
makosa madogo madogo ya
rushwa yasiyo ya maandishi au
mikataba ambapa Mkurugenzi
PCCB anaruhusiwa kupeleka mahakaman moja kwa moja na
kifungu cha 15 (2) ni Adhabu -
faini kati ya tshs 500,000/- na
1,000,000/- AU kifungo jela kati
ya miaka 3 na 5. AU vyote
kifungo na faini. Ukisoma kifungu cha 16 (1) (a)&
(b) na vifungu vingine vingi
siweza andika vyote, kinaelezea
makosa ambayo Mkurugenzi
hana mamlaka kupeleka kesi za
makosa hayo Mahakamani moja kwa moja isipokuwa mpaka
DPP atoe kibali chake, tena kwa
maandishi.
Kifungu cha 57 (1) & (2)
Kinamfunga mikono
mkurugenzi wa PCCB kutopeleka mafisadi papa
mahakamani moja kwa moja,
na ndicho anacholalamika
Dk.Hosea.
Hebu angalia sheria hii ilivyo ya
kibabaishaji. Katika kifungu cha 16 (3) adhabu yake ni kati ya
Tshs 1,000,000/- na 3,000,000/-
au kifungo jela kati ya miaka 3
hadi 5 AU vyote.
My take:-
*Dk. HOSEA yuko sahihi kuhusu kufungwa kwake mikono
kisheria.
* Sheria za adhabu kwa upande
wa faini haziangalii mpokea
rushwa amepiga bingo la kiasi
gani hata kama ni trilioni kadhaa, hakimu au jaji
atamtoza adhabu ya faini
isozidi Mill. 3
* Wanaotunga sheria ipo haja
kuifanyia marekebisho
*@ breki sina, Tusifanye ushabiki wa siasa ktk masuala
muhimu kama haya