Wazee wa Dar es Salaam ni akina nani?

Kila kukiwa na tatizo rais Jakaya Kikwete hukimbilia kwa wazee wa Dar es salaam. Je wazee wa Dar es salaam ndiyo wazee tu? Je hii si dharau kwa wazee wengine wa Tanzania? Je ni kwanini wazee wa Dar es salaam wanatumiwa kama dodoki wasitambue hili? Tatizo ni njaa, elimu au uroho? Heri angekuwa anakutana na wazee kujadili pesa yao ya ustaafu isivyokidhi mahitaji yao ingeingia akilini. Kwanini wazee wa Dar es salaam hawalioni hili kiasi cha kuonekana kama wasaliti, wachumia tumbo na vibaraka wanaotumiwa na watawala wa hovyo? Tusaidiene wanangu huenda wanaweza kutoka kwenye lindi la usingizi la kutumiwa kiholela.
 
pengine kwasababu anajua kuwa ndiyo wenye rangi ya kijani haswaa
 
Si Wazee wa Dar es salaam bali ni wazee wa ccm waliojichokea ambao hawawezi kumbanua mambo wakajua kipi ni mchele na pumba ni kipi ndo maana hata hotuba za jamaa huishia kuongea mbayuwayu kwa sababu anajua hakuna wa kumchalenji
 
jana niliwasikia bakwata nao wakiwaomba madaktari waache mgomo nikajiuliza kwanini Bakwata inajiiingiza ktk mchezo wa kuwapigania wanasiasa huku wakujua kigeugeu cha wanasiasa hawajifunza tu kwenye swala la kadhi?? badala ya kumwambia JK awaondoe wanasiasa wawili tu kati ya maelfu ya wanasiasa tusiowaitaji lakini as always Bakwata is there to defend incompetent politicians ni ajabu kuwa hivi Bakwata huwa hawakai wakajadili issue kabla ya kutoa tamko. bakwata inaweza kuwa inaongozwa kidikteta kuliko wengi tunavyofikiria.
 
Hao sio Wazee wa Dar bali ni Wazee Mafisadi wa CCM na wenye njaa. Hawana hata haya na aibu wameitwa na Mwenyekiti wao aliyehongwa Suti na Mwanamme, Hao wazee wa CCM wanaitwa kudangwa baada ya kupewa kahawa na kashata, nawahurumia kama wangekuwa baba zangu ningewatandika bakora ili wafunguke
 
mtindo wa rais kuongea na wazee wa dar aliuanzisha nyerere!hao wazee waendapo diamond hupewa chochote?
 
Je ni halali kwa mh. Rais wa nchi kila atakapo kuzungumza na taifa ama kutoa ufafanuzi wa jambo fulani kutumia wazee/makada wa ccm dar es salaam? Je huu uwakilishi ni sahihi kutumika ktk nchi yetu hii iliyodhamiria kufuata mfumo wa vyama vingi?
 
Haiwezekan kuwa na rais anaogopa wananchi tatizo la wa2 wengne anataka kuongea na wazee wa ccm akidai wazee wa mkoa flan kwel tutafika kwa namna hii?
 
TANGU ‘Enzi za Mwalimu’, kukiwa na jambo kubwa kitaifa, basi, Mwalimu aliliongea kupitia kwa “ Wazee Wa Dar Es Salaam”. Na mahali haswa wanapokutana ‘Wazee wa Jiji’ kumsikiliza ‘ Mkuu Wa Kaya’ ni pale Upanga kwenye Ukumbi wa Diamond.


Jambo hilo lililoasisiwa na Mwalimu sasa limekuwa ni utamaduni wa kisiasa. Mathalan, ni pale Upanga Diamond Jubilee ndipo Mwalimu alipotangaza vita dhidi ya Idi Amin kupitia Wazee Wa Dar Es Salaam . Nilipokuwa mtoto pale Ilala, nilitamani sana nikue nije kuwa mtu mzima, kisha niwe mmoja wa ‘ Wazee wa Dar Es Salaam’ ! Ndoto yangu hiyo imefutika! Naam, nimepoteza sifa ya kuwa ‘ Mzee wa Dar Es Salaam’!


Ndio, sifa ya kwanza ya kuwa ‘ Mzee wa Dar Es Salaam’ ni lazima uwe na zaidi ya miaka 50, uwe mkazi wa Dar Es Salaam kwa miaka isiyopungua 20 mfululizo! Hilo halijaandikwa popote lakini ‘ Wazee’ wenyewe wa jiji wanauzingatia utaratibu huo.


Siku za karibuni kuna “Kijana wa Dar es Salaam” kaninong’oneza kuwa wako mbioni kuwashawishi wazee wa jiji waongeze sifa za kuwa mzee wa Darisalama. Kwamba ili uwe Mzee wa Dar Es Salaam ni sharti, ama uwe umezaliwa na kukulia Dar, au umezaliwa nje ya Dar lakini ujana wako wote umeishi Dar. Hivyo basi, unapoteza sifa ya kuwa Mzee wa Dar es Salaam kama umekuja Dar ukubwani! Marekebisho hayo ya taratibu na sifa yakifanyika, huenda hata mie nitakuwa na sifa ya kuwa Mzee wa Dar es Salaam.


Na Wazee wa Dar Es Salaam wana Mwenyekiti wao. Kwa kawaida siku ya ‘ shughuli’ ya wazee, huvalia kanzu, kibagharashea na kizibau. Ndiye huyu ambaye huwa wa kwanza kumpokea ‘ Mkuu wa Kaya’ anapoingia ukumbini kuwahutubia wazee.


Ni kwa namna gani basi Mwenyekiti wa Wazee wa Dar Es Salaam anachaguliwa?

Jibu: Hilo ni swali la kizushi na usithubutu kuliuliza mbele ya ‘ Wazee wa Dar es Salaam’- watakutoa mbio kwa bakora! Lakini lililo dhahiri ni kuwa, Wazee Wa Dar Es Salaam hawajawahi kuwa na Mwenyekiti mwanamke. Hata Bi. Titi Mohammed hakupata kufikiriwa. Heshima ya kumpa barabara kuitwa kwa jina lake ilitosha, na amshukuru Julius, wanasema Wazee ‘ orijino’ wa Dar Es Salaam.


Ndio, Mkuu yeyote wa Kaya katika nchi hii atashauriwa aongee mbele ya Wazee wa Dar Es Salaam kama ana kubwa analotaka liwafike wananchi. Ni mara moja katika miaka ya karibuni nimemsikia Rais wa nchi akilihutubia taifa kupitia Wazee wa Mkoa wa Dodoma.


Inasemekana jambo hilo liliwashtua baadhi ya Wazee wa wa Dar Es Salaam. Na kuna siku nilitembea kwa miguu mitaa ya Kariakoo Kusini; Livingstone, Mahiwa, Swahili na mingineyo. Hatimaye nikafika kwenye kijiwe cha chai na kahawa pale Mtaa wa Lumumba. Nilianzisha mjadala juu ya Wazee wa Dar Es Salaam. Na hapo nikayasikia manung’uniko.

Ndio, baadhi ya Wazee wa Dar Es Salaam wanaamini kuwa Ilala ndio Dar Es Salaam. Na kwamba ni Wazee wa Ilala ndio waliompokea Julius Nyerere alipoingia mjini. Wanahoji; Iweje Wazee wa ‘ mashambani’ Kinondoni na Temeke nao waitwe Wazee Wa Dar Es Salaam? Swali linabaki; Wazee Wa Dar Es Salaam ni akina nani?

Maggid Mjengwa,

Iringa,
0788 111 765
mjengwablog.com
 
Daslam hamna wazee kwanza, uzee unaanzia Chalinze wanasemaga wenyewe
 
Wazee wa Dar es salaam ni wachawi wa Dar manake sionagi umuhimu wao. Kwani mikoani hawazeeki?
Huu upuuzi wauwache vibabu vya Dar kujifanya vinawasemea wazee wote Bongo shwain. Kwanza hivii vizee ndo vinakwamisha maendeleo manake vyenyewe ni kushabikia kama upepo kisa ubwabwa wa siku moja na kasoda.
 
Wazee wa kizaramo ndio ki-haki wanatakiwa kuwa wazee wa Dar es salaam. Waliobaki wote ni wakuja tu, watake wasitake.
 
Je ni halali kwa mh. Rais wa nchi kila atakapo kuzungumza na taifa ama kutoa ufafanuzi wa jambo fulani kutumia wazee/makada wa ccm dar es salaam? Je huu uwakilishi ni sahihi kutumika ktk nchi yetu hii iliyodhamiria kufuata mfumo wa vyama vingi?

Mkuu sio sahihi, jambo lingine la kushangaza,,kawaida "maongezi" huwa ni ya pande mbili 'mnaongea" cha ajabu katika "kuongea na wazee" kwa JK utakuta ni yeye tu anaongea/hutubia kisha hadhira inapiga makofi tu kisha wanaondoka na mara nyingi wana appera katika mavazi ya chama cha ccm. Real disguisting!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom