Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 9,485
- 14,353
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga juzi alilazimika kutumia salamu za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili kuwashawishi wanafunzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya (MIST) waweze kumsikiliza.
Kitwanga alilazimika kukikubali japo kwa muda Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kutokana na hatua ya wanafunzi wa chuo hicho kuguna kila alipoitaja ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi wakati akizungumza nao kuhusu inavyotekeleza sera ya elimu.
Waziri huyo alilazimika kuwasalimia wanafunzi hao akisema "CHADEMA hoyee!!, na ukumbi mzima ulizizima kwa mayowe na vifijo vya wanafunzi waliopaza sauti zao wakimjibu "Oyeeee" huku kila mmoja akimpungia alama ya vema kwa kuonyesha vidole viwili. Kitendo cha Waziri Kitwanga kutumia jina la CHADEMA katika kibwagizo hicho kilitokana na hatua ya wanafunzi hao kuguna pale alipoanza kujibu maswali yao kwa kusema "katika Ilani ya ya CCM….." bila kumalizia kusema alishtushwa na miguno
source: Tanzania Daima