Mkwawe
JF-Expert Member
- Jun 10, 2016
- 2,345
- 4,168
Katika miaka kadhaa nyuma wazanzibari walikuwa wakilalamika sana kuhusu kinachoitwa "unyonyaji" na "kukaliwa kimabavu" na watu wa "Bara" ( silipendi hili jina bara) ambayo ndiyo Tanganyika yetu. Kuna wakati sisi raia mmoja mmoja kutoka upande huu wa Tanganyika tulikuwa tukiwabembeleza sana hawa ndugu zetu kuwa shutuma mnazozotutolea si za kweli maana mtanganyika mmoja mmoja hafaidiki na chochote juu ya huu Muungano wa kipumbavu ambao tunao ila pengine mzanzibari ndiye mwenye ahueni nao
"Ndugu" zetu hawa miaka nenda miaka rudi wakawa wanasema hatutaki "mkoloni" mweusi kwenye ardhi yetu ambayo ni Zanzibar ilhali uhalisia unajulikana wazi kabisa nani ni mnyonyaji wa mwenzie
Umefika wakati mahususi kabisa kwa wazanzibari kupata kile ambacho mmekuwa mkikililia kwa miongo kadhaa sasa ila naona mmenogewa na kuibomoa Tanganyika kwa kushirikiana wasaliti wa Tanganyika yetu na mnaona kila kinachofanywa kwa majira haya ni sawa kabisa kwa kuwa tu hakiwaathiri nyie.
Huu ndiyo muda ambao sisi "wabara" (au machogo Kama mnavyotuita) pamoja na nyie wazanzibari tuunganishe nguvu zetu ili kila mmoja abaki stahiki yake, ilibidi majira haya nyie wazanzibari kuungana nasi watanganyika kuwaambia watawala kuwa huu uhusiano unatosha na inabidi uvunjwe ila kila ajiendeshe anavyojua yeye.
Lakini GHAFLA wazanzibari mmebadili upepo, eti sasa hivi na nyie mnaongelea utaifa! Daah aisee sijategemea kwa kweli lakini mnapaswa kujua kuwa haya mambo sisi ndiyo kwa nyakati hushika mpini hivyo kwa mustakabali wa visiwa vyenu huu ndiyo muda sahihi wa kujichukulia mamlaka yenu HAKUTAKUWA NA WAKATI MWINGINE maana watanganyika wengi tumeshajua tunaishi na watu wanafiki kiasi gani