Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,903
- 945
MWAKIBETE CUP2023 HATUA YA NUSU FAINALI KATIKA JIMBO LA BUSOKELO
Mashindano ya Kombe la Mwakibete CUP 2023 hatimaye yamefikia hatua ya Nusu Fainali ambapo yanayotarajiwa kuendelea kutimua vumbi tarehe 19 Novemba, 2023 Uwanja wa Lwangwa.
Mashindano ya michezo ya Mwakibete CUP 2023 yameandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Busokelo, Mhe. Atupele Mwakibete kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali ya CCM ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuinua vipaji vya michezo kwa vijana
Aidha, Huu ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2020-2025 katika kuendeleza michezo kwani michezo ni ajira, michezo ni burudani na michezo ni afya na michezo ni sehemu ya kutuweka pamoja kwa Umoja
WATU WOTE MNAKARIBISHWA