Waziri, Mh. Membe anioneaye aibu hapa duniani name………

Kibunago

JF-Expert Member
Jan 11, 2008
300
122
Leo nimeshangaa sana Waziri Mh. Membe kusema kuwa kwa kuwa Egypt imesaidia Tanzania, sisi hatupaswi kusema chochote juu ya utawala usiokubalika kidikteta ulioondolewa na wananchi wa Misri.

Mh. napenda kukujulisha kuwa usichanganye msaada unaotolewa na nchi ukadhani kuwa ni wa Rais aliyeko madarakani, ni wa wananchi wenye nchi!!

Nchi kama USA na wengineo walipotamka dhidi ya Rais wa Misri na leo Libya haina maana kuwa walikuwa hawazipendi nchi hizo wala Wananchi wa nchi hizo bali yule Rais mhusika aliyepo ambaye hakubaliki.

Ulielewe hili sasa hivi ndg yangu vinginevyo unamiss point ya nguvu sana. Elewa kukaka kimya pia kuna maana kuwa uongozi ujao huko kwenye mabadiliko kwa njia ya demokrasia na wananchi wake pia watakaa kimya juu ya uongozi wako as you try to sit on the fence! Si lazima utoe kauli chafu au kutukana lakini ni vyema uonyeshe msimamo kwa kushauri.

Kumbuka, kauli, "Anioneaye aibu hapa duniani nami nitamuonea huko mbinguni kwa Baba!"


Nimekusifu kwa jinsi unavyojua hisroria ya nchi mbalimbali lakini narudia tena kuna point unaimiss sana juu ya ni nani mwenye nchi na anayetoa misaada na kusomesha watu wetu huko nje kati ya Marais walioko madarakani na wananchi wa nchi hizo!
 
Kumradhi, maana nilisahahu kueleza kuwa Mh. Waziri alionyesha msimamo huo wakati wa mahojiano kupitia ITV.
 
nilimsikiliza! nikaacha kuendelea kusiliza baada ya kugundua anajenga saikolojia ya watu kutokuunga mkono mapindizi ya maandamano. si unajua tena tanzania ishaingia matatani kuna dalili kikwete asimalize miaka yake 5!
 
huyo hajui anachokiongea,yaani mtu hata kama amekusaidi hutakiwi ku-question??
Ndio maana tuna ona mikataba hovyo hovyo kila siku,
Ndio maana wanajinyenyekeza kwa wahisani kila siku kutembea na bakuli kuomba misaada na kila wakiambiwa wanasema YES SIR kumbe huwa wanogopa sababu wanasaidiwa??
Ukitegemea sana misaada unakuwa MTUMWA,kweli nchi yetu na viongozi wameshakuwa watumwa kabisa.
Mpaka najisikia vibaya sana kuwa mmoja wa hiyo nchi.
 
nilimsikiliza! nikaacha kuendelea kusiliza baada ya kugundua anajenga saikolojia ya watu kutokuunga mkono mapindizi ya maandamano. si unajua tena tanzania ishaingia matatani kuna dalili kikwete asimalize miaka yake 5!

Dalili hizo ni zipi mkuu,hebu tudodofyee kidogo
 
Ni yaleyale ya Rostam kumsaidia JK kifedha kuingia ikulu 2000 mpaka leo hata akiua mtu hakuna wa kumgusa wala kumsema.
 
Mara kwa mara huwa napata shida kuamini kuwa Tanzania yangu niipendayo kwa moyo na akili zangu zote, na ambayo ina hazina kubwa ya wasomi na wataalamu wa fani mbali mbali, waliobobea na kukubuhu; imefikia mahali ikawa na mtu mwenye hoja nyepesi, kama mwakilishi wake, katika medani za kimataifa!
 
Back
Top Bottom