Waziri Bashungwa: Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya vikosi vya jeshi

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
SERIKALI INAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA VIKOSI VYA JESHI: WAZIRI BASHUNGWA

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa (Mb) amesema Wizara inaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi na kuboresha miundombinu mbalimbali kwenye vikosi vya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ikiwemo ukarabati wa makambi na nyumba za makazi kwa maafisa na askari.

Bashungwa amesema hayo leo tarehe 12 Mei 2023 wakati akijibu swali la Mhe. Maryam Azan Mwimyi (Viti Maalum) aliyetaka kujua Je, ni lini Serikali itajenga upya na kufanya ukarabati nyumba zilizo katika Makambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania?

Bashungwa amesema Ukarabati wa makambi ulianza kutekelezwa tangu mwaka 2020, na unafanyika kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha na vipaumbele.

Amesema awamu ya kwanza ya ukarabati inahusu nyumba zilizonunuliwa kimakundi nje ya makambi ya Jeshi, ikiwemo magorofa ya Mwenge, Keko, Nyumba za makazi za Masaki, Kitangili, Nyegezi, Nyamanoro, Tabora, Tanga, Shinyanga na Mtwara.

Aidha, Bashungwa amesema ukarabati huo wa awamu ya kwanza umeanza kutekelezwa katika magorofa ya Mwenge Dar es salaamna Tanga na inategemewa ifikapo Disemba 2023, ukarabati wa awamu hii utakuwa umekamilika.

Kadhalika, amesema ukarabati awamu ya pili utahusisha nyumba zilizopo makambini kwa kuzingatia kanda mbalimbali kwa kuanza na Kanda ya Mashariki, Zanzibar, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Kati, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kusini, Kanda ya Ziwa na kumalizia ukarabati Kanda ya Magharibi.
 
Back
Top Bottom