Waumini wa dini ya Rastafari(Rastafarians) wapata afueni mahakamani baada ya kuwasilisha kesi dhidi ya Olympic High School

pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,923
13,344
1886448.jpg
Babaye mwanafunzi wa kike, 15 aliyefukuzwa shule kwasababu ya 'rasta'(mwenye miwani) akiwa na wenzake mahakamani.---Wanachama wa Rastafarian Society of Kenya wakifatilia kesi mahakamani.
rastafari.png
Kisa binti ya mmoja wa waumini wao kunyimwa nafasi ya kujiunga na shule hiyo ya sekondari kwasababu ya mtindo wake wa nywele, 'dreadlocks', almaarufu rasta. Jaji aliamuru bodi ya shule hiyo kuhakikisha mwanafunzi huyo atakubaliwa kuendelea na masomo yake bila ubaguzi wowote dhidi yake kwasababu ya dini yake. Kupitia wakili wao Wambui Shadrak mzazi alieleza mahakama kwamba ni mwanachama wa Rastafarian Society of Kenya na kwamba amemlea binti yake kwenye dini ya Rastafari.https://citizentv.co.ke/news/nairob...allow-rastafarian-girl-resume-studies-229017/
 
Walipowasilisha kesi yao mahakamani na kudhibitishia jaji kwamba dini yao haikubali waumini wake kunyoa nywele. Wakili wao alisema haikubaliki kisheria chini ya katiba mpya ya Kenya kwa wananchi kubagulia kwasabu ya dini zao. Hakimu aliamuru mwanafunzi akubaliwe kuendelea na masomo yake, maamuzi ya mwisho yatatolewa na mahakama ifikapo tarehe 3 mwezi wa Mei. Ni kiashiria kizuri sana kisheria kuona wakenya wakiamini mahakama zao na pia wakifahamu ipasavyo haki zao za msingi ambazo zimelindwa chini ya katiba ya Kenya. https://citizentv.co.ke/news/rastaf...r-kicking-out-daughter-over-dreadlocks-226722
 
Bhangi a.k.a Cannabis sativa nayo ni sehemu ya ibada yao. Hiyo shule ijipange mfereji wa maji taka umeelekezwa huko kupitia katiba na wanasheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbuka kwamba katiba hiyo inayowalinda imeharamisha matumizi ya bangi, iwe shuleni au nyumbani, na katiba hiyo hiyo pia imewapa uhuru wanafunzi waislamu kuvaa hijab mashuleni.
 
Ukisikia mkorogo au zege ndio hilo.
Unakataa kwa mkono wa kulia na kukubali kwa mkoni wa kushoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio maana kisheria haki za wananchi zinazolindwa na katiba zina 'limitations'. Kwa mfano haki ya mwananchi yeyote yule kujieleza, yaani freedom of speech/expression, huvuka mipaka na kuwa kitu haramu kisheria pale ambapo haki hiyo inapotumika kuingilia au kuvuruga haki zozote zile za mwananchi mwingine.
 
I never understood why most African schools insist on girls shaving their hair...It always sounded colonial to me...What has braided/permed/ blowed out hair got to do with education? I personally don’t like dreads but if someone wants to rock them cool...
 
Itakua alienda local schools ndiyo maana...

Ila international school hata ukiwa na boxer tupu sawa tuu...


Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom