Wazee wa Dar es Salaam ni akina nani?

Kwanini JK asiongee na madaktari kutatua tatizo? Hawa wazee si walidhulumiwa malipo yao katika sakata la EAC na kumwagiwa maji ya pilipili kwa ajili ya kudai madai yao? Leo wanakutana na rais wamshauri nini ikiwa wenyewe waliridhika kudhulumiwa.
 
Ni forum ya kupiga majungu na propaganda ili kuwapaka matope madaktari.
Wengi wa hao wazee wa Dar ni wale ambao hawawezi kuuliza why and how?
Watahubiriwa na kujazwa ujinga, then it will be broadcasted live on TVs.
The same propaganda was used by President Mwinyi in 1990 during the UDSM's saga.
However, report ya Judge Mloso (sikumbuki vizuri jina la judge), ikaja tofauti kabisa na propaganda za Mwinyi.

Ma Dr. Jiandaeni, Hizo propaganda zitawapa zitawapaka matope na kuwatia hasira!

Mkuu uzuri wa wasomi uwa wanabishana kwa hoja na kusimamia kwenye hoja na si propaganda,hizo propaganda ni kujipotezea muda tu kwa hao wapiga propaganda
 
Mkuu Maggid, heshima kwako!

Japo sitojaribu kuwaeleza hawa wazee wa Dar es Salaam ni watu gani nani-wa aina gani, ntasema kidogo yanayohusiana na maongezi yao na bwana mkubwa. Binafsi nafikiri hii kasumba imepitwa na wakati na vile vile viongozi wetu wamepitwa na wakati.

Kwa kifupi hawana umakini na ubunifu wa kuendesha Serikali kwa nyakati hizi tulizopo bado wanafikiri kwamba wanaishi miaka ile ya 60's. Kwenye kile kikao sijawahi kuona hata Mzee mmoja kauliza swali au kufikiri tofauti na mawazo ya bwana mkubwa. Utawaona wakipiga makofi na kufurahi hata pasipo stahili. Hadhara iyo wala si kuongea, imepoteza maana halisi ya kuongea. Maongozi ni shurti pande pande zote mbili zijibishane, lakini kinachotokea pale ni kinyume chake. Bwana mkubwa atafika pale na makabrasha yake atasoma moja mpaka la mwisho na akishamaliza anaondoka zake, wala hasipate nafasi ya kusikia mawazo na maoni ya hao wazee alowaita kuongea nao.

Kiongozi mzuri angetafuta hadhara nzuri ili apate kusikia maoni ya watu wengine wanasemaje kuhusu hoja iliyopo mezani. Kama anataka kuongea na madaktari anaogopa nini kwenda kuongea nao? Uwezi kuwa bondia alafu uishi na kuogopa ngumi za usoni na bado ukajiita bondia. Viongozi wetu hawapendi kutafuta suluhisho la mgogoro badala yake wana kasumba ya kuzunguka zunguka matatizo na kuya-hairisha wakidhani ya kwamba kesho yake mambo yatajipanga yenyewe.

Mchana mwema Mkubwa.
 
Ni vile vizee vichawi vya sisiem, mnakumbuka jk alitukana watumishi wa umma alipokuwa akiongea navyo, aliposema hataki kura zao? AKILI ZA KUAMBIWA UKICHANGANYA NA ZA MBAYUWAYU UNAPATA AKILI ZA BABA MWANAASHA
 
Wazee wa DSM wameshushiwa hadhi pale serikali ilipoanza kutembea na kusomba wanaoimba ""fikira za viongozi zidumu hata kama wamekosea"" halafu wanawaleta kwenye kikao eti
 
hivi mkapa ameshawahi kuongea na hao wachawi wa maendeleo ya nchi? (wazee wa dsm)
 
Mkuu umeniwahi,na wengi ya wazee hao ni kutoka Ilala na Temeke,na hasa wa Ilala wao ndio uwa wanajiita wenye jiji,elimu hawana,maisha ya kueleweka hawana,wao ni vijiweni na story za kale tu na story za Simba,Pan na Young,wazee waliostaarabika wako mbali kabisa na hao wazee!

True dat mkuu!
 
Wazee my foot!!

yani unaenda kuongea na mbuzi, mambo yanayowahusu punda milia?
Si wendawazimu huu!!!
 
Am glad my oldman is not one of them.........

379135_291077990931762_100000886912967_831391_1156534665_n.jpg
 
Hawa ni watu waliochoka na hawana hoja ya msingi kabisa, wako pale kwa ajili ya kupiga makofi na kungojea posho tu, kama angekuwa muungwana basi angeongea na wahariri wa vyombo vya habari kama si waandishi wote.
 
Ndugu yangu Mjengwa,

Kwanza natoa pongezi kwa kuibua mjadala huu.

Mimi binafsi nipo Dar kwa miaka 31 mfululizo lakini jambo ambalo huwa najiuliza ni hivi vigezo vya wazee hawa wa Dar wanavyopatikana na wakawa na tamko dhidi ya wakaazi wote waishio jijini.


nami pia nampongeza mtoa mada.

Mimi ni mzaliwa wa DSM pale Ocean Road Hospital; na maisha yangu yote nipo hapa DSM, na kama kwenda kwetu Morogoro huwa naenda mara chache sana tena baada ya muda mrefu na nakaa huko si zaidi ya wiki.

Kuhusu Wazee wa DSm nimesikia toka enzi za Mwalimu, lakini nami sikupata bahati ya kualikwa katika hivi vikao vya Wazee wa DSM, kwani sasa nami ni mkongwe hapa DSM, huenda hawa wanaoalikwa leo siyo wazawa wa jiji kama nilivyo mimi ni wa kuja toka mikoa mingine.


NAMI NAULIZA SIFA YA KUWA MZEE WA DSM NI IPI??

HUENDA NAMI NATAKIWA NIKAONGEE NA RAISI LEO.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Kwanini JK asiongee na madaktari kutatua tatizo? Hawa wazee si walidhulumiwa malipo yao katika sakata la EAC na kumwagiwa maji ya pilipili kwa ajili ya kudai madai yao? Leo wanakutana na rais wamshauri nini ikiwa wenyewe waliridhika kudhulumiwa.

:lalala:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom