MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,643
- 33,433
Kwa niaba yangu binafsi na wana Bunju tunashukuru mno kwa kambi uliyoweka zaidi ya wiki kutatua migogoro ya ardhi na kubwa zaidi ni kubeba timu zima kuhakikisha wananchi wana rasimisha ardhi zao.
Huu ndio ubunifu tunaotamani viongozi wawe nao badala ya kushinda ofisini. Umekuwa mnyenyekevu sana kusikiliza na kutatua changamoto instantly inapowezekana na pia timu yako uliyoambatana nayo imefanya kazi kubwa sana hadi muda wa ziada ili watu warasimishe ardhi zao.
Kupitia zoezi hili zuri nashauri ungeunda kamati makini kila wilaya ziweke kambi ya wiki moja kwa mfumo huu uliofanya Bunju. Matatizo mengi yatatatuliwa na pia wengi watapata hati zao kwa wakati na gharama nafuu.
Nashauri hilo zoezi kila wilaya liwe chini ya wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri na iitwe wiki ya ardhi. Muda utakuwa mdogo lakini matatizo mengi yatapunguzwa.
Mh. Waziri Silaa tunakushukuru sana kwa kazi hii ya mfano huku Bunju na umeacha alama muhimu sana kwetu, Leo ni jumapili lakini upo na wana Bunju kuhitimisha zoezi hili.
Asante sana