Watumishi wa umma tumemkosea nini Rais Magufuli?

Roho mbaya na chuki havileti maendeleo najua wewe una enjoy na kodi zetu na unatumia unavotaka. Kwa unawaonea wafanyakazi tena wengine mishahara yao midogo sana haikidhi hata mihataji bado wewe unaongeza makato ya 15% kweli ujue mungu anakuona
 
Makato hayo yakiongezeka kutoka 8% kuwa 15%, tayari mtumishi ana makato mingine.
MFANO MTUMISHI MWENYE TGHSD

Basic Salary = 1215000
Net pay amount (kiasi anacholipwa baada ya makato yote) = 356859

MAKATO KAMA IFUATAVYO

1. Income tax (PAYE) 17.89...%=217440
2.HELB (Mkopo wa elimu) 15%=182250
3.NMB (Mkopo sijui wa nini) 27.73...%=336951
4.LAPF (Mfuko wa hifadhi ya jamii) 5%=60,750
5.NHIF (bima ya afya) 3%=36450
6.TAWGU (chama cha wafanyakazi) 2%=24300
JUMLA YA MAKATO = Tsh 858,141/=
hata hiyo laki tatu inatosha kuna watu wanalipwa laki na nusu na maisha yanaenda na wana familia punguzeni anasa
 
Safi sana mh Rais

Nyie watumishi wa umma mlikuwa na viburi sana awamu iliyopita

Hebu fikiria mimi nilienda moja ya ofisi,tulikuwa tumepanga foleni lakini cha ajabu yule mtumishi alituambia tusimsumbue akaingia ndani na kujifungia sijui alikuwa anachati huku siye tukiwa hatuna la kufanya tena asubuhi saa tatu-nne akina mama wapo kwenye foleni wameacha shughuli zao lakini wanajibiwa kidharau halafu huyo mtumishi anajifungia mlango.

Magufuli big up ..washikishe adabu hawa watumishi walikuwa wajeuri sana awamu iliyopita
hvi unajielewa kweli ww! kama walikuwa na viburi awamu iliyopita chuki na serikali ya SSM zilianzia wapi??
watumishi wa umma wameishi vizuri kipindi cha mkapa tu
 
Sidhani kama hii ID inakufaa. Mtu analamikia kukukatwa 15% ya mshahara. Wewe wataka akachukue mkopo benki wenye riba kubwa zaidi ili alipe deni kwa mkupuo!!! Ushauri wa hovyo kabisa.

Dawa ya deni ni kulipa. Siku zote kukopa ni harusi kulipa mkopo ni matanga.

Ushauri wangu kwako na wenzako: kachukue mkopo mwingine benki ya biashara, halafu kalipe mkopo wote uliosomea kwa mkupuo mmoja na kubaki na kiasi ambacho utakizalisha kwa kufanya ujasiriamali baada ya saa zako za kazi ya serikali. Utaweza rejesha mkopo wa benki bila matatizo kwa faida utakayopata kwenye huo ujasiria mali. Dhamana ya mkopo benki ni hiyo salary slip yako ya serikali.

Hivyo acha kulalama. Shukuru serikali imekusomesha na imekupa kazi serikalini. Sasa chapa kazi, rudisha mkopo hata kwa mkupuo mmoja ili na vijana wengine waweze nao kupatiwa mkopo wa masomo. Acha kulalama, tumia Akili yako kujipanga. Kumbuka bila huo mkopo hungalisoma maana wazazi wako ni maskini. Shukuru serikali inayoongozwa na ccm kwani hungefika hapo ulipo. Hungeweza hata kupata hiyo laki 5 kwa mwezi unayopokea baada ya makato ya deni la masomo. Sana sana ungekuwa unapata elfu 30 kwa mwezi kwa kufanya kazi za unachinga.

Acha kabisa kukufuru. Hizo laki 5 unazopata kila mwezi uwe unapeleka angalao laki 1 kwa wazazi wako masikini huko kijijini kwenu ili nao waondokane na umaskini. Acha kutumia hela hiyo kwa anasa. Lengo kuu la mikopo hiyo ni kuondoa umasikini kwenye familia masikini za Watanzania kwa kuwasomeshea watoto wao ili waje waondoe umasikini kwenye hizo familia. Halafu hayo makato si indefinate, ni ya muda mchache tu.
 
Safi sana mh Rais

Nyie watumishi wa umma mlikuwa na viburi sana awamu iliyopita

Hebu fikiria mimi nilienda moja ya ofisi,tulikuwa tumepanga foleni lakini cha ajabu yule mtumishi alituambia tusimsumbue akaingia ndani na kujifungia sijui alikuwa anachati huku siye tukiwa hatuna la kufanya tena asubuhi saa tatu-nne akina mama wapo kwenye foleni wameacha shughuli zao lakini wanajibiwa kidharau halafu huyo mtumishi anajifungia mlango.

Magufuli big up ..washikishe adabu hawa watumishi walikuwa wajeuri sana awamu iliyopita
Kibaya zaid hata hata wale wawakilishi wetu wametusahau! Wanachokumbuka kuwasaidia bongo movie
 
Mkuu mbona unapata shida sana kumwelewa mkulu?

Yeye alisema mapema kabla hata hajaukwaa,

Nanukuu

"..nitakuwa rais wa wanyonge na masikini.. "

"...nataka muishi kama mashetani.. "
Hao wanyonge mwenyewe wana lipi la kujivunia zaidi ya kulia kwa ugumu wa maisha sasa
 
Unajua kuna vitu ktk maisha lazima ujiulize. Tangu rais achukue ofisi ya inchi ana hasira na wafanyakazi. Je tutamwelewaje wakati kuna vitu ni vya kawaida ktk utumishi wa umma mfano stahiki za watumishi ni jambo la msingi sana kuliko kitu kingine mana ndo matumaini yao. Lakini mkuu wa nchi anaona hakuna haja ya kuwapa.

Pili alizingua akijitetea na uhakiki wa watumishi hewa wakasubiri wakavumilia lakini inaonekakana habari hiyo imekuwa story ya zamani

Tatu ikaja ya uhakiki wa vyeti bado watumishi wakaona isiwe tabu lakini habari mwisho wake sijajua imefikia wapi lakini inaonekana imemshinda mana wakubwa wote ni magumashi.

Kubwa ni la mwezi huu wa pili kukata 15% kwa ajili ya wanufaika wa bodi ya mkopo. Hatukatai kulipa deni shida ni kwa nini iwe 15% badala 8%? Hapo ndipo tatizo lilipo lazima watu wajue kwa wazalendo hatukatai kulipa deni la mkopo. Kwanini anatukomoa watumishi? Na kama anataka tanzania ya viwanda na yenye neema ataipata kwa namna hii?

Wakati tunaomba mkopo makubaliano ilikuwa nikipata kazi nikatwe 8% kwa nin aongeze mpaka 15%? kwa hiyo unaona hasira yake kwa watumishi tunajiuliza tumemkosea nini?

Mwisho nchi inajengwa na watumishi wenye ari ya kufanya kazi kwa uwezo wao wote, akili yao yote, na nguvu zao zote. Sikitiko kubwa ni kwamba Rais ana hasira na watumishi wa umma tunajiuliza je malengo yake atafanikiwa kwa kuwa na watumishi ambao hawana raha na furaha moyoni mwao.

Hii post ni kwa wazalendo kweli kweli future ya tanzania imo katika kuhamasishana kupeana moyo, na kifatijiana huku tukikusanya nguvu zetu kwa ajili ya taifa.

Karibuni wadau
Mkuu alishasema anataka muishi kama mashetani,ina maana wewe haukuelewa?
 
Dawa ya deni ni kulipa. Siku zote kukopa ni harusi kulipa mkopo ni matanga.

Ushauri wangu kwako na wenzako: kachukue mkopo mwingine benki ya biashara, halafu kalipe mkopo wote uliosomea kwa mkupuo mmoja na kubaki na kiasi ambacho utakizalisha kwa kufanya ujasiriamali baada ya saa zako za kazi ya serikali. Utaweza rejesha mkopo wa benki bila matatizo kwa faida utakayopata kwenye huo ujasiria mali. Dhamana ya mkopo benki ni hiyo salary slip yako ya serikali.

Hivyo acha kulalama. Shukuru serikali imekusomesha na imekupa kazi serikalini. Sasa chapa kazi, rudisha mkopo hata kwa mkupuo mmoja ili na vijana wengine waweze nao kupatiwa mkopo wa masomo. Acha kulalama, tumia Akili yako kujipanga. Kumbuka bila huo mkopo hungalisoma maana wazazi wako ni maskini. Shukuru serikali inayoongozwa na ccm kwani hungefika hapo ulipo. Hungeweza hata kupata hiyo laki 5 kwa mwezi unayopokea baada ya makato ya deni la masomo. Sana sana ungekuwa unapata elfu 30 kwa mwezi kwa kufanya kazi za unachinga.

Acha kabisa kukufuru. Hizo laki 5 unazopata kila mwezi uwe unapeleka angalao laki 1 kwa wazazi wako masikini huko kijijini kwenu ili nao waondokane na umaskini. Acha kutumia hela hiyo kwa anasa. Lengo kuu la mikopo hiyo ni kuondoa umasikini kwenye familia masikini za Watanzania kwa kuwasomeshea watoto wao ili waje waondoe umasikini kwenye hizo familia. Halafu hayo makato si indefinate, ni ya muda mchache tu.
ungeelewa alicho kiandika usinge jisumbua kuandika haya yote. Ni hivi katika mambo mengi anayo lalamikia mleta mada hili la mkopo (ambalo hujamwelewa) anasema hakatai kulipa bali anapinga kulipa kinyume na makubaliano aliyo ingia wakati anakopa.
 
Naamini watumishi wa umma wakipewa stahiki zao, tutafanikiwa :-

1. Kupunguza wizi ktk mkutadha wa rasilimali na muda

2. Rushwa

3. Kuboresha huduma kwa umma.

4. Kuinua ari ya kufanya kazi

5. Kukuza uzalendo

6. Kuondoa matabaka ya watawala na watumishi
 
In any standard 15% kwa elimu uliyopata bado ni ndogo sana ukitilia maanani kwamba unalipa value added tax ya 18% kwa bidhaa ambazo unanunua kila siku? Lipa tu ulitaka nani akulipie? Kama yamekushinda kopa bank urudishe mkopo mzima hakuna atakayekufuatafuata, kusoma usome wewe then unataka Watanzania masikini wa vijijini wakulipie kwa dezo. Grow up! Kila mtu atachukua msalaba wake mwenyewe. Watu mlizoea vya bure then mnataka nchi iendelee, mnafikiri nchi zilizoendelea waliendelea kwa kudekeza mizoga? Ati nikuonee wivu ili iwe nini? Mimi nikuonee wivu wewe unayelialia kulipia elimu yako? Shame on you!
shida ya watu wenye elimu za kuunga unga,hamna nayekataa kulipa mkopo shida ni taratibu zilizotumika.Watumishi wa umma kila mwaka wa fedha huwa wanapewa increment kwenye mshahara wake hii sio ni kwa sababu serikali inapenda ni increment ya kufidia gharama za maisha ikwemo infalation.kiuchumi huwezi kukaa mwaka moja kusiwe na mabadiliko ya kiuchumi,sasa serikali haijatoa hiyo increment alafu bado unamuongeze mtumishi makato.
Jambo la pili,hata kama kungekuwa na hizo increment za kila mwaka wa fedha ni lazima utoe official statement angalau miezi 2 au 3 kabla ili watu waji twist kimatumizi sasa hamna official statement wala sio kutoka kwa Mkurugenzi wa bodi,wala waziri nini maana yake??
maana yake wanajua ikitolewa official statement ni rahisi kuishitaki serikali kwa kwenda tofauti na mkataba ndio maana wanafanya kimya kimya bila kutoa taarifa rasmi
 
Ulipokuwa unasoma ulikuwa unataka huo mkopo. Asilimia 15% ndio mapovu yote haya. Dawa ya deni ni kulipa na kulimaliza, hii mikopo wengi walikuwa wanapiga danadana. Wacheni longolongo, nchi haiendeshwi kwa mabua.
Tatizo hujasoma chuo kikuu hata, huo mkopo huujui wew na akili ndogo unadhani ni mkopo wa vicoba!!!.
 
Hiyo laki na nusu inategemea na kazi unayofanya.

Kama wewe mpiga deki wa lumumba hata buku 5 inakutosha..!
nyie watumishi mnafanya kazi gani ya maana ambayo wengine hawawezi kuifanya hiyo kazi unayofanya hata akipewa motto aliemaliza darasa la 7 anafanya vizuri Zaidi yako....achene kazi muone kama kutakuwa na effect yoyote!
 
lakini si alishinda.....ushindi ni ushindi hata wa kura moja nao ni ushindi tu watumishi msijidanganye hamna effect yoyote kwenye uchaguzi
Hakika alishinda, lakini haikuwa kwa kishindo kama mwanzo, ninahisi haikuishia pale aliyefuata zikapungua zaidi ikiwa hali hii ikaendelea zaidi anaweza akashinda kwa asilimia 41(kwa kuwa ana tume na jeshi).
 
Back
Top Bottom