Waziri Lukuvi amenukuliwa na Mwananchi leo kuwa Serikali itahakikisha wauwaji wa Kamanda RPC Barlow wanakamatwa. Kauli yake imenifariji sana na inaonyesha kuwa inao uwezo na itautumia kuwashika wauwaji hao.
Hata hivyo, napenda kutahadharisha kuwa kukamatwa kwa wauwaji hao na kushindwa kuwakamata wauwaji wa Makada wa CDM; Mbwana Masudi na Msafiri Mbwambo kwenye chaguzi ndogo za Igunga na Arumeru Mashariki kunaweza kuleta tafsiri ya kuwa kuna baadhi ya Watanzania uhai wao una thamani kuliko wengine.