Jabali la Siasa
JF-Expert Member
- Jul 10, 2020
- 2,583
- 2,215
Kwa haraka moja kwa moja kwenye hoja,
Kasi ya Waziri wa TAMISEMI Mhe Mohammed Omary Mchengerwa inaleta matumaini mapya kwa Watanzania hasa wanyonge na walalahoi huko vijijini.
Kwasasa Tanzania inahitaji Viongozi aina ya huyu kijana ambaye ni jasiri na shupavu asiyependa sifa,kujisifia Wala kumwonea mtu, mkweli na mnyenyekevu kwa watu wote.
Mchengerwa anafanya maamuzi kama kiongozi bila kujali nini kitatokea nani atachukia au huyu nae ni mteule wa Rais ila tu kulinda Tanzania,Watanzania na rasilimali zao.
Tanzania tumekuwa na Viongozi wengi wasiopenda lawama wala kulaumiwa wenye kupenda kusifiwa na kufurahiwa na kila mtu hata kama ni mkosaji.
Tanzania ya leo inahitaji vijana jeuri na shupavu aina ya Waziri Mohammed Mchengerwa(MOM)
Kwamsiofahamu hii kampuni ya Nyanza Road Works Limited ni mfupa uliowashinda mawaziri wengi kwani inakazi sizizoisha karibu katika kila kona ila ilikuwa nani amfunge paka Kengele?
Kazi inaendelea Vizuri, Mchengerwa chapa Kazi Taifa linakufuatilia kwa ukaribu sana ongeza gia twende mbele.
===