Waziri Dkt. Ndumbaro Akagua Eneo la Ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu Jijini Arusha

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro ametembelea na kukagua eneo la Olmoth ambalo litajengwa uwanja mpya wa mpira wa miguu wenye uwezo wa kuchukua watazamaji Elfu thelathini utakaotumika katika michuano ya AFCON 2027.​

Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekagua eneo hilo Desemba 15, 2023 Jijini Arusha sambamba na kupokea hati ya eneo hilo lenye ukubwa wa hekari 49 iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongella ambaye amebainisha kuwa hati ya sehemu ya eneo lililobaki itakabidhiwa kwa Wizara kabla ya mwezi Machi, 2024.

Akizungumza mara baada ya kupokea hati hiyo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameeleza kuwa Wizara inatarajia kumkabidhi mkandarasi eneo la mradi mwezi Januari, 2024 ili kazi ya ujenzi wa uwanja huo ianze.

GBo7NRnWkAAlIq0.jpg
GBo7OIeXAAAoqy6.jpg
GBo7PEJXsAEg-08.jpg
GBo7P1_WgAAj5u_.jpg
 
Back
Top Bottom