Waziri Aweso na Wizara ya Maji wizi umekithiri

robinson crusoe

JF-Expert Member
Oct 22, 2020
740
1,214
Tutaendelea kusema hata kama hakuna hatua lakini wizara ya maji ni wezi na viongozi wa wizara ndo vinara wa wizi.
Waziri Aweso na katibu mkuu wake ni wezi wa pesa za wizara kwa kushirikiana na watendaji walioko ktk ofisi za mabonde. Kuna pesa nyingi zinapelekwa ktk ofisi za mabonde na kurudishwa wizarani na kugawana. Huu siyo mtindo mpya na siyo kwa wizara hii tu.

Wizi mkubwa kabisa uliopo sasa hivi ni pesa kwa ajili ya uhifadhi wa bonde la mto Rufiji baada ya mradi wa bwawa la Mwalimu Nyerere kuanza kujengwa. Kuna mabilioni ya shilingi hupelekwa makao makuu ya bonde mjini Iringa kwa kisingizio cha uhifadhi, lakini ukweli ni kwamba pesa hizo huchotwa kwa pamoja na kurudishwa kwa watendaji wa wizara, kuanzia wizarani hadi ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali.

Upo uthibitisho wa vitendo hivi kupitia akaunti ya bonde ambayo huzitoa pesa zote kila zinapoingia, jambo ambalo kiutendaji ni ishara ya ufisadi kwa sababu huwezi kufanya shughuli za uhifadhi wa bilioni 2 kwa muda wa wiki moja. Uhifadhi ni shughuli za kila siku kwa muda mrefu.

Katika shughuli hizi waziri na watendaji husingizia kuitumia jamii iliyoko ktk bonde la mto rufiji, lakini uhalisia wa mambo siyo hivyo. Wananchi hawa hawafaidiki na lolote linalohusu shughuli hizo na hata hawahusishwi kabisa.

Barua ifuatayo ni malalamiko yaliyotumwa kwa katibu mkuu wa wizara ya maji kueleza juu ya ufisadi unaofanyika, lakini hakuna jawabu lolote liliotolewa. Kwa ujumla wananchi hawa hawatajibiwa kwa sababu waiziri na Katibu mkuu wa wizara wanahusika na wizi wa pesa za wizara hii.
 
Attachments

  • Barua_Mwenge_2021.pdf
    112.2 KB · Views: 38
Hii wizara ni shule ya rushwa! Bahati mbaya sana makandarasi wanaopewa kazi ktk wizara hii pia wanafahamu kwamba ni sehemu ya kuiba pesa. Wapo wale mashuhuri sana wanajiita Don Consult, hawa ndo mabingwa wa wizi wa pesa za wizara. Hii ni kwa sababu ni bureau iliyoanzishwa na wafanyakazi ndani ya wizara yenyewe!
 
Mwaka ujao wa fedha tutaanza kutumia mfumo wa MUSE nadhani itadhibiti mambo haya.
 
Mwaka ujao wa fedha tutaanza kutumia mfumo wa MUSE nadhani itadhibiti mambo haya.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Alichoandika kwenye thrd nimekisikia miaka mingi sana enzi za akina Lowasa. Yaani wakati ule injinia wa maji wa mkoa anapelekewa pesa baadaye wizara inaomba kiasi fulani kirudishwe kwa watendaji wizarani. Isipofanyika unaweza kupokonywa ofisi.
Naangalia pesa ya kuhifadhi mazingira ya mto, kama unapeleka milioni hata 200 huwezi kuzimaliza kwa wiki moja hata mwezi mmoja maana hakuna malipo ya mshahara hapo. Ina maana Katibu mkuu na waiziri na wakurugenzi wanajiwekea kiasi cha kupiga kwa makusudi.
 
Mwaka ujao wa fedha mkuu wa kitengo atakaa na mtu wa resource wataandaa plan of action kwa mwaka mzima wa fedha na bajeti yao..so kazi isipofanyika na hela ikarudi hazina lazima uulizwe kwanini hujaitumia so ni mfumo mzuri hata ruwasa wameutimia na wamefanikiwa..kikubwa ofisi za mabonde zijipange TU isije kuwa mwaka wa kwanza wakakosea ikaleta changamoto.maana kwa mfumo huu ukikosea mpango kazi wako itakubidi usubiri miezi sita ndo upeleke madokezo tena

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kwenye hiyo barua kuna sehemu eti wameandika 'mama yetu, mheshimiwa sana,kipenzi cha wanyonge' yaaani shobo mpk kero..
 
Sema Waziri anasifika sana saivi
Sijui km watasikiliza
Kweli! Yaonekana waziri anapendwa kwa sifa zingine, siyo utendaji wake. Niliwahi kukaa bar moja nikipata kinywaji, Kama kawaida ya pombe, watu wa wizara walianza kuropoka juu ya tabia ya Aweso. Nasikia ni mpigaji ni hakuna. Kila anakokwenda ni kelele tu lakini mara nyingi huwa ameshiriki kupiga pesa. Nimeangalia pia video clip ya hapa JF iliyomuonesha Aweso akipiga kelele na mkandarasi. Mara moja alipotaja viongozi kuhusika na rushwa, waziri alipotezea na kuanza kuwa mpole. Nadhani alikumbuka kwamba ni muhusika.

Taarifa nilizowahi kupata ni kwamba Maafisa bonde wanaopelekwa kwenye miradi ni wale wanaorudisha pesa kwa waziri na katibu mkuu wake. Pale Morogoro kuna dada ilisemekana ni mlokole akaondolewa na kupelekwa bonge la msanii. Kumbe kulikuwa na mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi za bonde. Hakika pesa imepigwa! Baada ya mradi, msanii kaondolewa, nasikia yuko wizarani. Sasa hapo Iringa yaonekana ni sehemu mpya ya upigaji. Fuatilia uone afisa bonde ni nani na tabia yake.
 
Hapo Waziri kakosa la kusema!!!!
 
Mnataka asubiri kikokotoo?

Hata kama ingekuwa wewe
Kikubwa miradi inaenda

Makuhani wanakula hekaluni jmn ndivyo ilivyo
Ibada zinaendelea
 
Mnataka asubiri kikokotoo?

Hata kama ingekuwa wewe
Kikubwa miradi inaenda

Makuhani wanakula hekaluni jmn ndivyo ilivyo
Ibada zinaendelea
Boss umechanganyikiwa? Yaani waziri na katibu mkuu wake wapige pesa, halafu miradi iendelee?
 
Back
Top Bottom