Waziri Membe ashiriki msiba wa mama mzazi wa Dk. Hoseah

alteza

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
209
53
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh.Bernard Kamillius Membe ameshiriki kikamilifu katika kuomboleza msiba wa mama mzazi wa Dk.Hoseah ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru.

Ni kawaida yake Waziri Membe kushiriki kikamilifu katika matukio ya kijamii.

Amekuwa akipongezwa kwa moyo wake wa kusaidia jamii bila kujali cheo,umri,kabila,rangi au hali.

Amenukuliwa mmoja wa waombolezaji akisema kuwa hii ni mara yake ya 29 anakutana katika matukio tofauti ya kijamii na Mh.Membe na amekuwa kivutio cha watu kila aonekanapo mbele ya macho ya jamii.

Waziri Membe baada ya kufika msibani alisaini kitabu cha waombolezaji na kisha kwenda kutoa rambirambi na salamu za pole kwa waliokuwa msibani.Hivi ndivyo jamii ipendavyo.

Inapenda kiongozi anayejishusha kwa wananchi na jamii yote kwa kushiriki masuala yao iwe katika shida au raha.
 
mmmm!!!! kwenda msibani si kwamba wewe unawajali watu! na wala sio upendo!! umakengeza ndo unawaponza!!!
 
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh.Bernard Kamillius Membe ameshiriki kikamilifu katika kuomboleza msiba wa mama mzazi wa Dk.Hoseah ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru.
So what?? Inatuhusu nini sisi?
Ni kawaida yake Waziri Membe kushiriki kikamilifu katika matukio ya kijamii.Amekuwa akipongezwa kwa moyo wake wa kusaidia jamii bila kujali cheo,umri,kabila,rangi au hali.
Juzi kulikua na msiba wa muuza bagia hapa jirani kwangu mbona sikumwona? Hao anaowajali ni akina nanj?
Amenukuliwa mmoja wa waombolezaji akisema kuwa hii ni mara yake ya 29 anakutana katika matukio tofauti ya kijamii na Mh.Membe na amekuwa kivutio cha watu kila aonekanapo mbele ya macho ya jamii.
Kwahiyo kivutio kwa huyo mama au?
Waziri Membe baada ya kufika msibani alisaini kitabu cha waombolezaji na kisha kwenda kutoa rambirambi na salamu za pole kwa waliokuwa msibani.
Katika waombolezaji wewe ulivutiwa na Membe tu au umetumwa??
Hivi ndivyo jamii ipendavyo.
kwahiyo jamii yenu inapenda sana misiba na pole za misiba?? Well nilifikiri jamii yako inapenda viongozi wenye ustadi ktk kuleta maendeleo na si kutafuta umaarufu kunuka wa misibani
Inapenda kiongozi anayejishusha kwa wananchi na jamii yote kwa kushiriki masuala yao iwe katika shida au raha.

Jamii haijali habari za wafu wala hakuna tija yoyote ktk kujali wafu wakati kuna walio hai wengi tu wanaohitaji msaada huyo unaesema anajali hatumuoni...
 
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh.Bernard Kamillius Membe ameshiriki kikamilifu katika kuomboleza msiba wa mama mzazi wa Dk.Hoseah ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru.

Ni kawaida yake Waziri Membe kushiriki kikamilifu katika matukio ya kijamii.Amekuwa akipongezwa kwa moyo wake wa kusaidia jamii bila kujali cheo,umri,kabila,rangi au hali.Amenukuliwa mmoja wa waombolezaji akisema kuwa hii ni mara yake ya 29 anakutana katika matukio tofauti ya kijamii na Mh.Membe na amekuwa kivutio cha watu kila aonekanapo mbele ya macho ya jamii.

Waziri Membe baada ya kufika msibani alisaini kitabu cha waombolezaji na kisha kwenda kutoa rambirambi na salamu za pole kwa waliokuwa msibani.Hivi ndivyo jamii ipendavyo.Inapenda kiongozi anayejishusha kwa wananchi na jamii yote kwa kushiriki masuala yao iwe katika shida au raha.

Membe misiba ya kule Uswahilini mbona huwa Haonekani? Kafa baba dull kafa mchezaji wa simba wa zamani na mezi B mbona hajafika huko? Hii promo unayompa Membe kamwe haitasaidia popote kwa hata WAMA sasa nao hawamtaki awe Rais walishamshitukia kitambo wakajua wakimweka tu lazima Chadema wataichukua Nchi kiulaini tu,
 
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh.Bernard Kamillius Membe ameshiriki kikamilifu katika kuomboleza msiba wa mama mzazi wa Dk.Hoseah ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru.

Ni kawaida yake Waziri Membe kushiriki kikamilifu katika matukio ya kijamii.

Amekuwa akipongezwa kwa moyo wake wa kusaidia jamii bila kujali cheo,umri,kabila,rangi au hali.

Amenukuliwa mmoja wa waombolezaji akisema kuwa hii ni mara yake ya 29 anakutana katika matukio tofauti ya kijamii na Mh.Membe na amekuwa kivutio cha watu kila aonekanapo mbele ya macho ya jamii.

Waziri Membe baada ya kufika msibani alisaini kitabu cha waombolezaji na kisha kwenda kutoa rambirambi na salamu za pole kwa waliokuwa msibani.Hivi ndivyo jamii ipendavyo.

Inapenda kiongozi anayejishusha kwa wananchi na jamii yote kwa kushiriki masuala yao iwe katika shida au raha.

Acha kujipendekeza mbona kwenye msiba wa mjomba wako hakuja? Dr Hosea ni Public figure wamekwenda wakubwa wengi ambao hujataka kuwaandika hapa na siyo huyo mtu wako pekee unayemnadi
 
Uwezo mdogo wa kufikiri pamoja na kushindwa kutumia akili katika kupembua mambo. Tanzania aihitaji kiongozi wa kwenda misibani. Zama hizo zimepita na mstokeo ya viongozi wenye upeo finyu ni kutopiga hatua kwenda mbele
 
Hii sio habari kabisa

Hata Jakaya, mzee wa kukaa kimya kwenye vifo vya albino na kupiga jaramba kwa Ray C alikuwepo
 
Mwaka wa uchaguzi tutasikia na kuona mengi sana.

vitu vya ajabu kabisa hivi... hakuna sera, mipango, mikakati, majumuisho ya michango kwa maendeleo ya taifa, imebaki misiba, ngoma, majungu, chuki na mapichapicha kwenye magazeti
 
Ovyooooooo!!! Tunataka Kiongozi mwenye mikakati ya kuzifanya hospitali zetu kuwa za kisasa, kama ile ya upasuaji wa tezi dume, aliyoifuata JK huko Marekani, ili kuongeza umri wa kuishi kwa raia, siyo Viongozi "wanaoshabikia misiba" kama JK, ambaye katika awamu yake, Kiongozi wa Madaktari wa Muhimbili alipodai maboresho ya Hospitali, ali-Ulimbokwa!!!!
 
Aaaaah membe kitu gani bana....bora ungesema presidaa tungekuelewa maana yeye hata misiba ya wasanii wenzie anashiriki....
 
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh.Bernard Kamillius Membe ameshiriki kikamilifu katika kuomboleza msiba wa mama mzazi wa Dk.Hoseah ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru.

Ni kawaida yake Waziri Membe kushiriki kikamilifu katika matukio ya kijamii.

Amekuwa akipongezwa kwa moyo wake wa kusaidia jamii bila kujali cheo,umri,kabila,rangi au hali.

Amenukuliwa mmoja wa waombolezaji akisema kuwa hii ni mara yake ya 29 anakutana katika matukio tofauti ya kijamii na Mh.Membe na amekuwa kivutio cha watu kila aonekanapo mbele ya macho ya jamii.

Waziri Membe baada ya kufika msibani alisaini kitabu cha waombolezaji na kisha kwenda kutoa rambirambi na salamu za pole kwa waliokuwa msibani.Hivi ndivyo jamii ipendavyo.

Inapenda kiongozi anayejishusha kwa wananchi na jamii yote kwa kushiriki masuala yao iwe katika shida au raha.

Kwa hiyo unasemaje. Tumpe kura ya uraisi? Jamani wanajf wengine vituko tupu. Mtu kuhudhuria kwenye msiba ni kawaida na haiitaji uadilifu au kutafsiriwa kwa namna yeyote ile. Ni wajibu wako na wengine kuhudhuria kwenye msiba kwani ndiyo maisha na sii sifa.
 
Back
Top Bottom