Wauguzi 9 kufikishwa mahakamani Mafinga

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
739
484
Wauguzi 9 kufikishwa mahakamani Mafinga

Tuesday , 9th Feb , 2016
Halmashauri ya mji wa Mafinga imepanga kuwafikisha mahakamani watumishi 9 wa hospitali ya wilaya ya Mufindi wanaodaiwa kufanya uzembe kazini na kusababisha vifo vya baadhi ya wajawazito wanaofika kujifungua katika hospitali hiyo.

Katibu.JPG

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mafinga,Shaibu Nnunduma

Akitoa taarifa hiyo ya maandalizi ya kuwafikisha mahakamani watumishi hao mahakamani akiwemo mganga mkuu mfawidhi wa hospitali hiyo kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya mji wa Mafinga mkurugenzi wa halmashauri hiyo Shaib Nnunduma amesema kwa sasa uongozi wa halmashauri hiyi unakamilisha taratibu za kisheria ili kuwafikisha watumishi hao mahakamani kutokana na uzembe kazini.

Hivi karibuni kuliripotiwa taarifa za mama mmoja aliyetajwa kwa jina la Sauda Muyinga alifika hospitalini hapo kujifungua lakini kutokana na uzembe uliofanywa na wahudumu wa hospitali hiyo mama huyo hakupata huduma hadi alipofariki Januari 11 bila kupata huduma ya upasuaji baada ya kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida

Akifungua kikao hicho mkuu wa wilaya ya Mufindi Jowika Kasunga amezitaka halmashauri za wilaya ya Mufindi na halmashauri mpya ya mji wa mafinga kushirikiana katika kutoa huduma kwa wananchi ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wake.

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Mafinga Charles Makoga, amesema kuwa halmashauri hiyo haitawavumilia watendaji wanaojihusisha na siasa badala ya kushughulika na masuala ya utendaji.

Chanzo: EATV
 
Back
Top Bottom