Akili Kichwani
JF-Expert Member
- Jan 7, 2010
- 1,508
- 216
imeandikwa na Hamis Shemdoe kutoka arusha
waziri wa afya na ustawi wa jamii mh. Dr Haji Mponda amesema serikali imesikitishwa sana na ushirikiano mdogo inaopata kutoka kwa wasadizi wa Mchungaji mstaafu wa KKKT Ambilikile Mwasapile anayetoa tiba ya magonjwa sugu huko Loliondo hasa katika kupata maelezo mbalimbali yanayotakiwa ili kukamilisha taratibu za kumsajili kama mganga wa tiba za jadi kwa mujibu wa sheria za nchi
waziri mponda aliyasema hayo muda mfupi baada ya katibu mkuu wa wizara yake Bi. Blandina Nyoni kumpa taarifa kwamba zoezi la kumsajili linakwama kutokanana wasaidizi wa babu kuonyesha ushirikiano mdogo ambapo wakati wote wamekuwa wakisema kuwa hawana muda wa kukusanya taarifa zake kwa vile wamebanwa na shughuli za kuandaa dawa na kuigawa kwa wagonjwa.
Mch. Mwasapile mwenyewe alipotafutwa kufafanua utata huo alisema kuwa yeye hawezi kusajiliwa kama mganga kwani hajui chochote katika masuala ya uganga na kwamaba anachofanya yeye sio uganga. aliongeza kuwa kama ni usajili, basi asajiliwe kama mhubiri wa injili aliye chini ya kanisa linalotambulika nchini yaani KKKT na siyo mganga kwani kazi zake ni za kichungaji na zimekwishabarikiwa na kanisa lake la KKKT ambalo limeishasajiliwa.
tangu kuibuka kwa tiba jiyo ya magonjwa sugu huko loliondo mkoani Arusha kaskazini mwa Tanzania, maelfu ya watu wamekuwa wakimiminika kutafuta tiba hiyo na kuilazimu serikali kuingilia kati kuboresha mazingira ya kutolea tiba na kuanza hatua mbalimbali za kumsajili
source: BBC Swahili - Mwanzo