abdulahsaf
JF-Expert Member
- Aug 31, 2010
- 858
- 130
Wazanzibari Slough UK wakusanyika Iydul Adh-ha
Nae Ustadh Omar Amiri wa Jumuiya ya Wazanzibari waishio Slough – Uk. baada ya swala ya iyd ul adh'ha alitoa khutbah ambayo ilizungumzia umoja na mshikamano kwa waislam, ambayo kwa kiasi kikubwa ilisisitiza kwa waislam wote duniani kutokubali kudhalilishwa na kudhulumiwa haki zao.
Kadhalika Ustadh Omar aligusia vipengele muhimu sana katika historia ya dini yetu pale ambapo Mtume wetu Muhammad (saw) alivitaja katika hijjatul wada'a pale aliposema kua " msidhulumiane, msizidishiane bei, msitukanane, msidharauliane, ni haramu kwa kila Muislam kumwaga damu ya Muislam mwenzake, kumvunjia hadhi na heshima yake, ikiwa anayahusisha haya na yale yanayofanyika Zanzibar, khususan kwa kile alichokiita ufedhuli wa wazi kwa masheikh na wanazuoni wa kizanzibari ( Sheikh Farid, Sheikh Mselem, Sheikh Azzan, Sheikh Mussa Juma na wenziwao.
kadhalika Ustadh Omar , alisema hichi wanachofanyiwa hawa Masheikh wa Zanzibar, ni kuendeleza sera za makafiri duniani na wasioupendelea kheri Uislam kwa vile haya alifanyiwa Sheikh Kishk wa Misr, Sheikh Aboud Rogo wa Mombasa Kenya na leo tunayaona haya kwa masheikh wetu wa zanzibar suala mbalo ni haramu kulivumilia.
Aidha amewataka waisilamu kuifahamu hadithi ya Bwana Mtume (saw) pale aliposema mmoja wenu akiuona uovu basi auondoe kwa mkono wake, na ikiwa hawezi kuuondoa kwa mkono wake basi ausemee (kwa mdomo wake ) na ikiwa hawezi kufanya hivyo basi achukie kwa moyo wake , lakini hiyo ni imani ya daraja la chini.
Alisema basi jee hawa viongozi wa Zanzibar ndio hawawezi hata kusemea au kuchukia kwa nafsi uovu huu na dhulma hizi juu ya Zanzibar na yale wanayofanyiwa wanazuoni wa Zanzibar ambao wanarithi kazi za Mitume kama alivyosema ,tume Muhammad (saw) ?
Pia masheikh wote wanaoshuhudia haya kwa Zanzibar hawaoni kama huu ni unafiq wa wazi ambao utawapeleka motoni siku ya qiyama. Kama ule unafiki wa wazi unaofanywa na Soraga ambae yeye sio Sheikh bali ni mtu ambae analinda tonge.
Imewekwa na MAPARA at 10:19 AM