Watumishi wa umma tumemkosea nini Rais Magufuli?

Dah!!!acha ni pite kwa mama Jerome nikapate angalau ka kisado kimoja cha mbege ntarudi baadae humu maana namba ninaziona kwa mbali sana.
 
Wanapokea zaidi ya laki 5 kwa mwezi hawa vijana baada ya hayo makato kutegemea na fani waliosomea na kazi walizoajiriwa serikalini. Kwa mfano madaktari ni zaidi ya million moja na nusu - starting salary. Tatizo la vijana wa siku hizi wanataka baada ya mwaka mmoja tu wa kuajiriwa wawe wanamiliki gari na wawe wamejenga nyumba na anasa kibao. Ni vijana wa fastjet hivyo akikatwa hiyo 15% anaona inamharibia anasa zake.

Maisha hayaendi hivyo. Enzi za Mwalimu despite kuwa elimu ilikuwa bure, kijana alikuwa akiajiriwa serikalini baada ya masomo yake ya chuo kikuu alikuwa akipokea only 25% ya mshahara wake kwa muda wa miaka miwii, hiyo nyingine ilikuwa ni makato ya jeshi la kujenga taifa(JKT). Yaani miaka miwili ya kwanzaa baada ya masomo alihesabika yuko JKT na kazini alivaa uniform ya JKT. Alipelekwa na kukaa kwanza JKT kwa miezi 3, na miezi 21 aliyoyobaki aliendelea na ajira yake akiwa kwenye combat na akipokea only 25% of his salary!!!
Makubariano ni aslimia 8% sasa hiyo 15% imetoka wapi?
 
Mkuu mbona unapata shida sana kumwelewa mkulu?

Yeye alisema mapema kabla hata hajaukwaa,

Nanukuu

"..nitakuwa rais wa wanyonge na masikini.. "

"...nataka muishi kama mashetani.. "
Jambo la kustaajabisha katika hao wanyonge walimu hawamo, nani asiyejua hali ngumu ya maisha ya walimu wa nchi hii? Lakini nao pia wanasomeshwa namba kwa spidi ya ajabu, wamepandishwa madaraja lakini wameishia kumiliki barua za mishahara mipya bila mabadiliko kwenye akaunti zao na sasa ni zaidi ya mwaka, pili, hakuna uhamisho tokea uhamisho tangu zoezi la uhakiki wa watumishi liaze, ikumbukwe uhamisho huo ni wa Kubadilishana hivyo IKAMA isingekuwa tatizo kwa pande zote, Tatizo nilionalo Mimi ni kukosekana kwa moral obligation kwa kiongozi wetu, haumizwi na hali mbaya ya maisha ya watumiahi (wananchi wake).
 
Ulipokuwa unasoma ulikuwa unataka huo mkopo. Asilimia 15% ndio mapovu yote haya. Dawa ya deni ni kulipa na kulimaliza, hii mikopo wengi walikuwa wanapiga danadana. Wacheni longolongo, nchi haiendeshwi kwa mabua.
Kazi kweli kweli, watu hawajakataa kulipa deni ndugu, wanacholalamika ni kwamba mkataba wa kukatwa asilimia 7 au nane umevunjwa. No wonder utawala wa sheria umetupwa shimoni kila upande
 
hivi sijui ni akili za wapi,JPM anadhani unaweza kulitatua tatizo kwa kulikimbia tatizo.kwa kweli kati ya watu wanaojitambu nchi hii angalau kidogo ni watumishi maana wao wana uelewa wa mambo kidogo,watumishi wengi walikuwa hawa support SSM moja ya sababu ni serikali kutozingatia masilahi ya watumishi na kwa kweli kwenye uchaguzi Mkuu wengi walikuwa kwenye upande wa pili wa shiling.
sasa huwezi bado kuwa unawakomoa eti kwa kuwa walikuwa upande mwingine,kitu ambacho SSM ijue ni kuwa waumishi hawa nao wana wategemezi ambao ni ndugu,watoto,jamaa na marafiki hawa watu ni kundi kubwa kama wote watawishiwa na mtumishi amabo wana mtegemea ni dhahili hali itakuwa mbaya upande wa SSM.
kitu ambacho serikali ya SSM ishukuru ni kuwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi ni corrupt hivyo hiyo inakuwa advantage kwao,tofauti na hivyo vyama vya wafanyakazi huwa si vya kufanyia mchezo vinaweza angusha serikali
 
unadhani mtu anayepokea laki moja kwa mwezi alikopa kujenga nyumba yake na huku ana familia atafanyanya kazi kwa ufanisi kweli umetoa utetezi mzuri ila ujue kazi onaendana na moyo wa mtu kuwa furaha kwanza hujampa stahiki zake atakuwaje na hamasa ya yakazi?
acha kazi kama unaona mshahara mdogo
 
Dawa ya deni ni kulipa. Siku zote kukopa ni harusi kulipa mkopo ni matanga.

Ushauri wangu kwako na wenzako: kachukue mkopo mwingine benki ya biashara, halafu kalipe mkopo wote uliosomea kwa mkupuo mmoja na kubaki na kiasi ambacho utakizalisha kwa kufanya ujasiriamali baada ya saa zako za kazi ya serikali. Utaweza rejesha mkopo wa benki bila matatizo kwa faida utakayopata kwenye huo ujasiria mali. Dhamana ya mkopo benki ni hiyo salary slip yako ya serikali.

Hivyo acha kulalama. Shukuru serikali imekusomesha na imekupa kazi serikalini. Sasa chapa kazi, rudisha mkopo hata kwa mkupuo mmoja ili na vijana wengine waweze nao kupatiwa mkopo wa masomo. Acha kulalama, tumia Akili yako kujipanga. Kumbuka bila huo mkopo hungalisoma maana wazazi wako ni maskini. Shukuru serikali inayoongozwa na ccm kwani hungefika hapo ulipo. Hungeweza hata kupata hiyo laki 5 kwa mwezi unayopokea baada ya makato ya deni la masomo. Sana sana ungekuwa unapata elfu 30 kwa mwezi kwa kufanya kazi za unachinga.

Acha kabisa kukufuru. Hizo laki 5 unazopata kila mwezi uwe unapeleka angalao laki 1 kwa wazazi wako masikini huko kijijini kwenu ili nao waondokane na umaskini. Acha kutumia hela hiyo kwa anasa. Lengo kuu la mikopo hiyo ni kuondoa umasikini kwenye familia masikini za Watanzania kwa kuwasomeshea watoto wao ili waje waondoe umasikini kwenye hizo familia. Halafu hayo makato si indefinate, ni ya muda mchache tu.
Hakika dawa ya deni ni kulipa sikatai,

Tufundishe na msemo mwingine basi juu ya hili la watu kupandishwa madaraja na kuishia kumiliki barua tu kwa zaidi ya mwaka sasa
 
hivi sijui ni akili za wapi,JPM anadhani unaweza kulitatua tatizo kwa kulikimbia tatizo.kwa kweli kati ya watu wanaojitambu nchi hii angalau kidogo ni watumishi maana wao wana uelewa wa mambo kidogo,watumishi wengi walikuwa hawa support SSM moja ya sababu ni serikali kutozingatia masilahi ya watumishi na kwa kweli kwenye uchaguzi Mkuu wengi walikuwa kwenye upande wa pili wa shiling.
sasa huwezi bado kuwa unawakomoa eti kwa kuwa walikuwa upande mwingine,kitu ambacho SSM ijue ni kuwa waumishi hawa nao wana wategemezi ambao ni ndugu,watoto,jamaa na marafiki hawa watu ni kundi kubwa kama wote watawishiwa na mtumishi amabo wana mtegemea ni dhahili hali itakuwa mbaya upande wa SSM.
kitu ambacho serikali ya SSM ishukuru ni kuwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi ni corrupt hivyo hiyo inakuwa advantage kwao,tofauti na hivyo vyama vya wafanyakazi huwa si vya kufanyia mchezo vinaweza angusha serikali
watumishi hawazidi laki tano wakati watanzania ni Zaidi ya milioni 50.....hamna effect yoyote kwenye uchaguzi wa viongozi bora make kimya tu
 
Kwani hiyo 15% mnakatwa watumishi wa umma tu!?, hata wafanyakazi wa mashirika binafsi nao wanakatwa. Kwahiyo sote tunaisoma namba.
Umeona eeeh,ht sisi huku tunasomeshwa namba kisawa sawa tu. Ndio kwanza tumemaliza kuzisoma kwa kiswahili tumeanza za kirumi.
 
Lazima uone mantiki katika mada husika!
Uzito wa madeni katika mshahara hupimwa kwa asilimia za makato.
mfano. Kama nakopa 1,000,000/- na makato yake ni asilimia 8 ya mshahara wangu wa laki 1 (100,000/-) ina maana nitakuwa napungukiwa 8,000 kila mwezi hivyo bajeti yangu naipanga ktk sh. 92,000/- ukija ghafla kukata asilimia 15% maana yake utakata 15,000/- na mimi sasa nita operate katika Sh. 85,000/- umenipunguzia elfu 7 Zaidi katika mipango yangu.
Issue yako ya dawa ya deni kulipwa haina mantiki hapo, kwa kuwa tofauti ya rate hizo mbili ni muda tu utakaotumika kulipa deni, lkn hakuna dalili zozote za kukataa kulipa deni.
Issue ya msingi Zaidi ni kukunyima sifa au kukuongezea mzingo ktk ceiling ya mikopo
mtumishi haruhusiwi kuwa na makato ya Zaidi ya 30% ya mshahara wake, kwa maana hiyo nusu ya uwezo wako wa kukopa inazuiwa na bodi ambapo ni kinyume na makubaliano ya awali, lkn mbaya Zaidi ni kwa yule ambaye jumla ya mikopo ilishamfikisha katika 30% je ongezeko hili la 7% si litamfanya muajiri avunje sheria kwa kumfanya mtumishi akatwe beyond 30% mark?
hela ya mkopo wa chuo mlikuwa mnafanyia anasa tena inatakiwa mkatwe 50% ya salary hata hiyo 15% ni ndogo mno
 
Siyo kweli. Kwanza hiyo 1/3 ya mshahara umeitoa wapi kwani 15% is not 1/3. Sawa hata kama ni 1/3 ukijumulisha na makato mengine hususani PAYE na NHIF (zote hazifiki 1/3) kama wewe kwa mfano ni daktari ambaye mshahara wake si chini ya 1.5 million hiyo 2/3 itakayobaki ni 1.0 million. Wachini kabisa kwenye fani zingine tunachosema hiyo 2/3 au take home income yake si chini ya laki 5. Sasa kwa nini benki ya biashara ikatae kumkopesha mtu ambaye inauhakuka home income yake ya uhakika is over 5 lakis per month? Zinakopesha hata wale ambao take home income zao ni chini ya hapo. Usitake kudanganya. Benki wanachoangalia cha mhimu ni uwezo wako wa kulipa hicho kiasi cha pesa unazotaka ukope. Halafu kuna tasisi nyingi tu zinazokopesha kama unataka. Na si lazima ukakope na kulipa deni lako la masomo kwa mkupuo. Ishi kwa bajeti hiyo ya take home income na wapelekee kiasi wazazi wako. Baada ya miaka 2 au 3 utakuwa umemaliza hilo deni.

Cha mhimu utakachokopa benki si uende ukanunulia gari la matanuzi au kujenga nyumba ya kuishi. Kaizalishe hiyo hela kwa kuiwekeza kwa ujasiriamali. Usiwe na haraka, gari, nyumba na kadhalika utakujaga kuyapata tu huko mbeleni, tena mazuri zaidi kama utajipanga vizuri. Rome was not built in one day. Karibu kila mtumiIshi wa serikali alianzia maisha kwenye nyumba au chumba cha kupanga na usafiri wa daladala kwa muda si chini ya 10 years kabla ya kupata nyumba na usafiri wake mwenyewe. Kwa nini wewe unataka immediately? Ndiyo maana mnafanya wizi na ufisadi. Lazima mfundishwe kuishi kulingana na kipato.
Makato hayo yakiongezeka kutoka 8% kuwa 15%, tayari mtumishi ana makato mingine.
MFANO MTUMISHI MWENYE TGHSD

Basic Salary = 1215000
Net pay amount (kiasi anacholipwa baada ya makato yote) = 356859

MAKATO KAMA IFUATAVYO

1. Income tax (PAYE) 17.89...%=217440
2.HELB (Mkopo wa elimu) 15%=182250
3.NMB (Mkopo sijui wa nini) 27.73...%=336951
4.LAPF (Mfuko wa hifadhi ya jamii) 5%=60,750
5.NHIF (bima ya afya) 3%=36450
6.TAWGU (chama cha wafanyakazi) 2%=24300
JUMLA YA MAKATO = Tsh 858,141/=
 
Tafadhali soma namba... 2015,2016,2017 endelea mpaka 2025 mtanyooka kwerikweri!!
 
Back
Top Bottom