Waziri Lukuvi atekeleza agizo la Rais Magufuli, aikabidhi Halmashauri ya Kigamboni ekari 715 za ardhi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
85,868
145,934
Waziri wa ardhi mh Lukuvi leo ametekeleza agizo la Rais Magufuli kwa kuikabidhi halmashauri ya Kigamboni ekari 715 zilizokuwa za Quality group iliyozimiliki kupitia International Village ltd.

Rais Magufuli alitoa siku 7 kwa Waziri Lukuvi awe ameikabidhi ardhi hiyo kwa halmashauri ya Kigamboni wakati anafungua ofisi za wilaya hiyo.

Wananchi msio na viwanja vya kujenga nyumba bila kujali itikadi zenu mnakaribishwa sana wilayani Kigamboni.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama

cc: Yericko Nyerere

====

Dar es Salaam. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Tanzania, William Lukuvi amekabidhi ekari 715 za ardhi kwa manispaa ya Kigamboni kama alivyoagizwa na Rais John Magufuli wiki iliyopita.

Februari 11, 2020 wakati akizindua ofisi za mkurugenzi na mkuu wa wilaya ya Kigamboni pamoja na hospitali ya wilaya hiyo, Rais Magufuli alimwagiza Lukuvi kuhamisha umiliki wa ekari hizo kutoka katika wizara yake kwenda kwa manispaa hiyo.

Leo Jumatatu Februari 17, 2020 , Lukuvi akiambatana na katibu mkuu wa wizara hiyo, Mary Makondo walikabidhi ekari hizo kwa viongozi wa wilaya na manispaa ya Kigamboni akiwamo mkuu wa wilaya hiyo, Sarah Msafiri.

"Leo nimetimiza maagizo ya Rais Magufuli ya kukabidhi ekari 715 mbele ya uongozi wa manispaa na wilaya ya Kigamboni. Natarajia kuona maeneo haya yanakuwa ya umma na sio kiwanja au makazi ya mtu mmoja moja," amesema Lukuvi.

Sarah amemshukuru Lukuvi kwa kutimiza ahadi hiyo na kuahidi kushirikiana na wizara hiyo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali katika ekari hizo walizokabidhiwa leo.
 
Hiyo Taarifa Sijaelewa hizo ekari 715 zilikua zinamilikiwa na Quality Group kupitia international Village Ltd

Zimefikaje mikononi Mikononi mwa Halmshauri kupitia Wizara ya Ardhi ??
Quality Group Wamepokonywa ?? Wameuzia Serikali ??
Ufafanuzi Tafadhali
 
Nikiona Mbaazi tu nakumbuka MBAAAAZI

Jiwe ni Joka Lenye Sumu, Koboko

= Kahawa, Korosho, Pamba, Chai, Mkonge, Mbaazi =
 
Hiyo Taarifa Sijaelewa hizo ekari 715 zilikua zinamilikiwa na Quality Group kupitia international Village Ltd

Zimefikaje mikononi Mikononi mwa Halmshauri kupitia Wizara ya Ardhi ??
Quality Group Wamepokonywa ?? Wameuzia Serikali ??
Ufafanuzi Tafadhali
... Rais wa JMTZ anayo mamlaka ya ku-revoke umiliki wa ardhi yoyote kutoka kwa yeyote kwa matumizi yoyote yatakayompendeza yeye bila kuhojiwa na yeyote popote wakati wowote ndani ya mipaka ya nchi. Hata kipande cha ardhi unachomiliki wewe (kama unacho) umekasimiwa tu umiliki wake kwa niaba ya Rais na ikimpendeza atakitwaa muda wowote without prior notice.

In short, Rais ndiye custodian wa ardhi yote ya Tanzania. Yaani linapokuja suala la umiliki wa ardhi yeye ndiye ALFA na OMEGA.
 
Back
Top Bottom