Waziri Dkt. Chana awatunuku vyeti wahitimu 106 Malya

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
810
513
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewatunuku vyeti wahitimu 106 wa Stashahada katika Chuo Cha Michezo Malya kilichopo wilayani Kwimba Mwanza leo Julai 15, 2023.

Mhe. Chana amewapongeza wahitimu hao ambapo amewataka kutumia elimu waliyoipata katika chuo hicho kuendeleza vipaji katika maeneo yao na shule wanazofundisha ili vijana wengi wa Kitanzania wapate fursa za ajira kupitia michezo.

"Wizara yangu, Elimu Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na Ofisi ya Rais-TAMISEMI tumejipanga kuondoa changamoto ya muundo wa Utumishi kwa wahitimu wa chuo hiki", amesema Mhe. Chana.

Ameongeza kuwa, Serikali katika mwaka ulioshia Juni 30, 2023 imeshatoa kiasi cha shilingi 1.699,156.17 kwa ajili ya maendeleo ya ujenzi wa Hosteli ya chuo hicho pamoja na shilingi 291,030,542.49 kwa ajili hatua za awali za ujenzi wa Akademia ya michezo ndani ya chuo hicho.

Wahitimu hao wamehitimu katika kozi ya Uongozi wa Michezo, Elimu ya ufundishaji michezo pamoja na elimu ya mazoezi ya viungo katika michezo.

IMG_20230715_205248_970.jpg
 
Back
Top Bottom