Kinkunti El Perdedo
JF-Expert Member
- Nov 28, 2020
- 4,647
- 11,392
Utaifa ni jambo ambalo mataifa yote duniani huulinda kwa nguvu zote,hakuna taifa lenye watu wenye akili timamu wako tayali kuona utaifa wao unachezewa hovyo,hili tuna liona kwa mifano michache kupitia mataifa kadhaa mfano ni mgogoro wa Israel na Palestine.
Ni mvutano wa uwepo na utetezi wa utaifa kwa pande zote mbili, nguvu ya mapambano imesukumwa na uzalendo halisi juu ya kufia utaifa wao kwa manufaa ya kizazi Cha sasa na kijacho.
Baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar hapo 1964 na kuundwa kwa taifa la Tanzania.Watanganyika walipoteza utaifa wao na taifa lao la Tanganyika na kujivika utaifa mpya kwenye taifa jipya la Tanzania.
Kwa upande wa pili Wazanzibar wakisukumwa na uzalendo halisi na ulio thabiti juu ya taifa lao na utaifa wao,waligoma kupoteza taifa lao na utaifa wao kama Wazanzibar kama walivyo fanya Watanganyika kwa kujivika koti la muungano.
Leo hii Zanzibar wana serikali Yao kwa mujibu wa katiba yao nje na katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya 1977.Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ipo kwa ajili ya kutetea na kulinda maslahi ya Zanzibar na Wanzibar.Lakini hakuna serikali wala katiba ya kulinda maslahi ya Tanganyika na Watanganyika.
Wazanzibar wameweka mipaka na ukomo kwa wasio Wazanzibar kujadili mambo yanayo husu Zanzibar ndio maana Wana Bunge lao na bajeti yoa,hili pia lipo katika fursa mbalimbali mwiko kabisa kwa mtu asiye Mzanzibar kufaidika na fursa ambazo zipo kwa ajili ya Wazanzibar mfano ajira,kumiliki ardhi nk ,hali ni tofauti kwa Tanganyika ambapo hakuna sehemu ya kulinda maslahi ya Watanganyika Wala ukomo kwa wasio Watanganyika kujadili mambo ya Tanganyika ndio maana hatuna Bunge la Tanganyika Wala bajeti ya Tanganyika kama ilivyo kwa Zanzibar.
Wazanzibar wanalinda rasilimali muhimu kwa ajili yao wenyewe mfano,mafuta,gesi,bandari
nk,kwa kuyafanya sio mambo ya muungano lakini Watanganyika rasilimali zetu tumezifanya kuwa kama karanga kwa Wazanzibar kupata gawio la pesa na ajira uku kukiwa hakuna gawio maalumu kwa Tanganyika.
Katika nafasi za kisiasa mwiko kwa wasio Wazanzibar Kushika nafasi za ngazi mbalimbali za kisiasa ndani ya visiwa,lakini ni fursa kwa Wazanzibar Kushika nafasi za kiserikali ndani ya jamhuri kwa mgongo wa muungano uku Watanganyika hawana fursa hiyo kupitia Tanganyika yao bali muungano.
Ni kheri umaskini wa pesa sio umasikini wa akili na fikra.Watanganyika tumekosa vyote pesa hakuna na akili hatuna.Tumepoteza taifa letu na utaifa wetu uku watu wachache wakiona umuhimu wa kulinda taifa lao na utaifa wao.
Hongera kwa Wazanzibar kwa kuwa Wazalendo kwa taifa lenu na kulinda kilicho chenu kwa maslahi ya taifa lenu na utaifa wenu.
RIP mchungaji Christopher Mtikila
G-55.