Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 3,795
- 3,361
Hayo ndo majibu ya Naibu Waziri wa Kazi na Ajira kuhusu hatima ya kikokotoo kipya kwa wastaafu. Kuwa kafanya utafiti unaoonesha ni kikokotoo bora kuliko cha zamani. Hivyo, wastaafu wafanye utafiti ndo waulize wasilalamike tuu.
Mawaziri kama hawa hawatufai katika nchi inayotambua haki na maslahi kwa makundi maalumu kama wazee wastaafu.
Wastaafu wengi wameonesha kitoridhika na kikokotoo kipya cha mafao yao. Wanadai walipwe kwa kutumia mfumo wa kikokotoo cha zamani. Ni haki yao, na ingefaa kuweka hata option au kura ya maoni ukweli upatikane.
Serikali isishinikize jambo lisilo na afya kwa walengwa wa mifuko hiyo. Ni jambo la aibu kwa Waziri kumwambia mstaafu mwenye miaka 80 akafanye utafiti ili agundue ubora wa vikokotoo hivyo viwili.
Mama yetu, na Rais wetu wanaokuangusha siyo wengine ni hao wateule wako.