Umaskini wa asili ni rahisi kuuondoa kuliko umaskini bandia (umaskini wa kutengenezwa na watawala)

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Anaandika, Robert Heriel,
Mtibeli.

Hakuna kazi rahisi kama kuuondoa Umaskini. Rahisi Sana. Ukisikia mtu anakuambia kupambana na umaskini na ikazidi ngumu basi jua huyo ni muongo au anazungumzia, Siasa.

Matatizo ya asili yanakabiliwa kwa urahisi na kanuni rahisi kuliko matatizo ya kutengenezwa.
Ujinga wa asili ni rahisi kuundoa kwenye jamii kuliko ujinga wa uliotengenezwa.

Taikon katika chunguzi zangu nikabaini ya kuwa matatizo mengi ya ulimwengu huu sio ya asili bali ni matatizo ya bandia ambayo yamebuniwa kwa Faida Fulani ya Watu fulani, na yale matatizo ya asili hakuna ugumu wa kuyaondoa.

Vijana lazima muelewe kuwa ni rahisi sana kupambana na umaskini ulioukuta hapo nyumbani kwenu, lakini ni ngumu sana kukabiliana na Umaskini wa kusababishwa na mtu au Watu wengine, na hapa nazungumzia wale walioitwa au wanaojiita watawala iwe kisheria au kwa namna yoyote ile.

Kanuni ya kupambana na Umaskini wa asili ni mbili tuu.
1. Kufanya kazi kwa juhudi, bidii akili na maarifa.
2. Kutumia rasilimali kwa usahihi bila kuathiri mazingira.

Rasilimali hizo ni muda, Watu, na Mali na maliasili. Kwenye muda kuna wakati uliopita(tumia Data Sahihi zilizopita) wakati uliopo ambao upo, na wakati ujao. Rasilimali Watu. Hapa utapata nguvu kazi na mawazo(akili) za Watu wengine ambazo wewe isingewezekana kuwa nazo. Ardhi, maji, misitu, wanyama ni sehemu ya maliasili.

Yaani kwenu kama ni maskini kwa asili. Basi ukitaka utoboe ni kanuni mbili hizo.

Wakati unahangaika kupambana na Umaskini wa asili unakuja kugundua kuwa kumbe kuna umaskini mwingine wa kutengeneza. Umaskini Bandia. Hapo ndio unashangaa Watu wanapambana lakini hatoboi.

Ni uongo kusema Kufanikiwa (kuushinda Umaskini) ni majaliwa ya Mungu. Mtu yeyote anayeweza hivyo jua tayari keshatengenezwa kifikra na walewale wasiotaka ajue ukweli.

Kufanikiwa (kuushinda Umaskini wa Asili) sio majaliwa kutoka kwa mwenyezi Mungu bali ni uamuzi wa mtu au jamii yenyewe. Mziki upo kwenye Umaskini Bandia.

Umaskini Bandia unaletwa kwa mwavuli wa kuuondoa Umaskini wa asili.

Mataifa makubwa hutengeneza mazingira ya kuufuta Umaskini wa asili ili kupumbaza Watu lakini nyuma yake kwa jicho jingine wanakuletea umaskini Bandia ambao ni mgumu sana kuuondoa

Serikali batili au zenye dhulma huzuga kwa kuonyesha zinahangaika kupambana na umaskini wa asili wa wananchi lakini ukiangalia kwa jicho jingine mambo huwa tofauti kabisa.

Umaskini Bandia sifa yake kuu ni ile dhana ya watawala kukuambia bila wao nchi haiwezi kuendelea. Au ile dhana ya kusema wataleta barabara au maendeleo. Hao ndio wanaotengeneza umaskini Bandia hata kama watajenga vitu wasemavyo lakini utastaajabu bado jamii ipo kwenye lindi la umaskini mkubwa.

Umaskini Bandia upo hata kwenye Dini. Ile kusema bila kwenda kwenye nyumba za ibada kuombewa hutofanikiwa(hutoushinda umaskini) ndio umaskini wenyewe huo.

Huna haja ya kumuomba Mungu ili uondokane na Umaskini wa asili kwa sababu naturally kila kiumbe kimezaliwa na uwezo wa kuuondoa Umaskini wake na jamii yake pasipo msaada kutoka nje, lakini Umaskini bandia yaani wakutengenezewa huo unahitaji nguvu ya ziada kukabiliana nao.

Je, mpaka sasa huo unapambana nao ni umaskini wa asili au Bandia(wakubambikiwa)?

Taikon acha nipumzike sasa.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
Kweli wewe no taikon wa Fasihi. Bandiko limegusa mshono, ni bora umasikini wa bandia wanaopandikiza kimataifa kuliko umasikini bandia unaowekwa na watawala wetu ili wao waendelee kuneemeka. Reformationskubwa inahitajika lakini walio wengi ni wale either wamekata tamaa kwa yanayoendelea au ni wale wasiokuwa na uwelewa/maarifa ya jinsi gani ya kupambana na kuwang'oa hawa wanaosababisha umasikini bandia.
 
Ukweli mchungu huu,kwa watawala wa bara la kiza,kwao kuwafanya wananchi kuwa masikini ni turufu muhimu kwenye siasa zao za maji taka.
 
Ccm imetengeneza umasikini kwa kutumia mfumo WA Kodi.
Kodi ni tool ya kuwafanya wengi wawe masikini.
Wanatoza Kodi kubwa wanakusanya kidogo.
Kodi kubwa ili wengi washindwe kulipa wawe masikini.
Mfano Kodi za magari.
Gari ni chombo Cha kukuza uchumi Kodi ya nini likiingia.Si itajilipa yenyewe kwenye mzunguko?
 
Ukiwa maskini wa category ya umaskini wa kutengenezwa,unakuwa na njaa kupitiliza na tamaa ,na hata akili inakuwa sio timamu kabisa ,ndo maana mambo mengine ukiyaona mtu yanakuwa ya kustajaabisha kabisa,mfano mama anampigaje mtoto wake mpaka kupelekea kifo eti kisa elfu moja,hakika yote Kwa sababu ya umaskini ambao huleta njaa ambayo humfanya mtu asiwe na akili timamu

Vilevile hivi mtu anawezaje kuhatarisha maisha yake kwenda kuiba mfano kandambili msikitini na mwisho wa siku kukamatwa na kuuliwa na raia wenye hasira Kali
Yote Kwa yote yanatokea Kwa nini Kwa sababu ya umaskini ambapo husababisha mtu kuwa na tamaa na njaa iliyopitiliza ambayo humfanya kutokuwa na akili timamu

Ndo maana maskini wengi Wana:chuki,husuda,rohombaya,unafiki,hasira za ovyo ovyo yote Kwa sababu ya kutokuwa na akili timamu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom