Waziri Kigwangalla: Walishindwa kuniua wakati ule! Naingia vitani kwa silaha zote na vita ni asili yangu

Huyo dada ni mjasiriamali mkubwa sana mjini. Anauza uchumi wake aliompa Muumbaji. Malaya yani, na hapo ndio Boss kafika

Marekebisho sio mjasiriamali bali ni MJASIRIAMWILI

Hawa ndio utawasikia vingereza vingi sana mara wanajiita beauty with brains mara wanajiita hardworking. Mara wajifanye motivation speakers yaani wanawaathiri sana watoto wa kike.
 
Vilaza kama hawa wanependwa sana Tanzania, not surprised maana majority of the people ni vilaza pia. Anachoongea hatuhitaji hata kukijua ni plain stupid.
 
Aliesema au kuandika haya ni Waziri wetu kweli mwenye shahada lukuki?
Napenda kujua zaidi

Au ndio sawa na Mo alipoghafilika simba kufungwa mara tukajua kumbe kuna 4billions ni mishahara na marupurupu wachezaji walipata.

By the way; kama kweli ameandika Waziri; mbona JPM alipewa sumu ila ndo tumejua siku Rais Mstaafu Mkapa anazindua kitabu?
Dr. Mwakyembe nae yalimkuta mabaya mpaka akapelekwa nje ya nchi; hatukuona kurasa za maandishi ukutani akiwa na hisia kali namna hii.

Mhe. kama ni yeye akumbuke aligombea Urais; sasa siku akikalia kile kiti mbona wale wote hata kama wamesingiziwa hasira yako mjukuu wa Mtemi itawamaliza?!

Mlio karibu na Waziri; mjuzeni atulie. Ni vema akawa mtulivu aka-focus kwenye kushinda war at expense of loosing battle.

Taifa linatambua mchango wako hata bila kujitetea. Na siasa hata ukifanya mema 99% moja ukachemka maana huo ni ubinadamu; rivals wako kisiasa watatumia 1% na kui-amplify as if umechemka 100%.

Sijui mtume anatuasa nini kwenye Koran; ila Yesu akijua wamesingizia alisema wasamehe maana hawajui walitendalo. Wanadamu ukijua hata Yesu walimfanyia fitna na majungu; bila shaka kwenye siasa mambo hayo ni sehemu ya vibuti.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaandika Waziri wa Maliasili na Utalii kupitia ukurasa wake wa Instagram;

"Kuna limit kwenye uvumilivu. Uvumilivu ni hekima. Uvumilivu unakuandaa kuwa mtu mwema na bora zaidi mbeleni. Uvumilivu wako usionekane kuwa ni ugoigoi ama upuuzi.

Kuna watu wamenijaribu kwa muda mrefu sana. Kwa kweli sasa wamefanikiwa kunifikisha ukomo wa uvumilivu wangu, naogopa uongo usijegeuka ukweli. Nafahamu watu wema, wachapakazi, watenda haki, wana mageuzi wamewahi kuumizwa kwa sababu ya uvumilivu wao.

Kuna wakati nilikata tamaa nikataka kujiuzuru uongozi wa Umma lakini nikaja kufikiri upya, hivi ni nani atafanya kazi hizi? Kama watu wema wanaopigwa fitna na majungu wakisusa na kuacha kazi za Umma za kujenga nchi? Ni nani atakayefanya? Siyo itakuwa ni kukubali uongo ushinde ukweli?

Ukiwa Waziri wa Maliasili na Utalii ukakuza idadi ya Watalii kwa kasi, ukaongeza mchango wa sekta yako kwenye pato la Taifa, ukadhibiti ujangili, ukaufanya utalii ikawa kitu ‘fashionable’, ukazuia ubadhirifu/rushwa/matumizi mabaya ya ofisi/uzembe, badala ya kupendwa na kuungwa mkono watu wanakushambulia.

Ukijiuzuru unakuwa umewapa raha na ruhusa ya kuendelea na mambo yao. Kuna watu mfano wananiandika kila siku kwenye gazeti lao, najua wanatumwa kwa kulipwa, wanaandika vitu vya kipuuzi visivyo na ushahidi wala substance, lengo ni kuchafua tu. Na hii ni dalili kwamba hawana cha maana cha kutumia kunichafua ili malengo yao yatimie, wangekuwa nacho ningeomba dunia isimame nishuke!

Kwa kuwa wao na washirika wao wamenifikisha ukomo wa uvumilivu wangu, nimewapeleka Mahakamani, Mahakama itaamua. Washirika wao wamewadanganya kwa rushwa, sasa wakawape ushahidi huko Mahakamani, nitawafilisi kuanzia Kampuni hadi wao binafsi.

Anayewapa taarifa za uongo naye tumemjua. Aliwahi kusema nilipopata ajali kuwa ‘bora ningekufa’ tu. Nilimjua na kumsamehe. Amejiunga wengine wawili, wananishughulikia. Hawa nitawashughulikia kwa namna yangu.

Waliwahi kupanga mbinu za kunidhuru, pengine kuniua. Mungu akanisalimisha. Walishindwa kuniua wakati ule, hawatoweza kuniangusha leo. Naingia vitani kwa silaha zote.

Usiombe kunifikisha hapa. I am the worst enemy you can shop around! Twende kazi sasa.

Kiasili, mimi ni mtoto wa kwanza wa mtoto wa kwanza wa babu yangu, ambaye alikuwa Mtemi/Chifu. Kwa mila zetu, mimi ni Mtemi/Chifu. Mababu zangu hawakupewa utemi, walichukua kwa kupigania. Hivyo, vita ni asili yangu. Kushinda ni asili yangu.

Mimi hupigana vita bila kujali nani atadhurika, iwe mimi ama adui ama collateral yeyote yule, sawa tu. Huwa sijali matokeo ya vita. Aliyenitia kidole jichoni sasa akae sawa. Naanza kujibu mashambulizi.

Aliyetaka vita sasa ameipata! Sijawahi kuwa dhaifu wala mnyonge. Sijawahi kukubali kuonewa, kukandamizwa wala kunyanyaswa maishani mwangu. Huwa napigania haki na heshima yangu. Huyu ndiye mimi.

Hizi nyingine ni tabia tu nilifundishwa na walimwengu na ulimwengu. Asonijua basi afuatilie historia yangu. Twende kazi!"
Toto la kinyamwezi laja juu! Sawa sawa kawatule mwanayoshi..
 
Nadhani ungetueleza ukweli wa zile tuhuma tungekuelewa lakini hapa unaonekana unatuomba tukuonee huruma na mwisho tukuogoe.
Upo ktk utumishi wa umma tueleze kwa jinsi gani zile tuhuma sio kweli. Tuna haki ya kujua ukweli na sio huruma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa Kuna vita Kaka Mkubwa au upuuzi? km unafahamu ukweli kiongozi unaleta mambo taarabu kikubwa mkumbushe khs Karma ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga hayo ndio majibu ya dhuruma alizowafanyia wenzie...
Huyu Dr. Kigwa, namfahamu kweli ni mpambanaji
Maadam vita imetangazwa, tusubirie mpambano.
P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ha ha ha ndio maana watu wenye vihela wakianzaga kuwa mezesha ujinga watu kwamba wamefanikiwa kwa vibiashara kama kuuza kashata nk huwa nawaangalia naishia kuwaonea huruma wasikilizaji wake sasa MTU kama kama huyo anaweza kuwa na kiduka cha kuuza kope za bandia lkn anamiliki VOGUE na mighorofa wajinga wanadhani nikile kiduka kumbe anauza Nyapu
Marekebisho sio mjasiriamali bali ni MJASIRIAMWILI

Hawa ndio utawasikia vingereza vingi sana mara wanajiita beauty with brains mara wanajiita hardworking. Mara wajifanye motivation speakers yaani wanawaathiri sana watoto wa kike.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Adolf Hitler aliwahi kusema" ni rahisi kupambana na jeshi hata liwe kubwa kiasi gani lakini si rahisi kupambana na mwandishi wa habari mwenye nia ya uchochezi"

Hapa Hitler alikuwa anazungumzia nguvu waliyonayo waandishi wa habari na media kwa ujumla, hakuna aliyewahi kushindana na media na akashinda.
Makonda Alishinda. Makonda JEMBE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom