Watumishi wa umma tumemkosea nini Rais Magufuli?

Dawa ya deni ni kulipa. Siku zote kukopa ni harusi kulipa mkopo ni matanga.

Ushauri wangu kwako na wenzako: kachukue mkopo mwingine benki ya biashara, halafu kalipe mkopo wote uliosomea kwa mkupuo mmoja na kubaki na kiasi ambacho utakizalisha kwa kufanya ujasiriamali baada ya saa zako za kazi ya serikali. Utaweza rejesha mkopo wa benki bila matatizo kwa faida utakayopata kwenye huo ujasiria mali. Dhamana ya mkopo benki ni hiyo salary slip yako ya serikali.

Hivyo acha kulalama. Shukuru serikali imekusomesha na imekupa kazi serikalini. Sasa chapa kazi, rudisha mkopo hata kwa mkupuo mmoja ili na vijana wengine waweze nao kupatiwa mkopo wa masomo. Acha kulalama, tumia Akili yako kujipanga. Kumbuka bila huo mkopo hungalisoma maana wazazi wako ni maskini. Shukuru serikali inayoongozwa na ccm kwani hungefika hapo ulipo. Hungeweza hata kupata hiyo laki 5 kwa mwezi unayopokea baada ya makato ya deni la masomo. Sana sana ungekuwa unapata elfu 30 kwa mwezi kwa kufanya kazi za unachinga.

Acha kabisa kukufuru. Hizo laki 5 unazopata kila mwezi uwe unapeleka angalao laki 1 kwa wazazi wako masikini huko kijijini kwenu ili nao waondokane na umaskini. Acha kutumia hela hiyo kwa anasa. Lengo kuu la mikopo hiyo ni kuondoa umasikini kwenye familia masikini za Watanzania kwa kuwasomeshea watoto wao ili waje waondoe umasikini kwenye hizo familia. Halafu hayo makato si indefinate, ni ya muda mchache tu.

Non Sense, vapour,
 
Unajua kuna vitu ktk maisha lazima ujiulize. Tangu rais achukue ofisi ya inchi ana hasira na wafanyakazi. Je tutamwelewaje wakati kuna vitu ni vya kawaida ktk utumishi wa umma mfano stahiki za watumishi ni jambo la msingi sana kuliko kitu kingine mana ndo matumaini yao. Lakini mkuu wa nchi anaona hakuna haja ya kuwapa.

Pili alizingua akijitetea na uhakiki wa watumishi hewa wakasubiri wakavumilia lakini inaonekakana habari hiyo imekuwa story ya zamani

Tatu ikaja ya uhakiki wa vyeti bado watumishi wakaona isiwe tabu lakini habari mwisho wake sijajua imefikia wapi lakini inaonekana imemshinda mana wakubwa wote ni magumashi.

Kubwa ni la mwezi huu wa pili kukata 15% kwa ajili ya wanufaika wa bodi ya mkopo. Hatukatai kulipa deni shida ni kwa nini iwe 15% badala 8%? Hapo ndipo tatizo lilipo lazima watu wajue kwa wazalendo hatukatai kulipa deni la mkopo. Kwanini anatukomoa watumishi? Na kama anataka tanzania ya viwanda na yenye neema ataipata kwa namna hii?

Wakati tunaomba mkopo makubaliano ilikuwa nikipata kazi nikatwe 8% kwa nin aongeze mpaka 15%? kwa hiyo unaona hasira yake kwa watumishi tunajiuliza tumemkosea nini?

Mwisho nchi inajengwa na watumishi wenye ari ya kufanya kazi kwa uwezo wao wote, akili yao yote, na nguvu zao zote. Sikitiko kubwa ni kwamba Rais ana hasira na watumishi wa umma tunajiuliza je malengo yake atafanikiwa kwa kuwa na watumishi ambao hawana raha na furaha moyoni mwao.

Hii post ni kwa wazalendo kweli kweli future ya tanzania imo katika kuhamasishana kupeana moyo, na kifatijiana huku tukikusanya nguvu zetu kwa ajili ya taifa.

Karibuni wadau
Anawaandalia maisha mema hapo baadae ikiwa ni pamoja na kuwatunzia pesa zenu kisiri mkijua amewapa wala msijali hamtapoteza kama ni aslimia 8 makubaliano basi zile 7 anawatunzia na atawafungulia kila mmoja acount yake ki siri bila nyie kujua mwishoni anakuja anawapa kwa ajiri ya maisha yenu ya uzeeni kwani amegundua huwa mnateseka sana.
 
kama huna cha kusema ungetulia zako kuliko masiara haya
 
Siyo kweli. Kwanza hiyo 1/3 ya mshahara umeitoa wapi kwani 15% is not 1/3. Sawa hata kama ni 1/3 ukijumulisha na makato mengine hususani PAYE na NHIF (zote hazifiki 1/3) kama wewe kwa mfano ni daktari ambaye mshahara wake si chini ya 1.5 million hiyo 2/3 itakayobaki ni 1.0 million. Wachini kabisa kwenye fani zingine tunachosema hiyo 2/3 au take home income yake si chini ya laki 5. Sasa kwa nini benki ya biashara ikatae kumkopesha mtu ambaye inauhakuka home income yake ya uhakika is over 5 lakis per month? Zinakopesha hata wale ambao take home income zao ni chini ya hapo. Usitake kudanganya. Benki wanachoangalia cha mhimu ni uwezo wako wa kulipa hicho kiasi cha pesa unazotaka ukope. Halafu kuna tasisi nyingi tu zinazokopesha kama unataka. Na si lazima ukakope na kulipa deni lako la masomo kwa mkupuo. Ishi kwa bajeti hiyo ya take home income na wapelekee kiasi wazazi wako. Baada ya miaka 2 au 3 utakuwa umemaliza hilo deni.

Cha mhimu utakachokopa benki si uende ukanunulia gari la matanuzi au kujenga nyumba ya kuishi. Kaizalishe hiyo hela kwa kuiwekeza kwa ujasiriamali. Usiwe na haraka, gari, nyumba na kadhalika utakujaga kuyapata tu huko mbeleni, tena mazuri zaidi kama utajipanga vizuri. Rome was not built in one day. Karibu kila mtumiIshi wa serikali alianzia maisha kwenye nyumba au chumba cha kupanga na usafiri wa daladala kwa muda si chini ya 10 years kabla ya kupata nyumba na usafiri wake mwenyewe. Kwa nini wewe unataka immediately? Ndiyo maana mnafanya wizi na ufisadi. Lazima mfundishwe kuishi kulingana na kipato.
Halafu wewe huna akili kabisa ndii maana hutumii akili katika kuchanganua mada. Suala ni mkataba uheshimiwe kati ya pande mbili. Mtumishi aliyekopeshwa na Serikali. Wewe pia unafikiria kwa njia inayoonyesha wivu na husda. Inaelekea bado utoto unakusumbua kwani usingeweza kuwaza tu watumishi waliopo kazini kwa sasa hata watoto wako au ndugu zako wanaweza kufanyiwa hivyo.
Umekurupuka tu na kujibu sijui kwa kutumia ubongo gani halafu unajiita Dr Akili. Shame upon you!!
 
Maasira gani as hapo kusema kweli imekuwa hasira,huwezi amini huyu mtu anawapenda sana ameona huwa mnateseka sana uzeeni.
anakupendaje mkuu kwanza hawap stahilki zao pili hakuna promotion huu mwaka wa pili kwa hiyo ndo upendo huo? huku anatujazia makodi wew bana kama unanufaika myamaza kimya usiongee jamaa mchi imemshinda
 
Halafu wewe huna akili kabisa ndii maana hutumii akili katika kuchanganua mada. Suala ni mkataba uheshimiwe kati ya pande mbili. Mtumishi aliyekopeshwa na Serikali. Wewe pia unafikiria kwa njia inayoonyesha wivu na husda. Inaelekea bado utoto unakusumbua kwani usingeweza kuwaza tu watumishi waliopo kazini kwa sasa hata watoto wako au ndugu zako wanaweza kufanyiwa hivyo.
Umekurupuka tu na kujibu sijui kwa kutumia ubongo gani halafu unajiita Dr Akili. Shame upon you!!
hilo la mkataba ndo tatizo na ndo uonevu wenyew maccm siku zote hawatumii akili kwa mawazo unategea tutaendelea? tena usikute ni mtu mkubwa serikalin na anampa mkuu ushairi huo. ni shida sana
 
anakupendaje mkuu kwanza hawap stahilki zao pili hakuna promotion huu mwaka wa pili kwa hiyo ndo upendo huo? huku anatujazia makodi wew bana kama unanufaika myamaza kimya usiongee jamaa mchi imemshinda
Wakat mnamchagua mlikuwa hamjui hayo ni lini mfanyakazi amekuwa na maisha bora kwa utawala huu wa ccm? Nyinyi mmekuwa tatizo kubwa sana Neil mnaotumika kuona kura na kuwapa hawa ambao mnawaraum leo mmekuwa wakifa kura wazuri sana kwa chama hiki kifupi mmevuna mlichopanda tena kwakuwa mnakipenda sana chama hiki ni bora mngetumikia bure kwa miaka hata 6 ndo mkaanza kulipwa mishahara na kukatwa aslimia 20 ili mapenzi yenu yatimizwe kwa chama mnalalamika nn tena nyinyi ni tatizo kubwa sana wasaliti wakubwa nyie.
 
Ulipokuwa unasoma ulikuwa unataka huo mkopo. Asilimia 15% ndio mapovu yote haya. Dawa ya deni ni kulipa na kulimaliza, hii mikopo wengi walikuwa wanapiga danadana. Wacheni longolongo, nchi haiendeshwi kwa mabua.
Mkuu mbona unaonekana kama unaishi nchi nyingine au hukupewaga mkopo? Huwezi Saini mkopo wa riba ya 8℅ alafu in BTN unaambiwa ulipe 15% this is too much. Kumbuka sio kila MTU alikuwa halipi mkopo na hatakama ingekuwa hivyo je ni uzembe wa Nani katika kufatilia wanufaika wa mkopo? Mbona mabenki yanaweza kufuatilia! Watu walijaza taarifa zao kwenye form za kuomba mkopo kwanini wasiwatafute wasio rejesha? Kwanini bodi haiwasiliani na mteja wake mpaka kuwe na defaults? Think twice before comment a general comment
 
Ulipokuwa unasoma ulikuwa unataka huo mkopo. Asilimia 15% ndio mapovu yote haya. Dawa ya deni ni kulipa na kulimaliza, hii mikopo wengi walikuwa wanapiga danadana. Wacheni longolongo, nchi haiendeshwi kwa mabua.
Lazima uone mantiki katika mada husika!
Uzito wa madeni katika mshahara hupimwa kwa asilimia za makato.
mfano. Kama nakopa 1,000,000/- na makato yake ni asilimia 8 ya mshahara wangu wa laki 1 (100,000/-) ina maana nitakuwa napungukiwa 8,000 kila mwezi hivyo bajeti yangu naipanga ktk sh. 92,000/- ukija ghafla kukata asilimia 15% maana yake utakata 15,000/- na mimi sasa nita operate katika Sh. 85,000/- umenipunguzia elfu 7 Zaidi katika mipango yangu.
Issue yako ya dawa ya deni kulipwa haina mantiki hapo, kwa kuwa tofauti ya rate hizo mbili ni muda tu utakaotumika kulipa deni, lkn hakuna dalili zozote za kukataa kulipa deni.
Issue ya msingi Zaidi ni kukunyima sifa au kukuongezea mzingo ktk ceiling ya mikopo
mtumishi haruhusiwi kuwa na makato ya Zaidi ya 30% ya mshahara wake, kwa maana hiyo nusu ya uwezo wako wa kukopa inazuiwa na bodi ambapo ni kinyume na makubaliano ya awali, lkn mbaya Zaidi ni kwa yule ambaye jumla ya mikopo ilishamfikisha katika 30% je ongezeko hili la 7% si litamfanya muajiri avunje sheria kwa kumfanya mtumishi akatwe beyond 30% mark?
 
Wanapokea zaidi ya laki 5 kwa mwezi hawa vijana baada ya hayo makato kutegemea na fani waliosomea na kazi walizoajiriwa serikalini. Kwa mfano madaktari ni zaidi ya million moja na nusu - starting salary. Tatizo la vijana wa siku hizi wanataka baada ya mwaka mmoja tu wa kuajiriwa wawe wanamiliki gari na wawe wamejenga nyumba na anasa kibao. Ni vijana wa fastjet hivyo akikatwa hiyo 15% anaona inamharibia anasa zake.

Maisha hayaendi hivyo. Enzi za Mwalimu despite kuwa elimu ilikuwa bure, kijana alikuwa akiajiriwa serikalini baada ya masomo yake ya chuo kikuu alikuwa akipokea only 25% ya mshahara wake kwa muda wa miaka miwii, hiyo nyingine ilikuwa ni makato ya jeshi la kujenga taifa(JKT). Yaani miaka miwili ya kwanzaa baada ya masomo alihesabika yuko JKT na kazini alivaa uniform ya JKT. Alipelekwa na kukaa kwanza JKT kwa miezi 3, na miezi 21 aliyoyobaki aliendelea na ajira yake akiwa kwenye combat na akipokea only 25% of his salary!!!
Mkuu jina lako ni the opposite of you.......Yani unaropoka tu unayoyawaza kichwani mwako...eti wanapokea zaidi ya laki 5 baada ya makato!

Then maisha ya sasa usiyafananishe na enzi za nyerere wewe em kuwa na akili
 
Siyo kweli. Kwanza hiyo 1/3 ya mshahara umeitoa wapi kwani 15% is not 1/3. Sawa hata kama ni 1/3 ukijumulisha na makato mengine hususani PAYE na NHIF (zote hazifiki 1/3) kama wewe kwa mfano ni daktari ambaye mshahara wake si chini ya 1.5 million hiyo 2/3 itakayobaki ni 1.0 million. Wachini kabisa kwenye fani zingine tunachosema hiyo 2/3 au take home income yake si chini ya laki 5. Sasa kwa nini benki ya biashara ikatae kumkopesha mtu ambaye inauhakuka home income yake ya uhakika is over 5 lakis per month? Zinakopesha hata wale ambao take home income zao ni chini ya hapo. Usitake kudanganya. Benki wanachoangalia cha mhimu ni uwezo wako wa kulipa hicho kiasi cha pesa unazotaka ukope. Halafu kuna tasisi nyingi tu zinazokopesha kama unataka. Na si lazima ukakope na kulipa deni lako la masomo kwa mkupuo. Ishi kwa bajeti hiyo ya take home income na wapelekee kiasi wazazi wako. Baada ya miaka 2 au 3 utakuwa umemaliza hilo deni.

Cha mhimu utakachokopa benki si uende ukanunulia gari la matanuzi au kujenga nyumba ya kuishi. Kaizalishe hiyo hela kwa kuiwekeza kwa ujasiriamali. Usiwe na haraka, gari, nyumba na kadhalika utakujaga kuyapata tu huko mbeleni, tena mazuri zaidi kama utajipanga vizuri. Rome was not built in one day. Karibu kila mtumiIshi wa serikali alianzia maisha kwenye nyumba au chumba cha kupanga na usafiri wa daladala kwa muda si chini ya 10 years kabla ya kupata nyumba na usafiri wake mwenyewe. Kwa nini wewe unataka immediately? Ndiyo maana mnafanya wizi na ufisadi. Lazima mfundishwe kuishi kulingana na kipato.
Unauzoefu na hili unalosema mkuu? Mtu mwingine anadaiwa zaid ya million 12 unasema anauwezo wa kulipa miaka miwil -mitatu kwa mchanganuo upi?kumbuka kuna watumish wengine (walonufaika na mkopo) take home n laki nne na nusu baada ya ongezeka la 15%
 
Siyo kweli. Kwanza hiyo 1/3 ya mshahara umeitoa wapi kwani 15% is not 1/3. Sawa hata kama ni 1/3 ukijumulisha na makato mengine hususani PAYE na NHIF (zote hazifiki 1/3) kama wewe kwa mfano ni daktari ambaye mshahara wake si chini ya 1.5 million hiyo 2/3 itakayobaki ni 1.0 million. Wachini kabisa kwenye fani zingine tunachosema hiyo 2/3 au take home income yake si chini ya laki 5. Sasa kwa nini benki ya biashara ikatae kumkopesha mtu ambaye inauhakuka home income yake ya uhakika is over 5 lakis per month? Zinakopesha hata wale ambao take home income zao ni chini ya hapo. Usitake kudanganya. Benki wanachoangalia cha mhimu ni uwezo wako wa kulipa hicho kiasi cha pesa unazotaka ukope. Halafu kuna tasisi nyingi tu zinazokopesha kama unataka. Na si lazima ukakope na kulipa deni lako la masomo kwa mkupuo. Ishi kwa bajeti hiyo ya take home income na wapelekee kiasi wazazi wako. Baada ya miaka 2 au 3 utakuwa umemaliza hilo deni.

Cha mhimu utakachokopa benki si uende ukanunulia gari la matanuzi au kujenga nyumba ya kuishi. Kaizalishe hiyo hela kwa kuiwekeza kwa ujasiriamali. Usiwe na haraka, gari, nyumba na kadhalika utakujaga kuyapata tu huko mbeleni, tena mazuri zaidi kama utajipanga vizuri. Rome was not built in one day. Karibu kila mtumiIshi wa serikali alianzia maisha kwenye nyumba au chumba cha kupanga na usafiri wa daladala kwa muda si chini ya 10 years kabla ya kupata nyumba na usafiri wake mwenyewe. Kwa nini wewe unataka immediately? Ndiyo maana mnafanya wizi na ufisadi. Lazima mfundishwe kuishi kulingana na kipato.
Umesoma mpaka darasa la ngapi na unafanya kazi wapi? Uelewa wako ktk jambo hili ni mdogo kama punje ya ulezi
 
Watumishi wa umma ndo walio haribu nchi hii kwahiyo rais lazima awanyooshe. Kila kiongozi anapoingia madarakani anakuwa na mentality yake ya nani adeal naye kufanikiwa.
Nyerere aliamua kudeal na wananchi wa kawaida akawahimiza walime, akahimiza wasome ili nchi iendelee.
Mwinyi akadeal na wafanyabiashara wafanye biashara kiuhuru ili watu wapate mahitaji yao kiurahisi, Mkapa yeye aldeal sana na wafahisani wa nje ali-communicate nao kila wakati ili kusaidia nchi walimpa ushauri na programs nyingi za donors zilionekana kipindi chake. Kikwete alideal sana na wanasiasa awamu yake hakuna kipindi ambacho wanasiasa walifaidi na kuumia zaidi ya awamu ya Kikwete. kipindi hicho siasa watu wengine imewanufaisha sana ila wengine siasa imewanyoosha.
Kipindi cha Magu ni kipindi cha kudeal na watumishi yeye ndo kaona mafanikio yatatokea hapo ktk utawala wake. Akiwanyoosha watumishi wa umma nchi itanyooka.
 
Back
Top Bottom