Kujiajiri ni wito wenye mafanikio kama mtu atakubali kufanya kwa kupenda

La3

Member
Jul 29, 2022
13
14
Kujiajiri ni nini? Kujiajiri ni uwezo wa kuwa na chanzo cha kipato kama mtu binafsi, kukianzisha chanzo hicho, kukisimamia, kukiendesha, kukiinua kutoka chini na kukiendeleza.
Kujiajiri ni wito unaokuja ndani ya mtu mwenyewe bila sababu nyingine yoyote isipokuwa mtu mwenyewe amependa kujiajiri, ni msukumo wenye shauku ya kupenda kufanya kitu kutoka ndani ya mtu mwenyewe.

Pamoja na kwamba tatizo la ukosefu/ uhaba wa ajira ni kubwa sana nchini na duniani kote, kujiajiri bado kunabaki kuwa ni wito kutoka ndani ya mtu kwa sababu sio kila mtu aliyejiajiri anaweza kufanya kwa mafanikio makubwa kama ambavyo wengine wameweza. Kujiajiri sio kazi nyepesi kwamba kila mtu anaweza, kujiajiri kunahitaji moyo wa kujitoa kweli kweli kama ambavyo wanajeshi wanajitolea vitani.
Sasa kuwa msomi hakumaanishi anaweza kujiajiri, ndio maana kuna wasomi (wengine maprofesa kabisa) wameshindwa kujiajiri wakati huohuo watu wa elimu ya darasa la saba wameweza.
Kujiajiri haipaswi kuwa ni kazi ya kufanywa na watu waliokosa ajira, au waliofeli shule , uhaba wa ajira, n.k
Kujiajiri kunapaswa kuwa kitu kinachomvutia mtu anayetaka kujiajiri ( mwenye wito wa kujiajiri) yaani mtu mwenyewe avutiwe (apende) kuwa na mradi wake au biashara yake binafsi.

Sasa kujiajiri sio kazi nyepesi inayoweza kufanywa na kila mtu. Ndio maana hata walimu wengi wa ujasiriamali vyuoni wameshindwa kuwa na mradi hata mmoja wa kuwaingizia fedha tofauti na kazi zao, wanahamasisha wanafunzi kufanya biashara au kujiajiri, vitu ambavyo wao wenyewe hawawezi. Hata hawa wanasiasa wanaohamasisha vijana wajiajiri wao wenyewe pia wameshindwa kuacha kazi zao wajiajiri. Kama wenyewe tu hawawezi kujiajiri wanawezaje kuhamasisha wengine kujiajiri.
Kwenye kujiajiri ujasiriamali hauepukiki.

Sasa mabadiliko yafuatayo ni lazima yafanyike Ili eneo hili la kujiajiri lipate matokeo chanya;

1. Walimu wa ujasiriamali vyuoni ni lazima wawe na mradi hata mmoja wa mfano wa kuigwa Ili wafuzu kupata ajira ya ualimu wa ujasiriamali.

Kama ambavyo nimesema hapo mwanzoni kwamba katika kujiajiri, ujasiriamali hauepukiki, Ili mtu afanikiwe katika ajira binafsi ni lazima awe mjasiriamali.
Kuna ulazima wa kuwaondoa kazini wahadhiri wa kozi ya ujasiriamali na kozi nyingine za biashara ambao hawana mradi hata mmoja wa mfano.
(Hawa hawana sifa ya kufundisha masomo hayo, ni sawa na kufundishwa utakatifu na mchungaji mzinzi).
Ni uendawazimu mhadhiri anapokuambia kwamba hata hiyo kazi yake ya kufundisha ni ujasiriamali.
Ili vijana wahamasike kupenda kujiajiri basi;
Sifa kuu ya kwanza wanayotakiwa kuwa nayo walimu wa somo la ujasiriamali iwe ni kuwa na mradi mmoja wa mfano wa kuigwa kwa wanafunzi wake.
Huwezi kumpa kazi ya kufundisha ujasiriamali mtu ambaye yeye mwenyewe ameshindwa, Sasa vijana watahamasikaje? Hawa walimu wa ujasiriamali na biashara walioshindwa kujiajiri waondolewe kazini sababu wanalipwa mishahara bure tu.
Hawana maana, sababu vijana wengi bado wanashindwa kujiajiri.

Mhadhiri wa ujasiriamali hana hata mradi wa kuku wa kienyeji, ondoeni hawa wote, wekeni, wale wenye miradi yao binafsi ya kijasiriamali, na miradi yenyewe iwe inaingiza angalau, kiasi cha fedha kikubwa Kwa mwezi ndipo wanafunzi vyuoni watahamasika kufanya ajira binafsi katika nyakati hizi ambazo kupata ajira ni bahati sana.
Kuajiri wahadhiri hawa wenye miradi yao binafsi kunaweza kuchangia mafanikio kwenye eneo hili la kujiajiri kwa sababu itawatia morali vijana kupenda kujiajiri hata kama wakiajiriwa.

2.Mitaji
Changamoto ya vijana wengi kushindwa kujiajiri ni mitaji. Mikopo sio mizuri sana kuikimbilia.
Mikopo ya serikali (mikopo ya halmashauri) kabla ya kutolewa kwa hawa vijana wanatakiwa kuandika mpango wa biashara au mpango wa mradi.
Nasema hivi sababu biashara nyingi zinazoanza leo, miaka kadhaa ijayo zitakuwa zimekufa.
Bila mipango ya biashara mikopo isitolewe labda kama mnafanya ufadhili.
Zamani urithi kutoka kwa wazazi ilikuwa ni ardhi, lakini Miaka ya hivi karibuni wazazi walikuwa wakisema urithi wa mtoto ni elimu kwa sababu ya uchache/ ufinyu wa ardhi.
Sasa mambo yamebadilika, hali ni tofauti, tatizo la ukosefu wa ajira ni kubwa na litaendelea kuwa kubwa kadri wasomi wanavyoongezeka.
Leo hii ni kawaida nafasi 10 za ajira kugombaniwa na watu 1000.
Kwa hiyo wazazi ni lazima wamuandalie mtoto urithi wa elimu pamoja na kumuandalia mtaji wa kuanzia ujasiriamali.
Mikopo sio kitu cha uhakika kuweza kufanyia biashara.

Soma Kwa utulivu, hapa naongea na wazazi wa sasa na wale wa vizazi vijavyo; Mfano kule Njombe, Iringa, Lushoto-Tanga, au Mbinga Ruvuma; wazazi wanaweza kuwaandalia shamba la miti ya mbao, milunda, nguzo za umeme au miti ya parachichi angalau ekari moja au mbili kwa kila mtoto kama mtaji wa kuanzia badala ya kurithisha shamba tupu. Mradi uwekezwe tangu akiwa elimu ya ngazi ya chini mfano hata darasa la kwanza.
Pamoja na kwamba vijana hawapaswi kufikiria urithi kutoka kwa wa wazazi, ni lazima wazazi waandae msingi wa mitaji kwa vijana wao na ni aibu kubwa mno kwa mzee mtu mzima kufariki bila kuacha urithi Kwa vizazi vingi.
Sasa ardhi ni chache, lakini katika uchache huo, wanaweza kuiongezea thamani kwa kupanda hiyo miti.
Na kama unataka shamba la kununua, nenda ulizia, wapo wengi wanaouza ardhi na kukimbilia mijini.

Au kule Mbozi-Songwe, Mbinga-Ruvuma, Kilimanjaro au Kagera wazazi wanaweza kuwaandalia watoto shamba la kahawa ekari moja kwa kila mtoto kama mtaji wa kuanzia.
Thamani ya ardhi inaongezeka kila siku.
Au kule Singida na Tabora wazazi wanaweza kuwaandalia watoto shamba lenye mizinga kadhaa ya nyuki kama mtaji wa kuanzia kwa vijana wao.
Waandalieni urithi wa ardhi iliyoongezewa thamani kwa ufugaji wa nyuki.
Aamue yeye kuendeleza au auze aanzishe biashara nyingine. Ingawa hakuna aliyeuza ardhi ya urithi mwenye maisha mazuri.

Au kule Lindi na Mtwara wazazi wanaweza kuwaandalia watoto shamba la mikorosho angalau ekari moja kwa kila mtoto kama mtaji wa kuanzia.

Kule Makete-Njombe kuna wakinga wamewekeza mashamba ya miti Kwa ajili ya mitaji ya kibiashara kwa watoto na wajukuu.
Na vijana wengi wa makete wamepata mitaji kutokea kwenye mashamba hayo.

Au wakulima wa chai kule Rungwe-Mbeya, Mafinga-Iringa na Njombe watenge mashamba ya chai ekari moja au zaidi kama urithi wa mitaji Kwa watoto.

Hata Kwa wafugaji, mifugo kadhaa iwekwe kama urithi wa mitaji Kwa watoto, wajukuu na vizazi vinavyofuata.

Wazazi wawekeze kwenye soko la hisa, kwamba hisa hizi ni za mtoto huyu, hizi ni za mtoto huyu. Hii itasaidia sana vijana kupata mitaji.
Wazee wa zamani waliacha urithi wa ardhi, ninyi wa sasa muache urithi wa ardhi yenye kitu cha thamani kwa sababu ardhi ni bidhaa adimu (chache sana) nyakati hizi na miaka ijayo.

Msisikilize wapumbavu wanaosema ardhi bado ni kubwa, ardhi haiongezeki.
Kutokana na changamoto kubwa ya ajira nyakati hizi;
Urithi kwa mtoto kipindi hiki ni 1.elimu pamoja na
2.mtaji wa kuanzia.
(Mtaji wa kuanzia ni kama nilivyoelezea hapo juu). Ikiwezekana katika hili, changamoto ya vijana kushindwa kujiajiri Kwa kisingizio cha mtaji itakuwa imetatuliwa.
NB; Kila mtu anayeleta watoto duniani kwa sasa anawajibika kuandaa urithi wa elimu na mtaji kuanzia maisha.

3. Sapoti kutoka serikalini.
Ni kweli serikali imejitahidi kufanya vizuri katika kuwapatia vijana mikopo kwa vikundi mbalimbali, lakini ni muhimu ikalegeza na kuruhusu kijana mmoja mmoja kuweza kuchukua mkopo, sababu wanapokuwa kundi, ni rahisi mmoja wao kutoka na kiasi cha fedha ambacho wamekopa Kwa pamoja kama kikundi. Siku hizi waaminifu ni wachache sana. Nimeshuhudia mahali pengine kwamba kuna vijana walikopa pesa halmashauri lakini mwenzao mmoja akakimbia na fedha zote.

4. Vijana wanaweza kujiajiri katika maeneo mengi, hasa ambavyo Wana elimu au ujuzi nayo ni nzuri zaidi,
Mfano fundi umeme wa majumbani anaweza kufanya kazi zake pamoja na duka la vifaa vya umeme Ili mteja akimpa kazi, vitendea kazi anachukua dukani kwake.
Ni faida kwake kwamba bidhaa zinauzika, pili wateja wanamfuata ofisini kwake tofauti na fundi asiye na ofisi.
Pia mafundi wasio na maduka ya vifaa vya umeme wanakuja kununua kwake.

Au fundi bomba anaweza kuwa na duka la vifaa vya bomba Ili akipata kazi, vifaa anachukua dukani kwake.
Pia wateja wengi wanamfuata ofisini kwake tofauti na fundi asiye na ofisi. Pia mafundi wasio na maduka ya vifaa vya bomba wanakuja kununua vifaa kwake.
Au fundi kujenga akiwa na duka la hardware, vifaa anachukua dukani kwake mwenyewe.
Naye wateja wengi wanamfuata ofisini kwake tofauti na fundi asiye na ofisi.

Au fundi simu, redio, runinga na tarakilishi akiwa na duka la vifaa hivyo, akipata kazi vifaa anachukua dukani kwake mwenyewe. Biashara hii ni nyepesi na bora zaidi kuliko nyingine.

5. Mtu anapojiajiri anatakiwa atambue kwamba ana jukumu la kutengeneza ajira Kwa wengine. Unapojiajiri unatakiwa utambue kwamba wewe ndio unapaswa kutumia akili zaidi kuliko walioajiriwa. Kila kitu kwenye biashara au mradi wako vinakutegemea wewe zaidi katika uendeshaji.
Aliyejiajiri ana kazi ngumu zaidi kuliko aliyeajiriwa.

Mtu mwingine anaweza kudhani yupo huru Kwa sababu yeye ni bosi, sio kweli, anayejiajiri hayupo huru, yeye ndiye moyo wa biashara, kuanguka au kuinuka Kwa biashara kunamtazama yeye zaidi.

6. Vijana wasijiajiri kwa sababu wamekosa ajira au kwa sababu wamefeli shule. Kujiajiri ni wito, sio kila mtu anaweza kufanya. Ni vizuri mtu mwenyewe akapenda kufanya mwenyewe kutoka moyoni mwake. Jambo hili likifanywa Kwa kupenda Lina matokeo mazuri zaidi kuliko likifanywa bila kuwa tayari kukabiliana na changamoto yoyote inayoweza kujitokeza kutishia au kutikisa biashara Yako. Ushindi kwenye shughuli zako utategemeana na utayari wako wa kupambana.

7. Nguvu ya rohoni.
Nguvu ya rohoni haiepukiki katika jambo lolote iwapo unataka kufanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu.
Utake usitake ni lazima ukubali nguvu ya rohoni itumike katika shughuli zako za kila siku. Kuna watu wanakesha Kwa waganga, wengine wanafanya mambo ya aibu na waganga Ili mambo yaende.

Lakini pamoja na haya yote ipo nguvu ya rohoni kutoka kwenye Nuru (mwanga) nayo ni nguvu ya MUNGU ambayo ina nguvu kubwa sana kuliko Giza la kuzimu. Lakini nguvu hii ya nuru inahitaji utakatifu wa hali ya juu na kujiepusha na anasa zote tofauti giza.
Faida za kujiajiri;
Matokeo ya kujiajiri;
Changamoto za kujiajiri;
Namna ya kuzikabili;
 
Kujiajiri ni wito unaokuja ndani ya mtu mwenyewe bila sababu nyingine yoyote isipokuwa mtu mwenyewe amependa kujiajiri, ni msukumo wenye shauku ya kupenda kufanya kitu kutoka ndani ya mtu mwenyewe.

Huu ni wito kwa sababu sio kila mtu anaweza kufanya kwa mafanikio makubwa kama ambavyo wengine wameweza. Kujiajiri sio kazi nyepesi kwamba kila mtu anaweza, kujiajiri kunahitaji moyo wa kujitoa kweli kweli kama ambavyo wanajeshi wanajitolea vitani. Sasa kuwa msomi hakumaanishi anaweza kujiajiri.

Ndio maana hata walimu wengine wa ujasiriamali vyuoni wameshindwa kuwa na mradi hata mmoja wa kuwaingizia fedha tofauti na kazi yake, hata hawa wanasiasa wanaohamasisha wengine wajiajiri wao wenyewe wameshindwa kuacha kazi zao wajiajiri. Kwenye kujiajiri ujasiriamali hauepukiki.

Sasa mabadiliko yafuatayo ni lazima yafanyike Ili eneo hili la kujiajiri lipate matokeo chanya;

1. Walimu wa ujasiriamali vyuoni ni lazima wawe na mradi hata mmoja wa mfano wa kuigwa Ili wafuzu kupata ajira ya ualimu wa ujasiriamali.

Kama ambavyo nimesema hapo mwanzoni kwamba katika kujiajiri, ujasiriamali hauepukiki, Ili mtu afanikiwe katika ajira binafsi ni lazima awe mjasiriamali. Kuna haja ya kuwaondoa kazini wahadhiri wa kozi ya ujasiriamali na kozi nyingine za biashara ambao hawana mradi hata mmoja, badala yake muanze kuweka sifa ya wahadhiri hawa wa ujasiriamali kuwa na mradi wowote Ili kuwapa hamasa wanafunzi kupenda kujiajiri.

Utapata kuona kwamba mhadhiri mwingine bila aibu, anafundisha kwamba hata yeye anavyofundisha ni ujasiriamali, mambo gani haya?

Mhadhiri wa ujasiriamali hana hata mradi wa kuku wa kienyeji, ondoeni hawa wote, wekeni, wale wenye miradi yao binafsi ya kijasiriamali, na miradi yenyewe iwe inaingiza angalau, kiasi cha fedha kikubwa Kwa mwezi ndipo wanafunzi vyuoni watahamasika kufanya ajira binafsi katika nyakati hizi ambazo kupata ajira ni bahati sana.
Kuajiri wahadhiri hawa wenye miradi yao binafsi kunaweza kuchangia mafanikio kwenye eneo hili la kujiajiri.

2.Mitaji
Changamoto ya vijana wengi kushindwa kujiajiri ni mitaji. Mikopo sio mizuri sana kuikimbilia.
Kama ambavyo miaka ya hivi karibuni wazazi walikuwa wakisema urithi wa mtoto ni elimu, Sasa Hali ni tofauti, tatizo la ajira ni kubwa, wazazi ni lazima wampe mtoto urithi wa elimu pamoja na mtaji wa kuanzia.

Soma Kwa utulivu, hapa naongea na wazazi wa sasa na wale wa vizazi vijavyo; Mfano kule Njombe, Iringa, Lushoto-Tanga, au Mbinga Ruvuma; wazazi wanaweza kuwaandalia shamba la miti ya mbao, milunda, nguzo za umeme au miti ya parachichi angalau ekari moja au mbili kwa kila mtoto kama mtaji wa kuanzia badala ya kurithisha shamba tupu.

Au kule Mbozi-Songwe, Mbinga-Ruvuma, Kilimanjaro au Kagera wazazi wanaweza kuwaandalia watoto shamba la kahawa ekari moja Kwa Kila mtoto kama mtaji wa kuanzia
Au kule Singida na Tabora wazazi wanaweza kuwaandalia watoto shamba lenye mizinga kadhaa ya nyuki kama mtaji wa kuanzia.

Au kule Lindi na Mtwara wazazi wanaweza kuwaandalia watoto shamba la mikorosho angalau ekari moja Kwa Kila mtoto kama mtaji wa kuanzia.

Kule Makete-Njombe kuna wakinga wamewekeza mashamba ya miti Kwa ajili ya mitaji ya kibiashara kwa watoto na wajukuu.

Au wakulima wa chai kule Rungwe-Mbeya, Mafinga-Iringa na Njombe watenge mashamba ya chai ekari moja au zaidi kama urithi wa mitaji Kwa watoto.

Hata Kwa wafugaji, mifugo kadhaa iwekwe kama urithi wa mitaji Kwa watoto, wajukuu na vizazi vinavyofuata.
Wazee wa zamani waliacha urithi wa ardhi, ninyi wa sasa muache urithi wa ardhi yenye kitu Cha thamani kwa sababu ardhi ni bidhaa adimu (chache sana) nyakati hizi na miaka ijayo.

Msisikilize wapumbavu wanaosema ardhi bado ni kubwa, ardhi haiongezeki.
Kutokana na changamoto kubwa ya ajira nyakati hizi. Urithi kwa mtoto kipindi hiki ni elimu pamoja na mtaji wa kuanzia.(Mtaji wa kuanzia ni kama nilivyoelezea hapo juu). Ikiwezekana katika hili, changamoto ya vijana kushindwa kujiajiri Kwa kisingizio cha mtaji itakuwa imetatuliwa.

3. Sapoti kutoka serikalini.
Ni kweli serikali imejitahidi kufanya vizuri katika kuwapatia vijana mikopo kwa vikundi mbalimbali, lakini ni muhimu ikalegeza na kuruhusu kijana mmoja mmoja kuweza kuchukua mkopo, sababu wanapokuwa kundi, ni rahisi mmoja wao kutoka na kiasi cha fedha ambacho wamekopa Kwa pamoja kama kikundi. Siku hizi waaminifu ni wachache sana. Nimeshuhudia mahali pengine kwamba kuna vijana walikopa pesa halmashauri lakini mwenzao mmoja akakimbia na fedha zote.

4. Vijana wanaweza kujiajiri katika maeneo mengi, hasa ambavyo Wana elimu au ujuzi nayo ni nzuri zaidi,
Mfano fundi umeme wa majumbani anaweza kufanya kazi zake pamoja na duka la vifaa vya umeme Ili mteja akimpa kazi, vitendea kazi anachukua dukani kwake.

Au fundi bomba anaweza kuwa na duka la vifaa vya bomba Ili akipata kazi, vifaa anachukua dukani kwake.
Au fundi kujenga akiwa na duka la hardware, vifaa anachukua dukani kwake mwenyewe.

Au fundi simu, redio, runinga na tarakilishi akiwa na duka la vifaa hivyo, akipata kazi vifaa anachukua dukani kwake mwenyewe. Biashara hii ni nyepesi na bora zaidi kuliko nyingine.

5. Mtu anapojiajiri anatakiwa atambue kwamba ana jukumu la kutengeneza ajira Kwa wengine. Unapojiajiri unatakiwa utambue kwamba wewe ndio unapaswa kutumia akili zaidi kuliko walioajiriwa. Kila kitu kwenye biashara au mradi wako vinakutegemea wewe zaidi katika uendeshaji.

Mtu mwingine anaweza kudhani yupo huru Kwa sababu yeye ni bosi, sio kweli, anayejiajiri hayupo huru, yeye ndiye moyo wa biashara, kuanguka au kuinuka Kwa biashara kunamtazama yeye zaidi.

6. Vijana wasijiajiri kwa sababu wamekosa ajira au kwa sababu wamefeli shule. Kujiajiri ni wito, sio kila mtu anaweza kufanya. Ni vizuri mtu mwenyewe akapenda kufanya mwenyewe kutoka moyoni mwake. Jambo hili likifanywa Kwa kupenda Lina matokeo mazuri zaidi kuliko likifanywa bila kuwa tayari kukabiliana na changamoto yoyote inayoweza kujitokeza kutishia au kutikisa biashara Yako. Ushindi kwenye shughuli zako utategemeana na utayari wako wa kupambana.

7. Nguvu ya rohoni.
Nguvu ya rohoni haiepukiki katika jambo lolote iwapo unataka kufanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu.
Utake usitake ni lazima ukubali nguvu ya rohoni itumike katika shughuli zako za kila siku. Kuna watu wanakesha Kwa waganga, wengine wanafanya mambo ya aibu na waganga Ili mambo yaende.

Lakini pamoja na haya yote ipo nguvu ya rohoni kutoka kwenye Nuru (mwanga) nayo ni nguvu ya MUNGU ambayo ina nguvu kubwa sana kuliko Giza la kuzimu.
Kweli umejitetea new member,uraiani kutamu ukiwa na kitu Cha kukuingizia hela,Haya Mambo ungepigs kelele ukiwa Bado uko chuoni,ungekuta mambo mswanu(mazuri)Uraiani!
 
Back
Top Bottom