wazazi kulazimisha nikaoe kijijini

Ishi na huyo mpenzi wako, zaa naye mtoto baadaye mbariki ndoa!

Some wazazi, du! Pole lkn.
 
wazazi ni mungu wa pili katka maisha yako na wanajua meng kuliko wewe. Hata kama wewe una elimu ya kidunia lakin wao kama wazazi kamwe hawawezi kukuambia kitu ambacho kitakuwa na matokeo mabaya. Hebu rudisha moyo wako kwa wazaz wako. Labda kuna kitu ambacho hujajua. Kuna familia ambazo hawaolew na hata kama wakiolewa hawaishi na wanaume zao. Kuna wengne kwao kituo cha polis ni kama banda la kuku saa zote yeye ana kesi. Kuna wengne hata ukifanyaje yeye ndio kwanza anahamisha mali kupeleka kwa nduguze. Kuwa makni sana kaa na wazazi wako wakueleze vizur kwan si vema kuoa mwanamke ambaye wazazi hawatawasiliana nae.
 
Je ndugu zao...Baba Mkubwa/Mdogo...Mjomba na Shangazi wote lao moja?? Hakuna mwenye upeo wa kuwakalisha chini na kuwapa darsa kidogo wakalegeza msimamo na kuheshimu maamuzi yako??
 
Hizi sio zama za kuchaguliana wake..
Kwa sababu una mpango wa kuoa next year endelea kutafuta mbinu za kuwaconvice kuwa unae mtu tayari mnayependana
Tumia hata wazee wa kijijini wenye hekima zao.
 
Ishi na huyo mpenzi wako, zaa naye mtoto baadaye mbariki ndoa!

Some wazazi, du! Pole lkn.

Sasa my dear Kaunga hapa si unakuwa unawashauri waishi katika uzinzi?? Je in between kabla ya kubariki iyo ndoa mungu akampenda mmojawapo zaidi.....
 
Je ndugu zao...Baba Mkubwa/Mdogo...Mjomba na Shangazi wote lao moja?? Hakuna mwenye upeo wa kuwakalisha chini na kuwapa darsa kidogo wakalegeza msimamo na kuheshimu maamuzi yako??


ok, nimekusoma mkuu. Ngoja nitajaribu kuwashirikisha..
 
Mke Unaoa ili uishi naye au akaishi na wazazi wako? Kama ataishi na wazazi wako go ahead, lakini kama utaishi naye wewe then you need to think otherwise. Mi nafikiri ni vyema kuoa mke unayempenda wewe kwa dhati na siyo kuchaguliwa na wazazi. Mke mwenyewe toka kijijini, tabia zitaendana kweli? Upeo wa kufikiri na mabadiliko na changamoto za mjini ataziweza kweli? Hao wa vijijini si ndio wakija mjini huzibuka na kuangukia kwenye mikono ya ma-pedeshee na kuleta mtafaruku ndani ya familia? Tafakari!
 
nahisi wazazi wako wanasumbuliwa na ukabila zaidi, hayo mambo siku hizi yamepitwa na wakati, unabidi uwe na msimamo sana katika maamuzi yako. najuwa unawaheshimu sana wazazi wako, na ni haki yao kuheshimiwa, naomba ukae na wazazi wako ongea nao kwa upole na kuwaeleza maamuzi yako, ikishindikana washirikishe ndugu zako wa karibu, nayo ikishindikana wahusishe viongozi wa dini, sikushauri kabisa kuoa mtu usiye mjua wala kumpenda lazima itakuwa ndoa ya machungu, siku nzote upendo huziba mapungufu mengi kwenye ndoa, sasa hiyo ndoa ambayo haina upendo unadhani itahimili misukosuko ya ndoa, au ndio kuachana baada ya muda. sikushauri kabisa huo ujinga wa kuchaguliwa, umeshapitwa na wakati ndugu.
 
Back
Top Bottom