Waziri Mkuu Majaliwa aahidi kuwasomesha Watoto wa Abdulaziz Ahmeid, Mwandishi wa Habari wa Channel Ten aliyefariki

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
299678273_5669386473124166_3234961862142838190_n.jpg
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameahidi kuendelea kuwasomesha Watoto wa aliyekuwa mwandishi wa Habari wa Channel Ten, Abdul -Aziz Ahmed ambaye amefariki Dunia Machi 13, 2023 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Majaliwa ametoa ahadi hiyo wakati wa ibada ya kumuaga marehemu Aziz ambapo amesema alikuwa ni moja kati ya waandishi waliokuwa wakiutangaza mkoa huo vizuri. Aziz amepumzishwa katika makaburi ya Mitandi Manispaa ya Lindi.

Aidha, kauli ya Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Lindi, Fatuma Maumba akimzungumzia msibani hapo amesema Abdulaziz Ahmed hakuwa mtu wa kuficha mambo, alikuwa mpambanaji na alifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Wadau wengi.

Hizo ahadi zinazotokana na hisia na simanzi wakati wa mazishi huwa ni utapeli mtupu. Hapo mfuate mwezi baada ya hizo hisia za msiba kuisha, utaona hata kama atakuwa anapokea simu.
 
Back
Top Bottom