Watumishi wa umma tumemkosea nini Rais Magufuli?

2020 tutalipiza kisasi.
Kura za wafanyakazi tulishazitoa toka uchaguzi wa 2010
2010 TUKASHINDA bila kura za wafanyakazi wa UMMA
2015 TUKASHINDA bila kura za wafanyakazi wa UMMA
2020 TUTASHINDA bila kura za wafanyakazi wa UMMA
 
Rais ni Mwalimu kitaaluma ila ameacha kutoa ajira za walimu wakati anajua kabisa asilimia kubwa ya wanaosomea ualimu ni watoto wa masikini wanaotegemea kuajiriwa na serikali baada ya kumaliza mafunzo.

Unajua kuna vitu ktk maisha lazima ujiulize. Tangu rais achukue ofisi ya inchi ana hasira na wafanyakazi. Je tutamwelewaje wakati kuna vitu ni vya kawaida ktk utumishi wa umma mfano stahiki za watumishi ni jambo la msingi sana kuliko kitu kingine mana ndo matumaini yao. Lakini mkuu wa nchi anaona hakuna haja ya kuwapa.

Pili alizingua akijitetea na uhakiki wa watumishi hewa wakasubiri wakavumilia lakini inaonekakana habari hiyo imekuwa story ya zamani

Tatu ikaja ya uhakiki wa vyeti bado watumishi wakaona isiwe tabu lakini habari mwisho wake sijajua imefikia wapi lakini inaonekana imemshinda mana wakubwa wote ni magumashi.

Kubwa ni la mwezi huu wa pili kukata 15% kwa ajili ya wanufaika wa bodi ya mkopo. Hatukatai kulipa deni shida ni kwa nini iwe 15% badala 8%? Hapo ndipo tatizo lilipo lazima watu wajue kwa wazalendo hatukatai kulipa deni la mkopo. Kwanini anatukomoa watumishi? Na kama anataka tanzania ya viwanda na yenye neema ataipata kwa namna hii?

Wakati tunaomba mkopo makubaliano ilikuwa nikipata kazi nikatwe 8% kwa nin aongeze mpaka 15%? kwa hiyo unaona hasira yake kwa watumishi tunajiuliza tumemkosea nini?

Mwisho nchi inajengwa na watumishi wenye ari ya kufanya kazi kwa uwezo wao wote, akili yao yote, na nguvu zao zote. Sikitiko kubwa ni kwamba Rais ana hasira na watumishi wa umma tunajiuliza je malengo yake atafanikiwa kwa kuwa na watumishi ambao hawana raha na furaha moyoni mwao.

Hii post ni kwa wazalendo kweli kweli future ya tanzania imo katika kuhamasishana kupeana moyo, na kifatijiana huku tukikusanya nguvu zetu kwa ajili ya taifa.

Karibuni wadau
 
Wengi wa waliokopeshwa wapo mtaani hawana ajira.

Serikali haitengenezi mazingira ya kuongeza ajira.

Niache vipi uongo? hadi mnasakwa ili mlipe mikopo yenu, na wao wanataka pesa zao zirudi mapema kutokana na huo ujinga wa kukwepa kulipa madeni-wakati wa kukopa mnakuwa wapole sana, wakati wa kulipa mnajidai wajanja sana na kuwa na uchungu wa pesa.
 
hela ya mkopo wa chuo mlikuwa mnafanyia anasa tena inatakiwa mkatwe 50% ya salary hata hiyo 15% ni ndogo mno
sijui kama unajua matumizi sahihi ya neno anasa!
Boom la kiwango cha 2500 - 10,000/- kama Dar utafanya anasa gani kwa sh 10,000/ per day?
Hivi unajua kuwa accommodation pia ni sehemu hilo boom, mlo wa siku na kuna ambao walikuwa wanagawana na familia zao?

Hii nchi sasa hivi watu wenye mawazo ya kifukara wamezidi, sijui wametokea wapi?
 
Wanapokea zaidi ya laki 5 kwa mwezi hawa vijana baada ya hayo makato kutegemea na fani waliosomea na kazi walizoajiriwa serikalini. Kwa mfano madaktari ni zaidi ya million moja na nusu - starting salary. Tatizo la vijana wa siku hizi wanataka baada ya mwaka mmoja tu wa kuajiriwa wawe wanamiliki gari na wawe wamejenga nyumba na anasa kibao. Ni vijana wa fastjet hivyo akikatwa hiyo 15% anaona inamharibia anasa zake.

Maisha hayaendi hivyo. Enzi za Mwalimu despite kuwa elimu ilikuwa bure, kijana alikuwa akiajiriwa serikalini baada ya masomo yake ya chuo kikuu alikuwa akipokea only 25% ya mshahara wake kwa muda wa miaka miwii, hiyo nyingine ilikuwa ni makato ya jeshi la kujenga taifa(JKT). Yaani miaka miwili ya kwanzaa baada ya masomo alihesabika yuko JKT na kazini alivaa uniform ya JKT. Alipelekwa na kukaa kwanza JKT kwa miezi 3, na miezi 21 aliyoyobaki aliendelea na ajira yake akiwa kwenye combat na akipokea only 25% of his salary!!!
Nakuelewa sana mkuu tatizo la sisi vijana tulio wengi tunapenda sana maisha ya anasa unlimited. Ila pia ni haki yao wanaokumbwa na makato hayo kuambiwa yanatokana na nini tofauti na mkataba wao wa awali
 
nyie watumishi mnafanya kazi gani ya maana ambayo wengine hawawezi kuifanya hiyo kazi unayofanya hata akipewa motto aliemaliza darasa la 7 anafanya vizuri Zaidi yako....achene kazi muone kama kutakuwa na effect yoyote!
wew sio mzima unaumwa
 
Unajua kuna vitu ktk maisha lazima ujiulize. Tangu rais achukue ofisi ya inchi ana hasira na wafanyakazi. Je tutamwelewaje wakati kuna vitu ni vya kawaida ktk utumishi wa umma mfano stahiki za watumishi ni jambo la msingi sana kuliko kitu kingine mana ndo matumaini yao. Lakini mkuu wa nchi anaona hakuna haja ya kuwapa.

Pili alizingua akijitetea na uhakiki wa watumishi hewa wakasubiri wakavumilia lakini inaonekakana habari hiyo imekuwa story ya zamani

Tatu ikaja ya uhakiki wa vyeti bado watumishi wakaona isiwe tabu lakini habari mwisho wake sijajua imefikia wapi lakini inaonekana imemshinda mana wakubwa wote ni magumashi.

Kubwa ni la mwezi huu wa pili kukata 15% kwa ajili ya wanufaika wa bodi ya mkopo. Hatukatai kulipa deni shida ni kwa nini iwe 15% badala 8%? Hapo ndipo tatizo lilipo lazima watu wajue kwa wazalendo hatukatai kulipa deni la mkopo. Kwanini anatukomoa watumishi? Na kama anataka tanzania ya viwanda na yenye neema ataipata kwa namna hii?

Wakati tunaomba mkopo makubaliano ilikuwa nikipata kazi nikatwe 8% kwa nin aongeze mpaka 15%? kwa hiyo unaona hasira yake kwa watumishi tunajiuliza tumemkosea nini?

Mwisho nchi inajengwa na watumishi wenye ari ya kufanya kazi kwa uwezo wao wote, akili yao yote, na nguvu zao zote. Sikitiko kubwa ni kwamba Rais ana hasira na watumishi wa umma tunajiuliza je malengo yake atafanikiwa kwa kuwa na watumishi ambao hawana raha na furaha moyoni mwao.

Hii post ni kwa wazalendo kweli kweli future ya tanzania imo katika kuhamasishana kupeana moyo, na kifatijiana huku tukikusanya nguvu zetu kwa ajili ya taifa.

Karibuni wadau
KWELI UMESEMA MKUU, HAIWEZEKANI TU MARA MOJA NO EMPLOYMENT AND MAKATO YA MKOPO JUU. WHY ?.. INGAWA MIMI SIO MWAJIRIWA LAKINI NAONA WATUMISHI WAMEKATA TAMAA na WANAFUNZI VYUONI WAMEKATA TAMAA NA UNEMPLOYED PEOPLE WAMEKATA TAMAA .
Sasa mbona kujinadi kwa wananchi itakuwa ngumu sana?
 
tangu nimeanduka mada jana ccm mwenye akili ni wew waambie wenzako hapo juu serikali isiyo ajir, isiyowapa stahiki zao watumishi, serikali isijali raia wake wakati wa majanga kama bukoba ni serikali namna gani inatosha nitatukana bure nilupishwe m7
 
Kura za wafanyakazi tulishazitoa toka uchaguzi wa 2010
2010 TUKASHINDA bila kura za wafanyakazi wa UMMA
2015 TUKASHINDA bila kura za wafanyakazi wa UMMA
2020 TUTASHINDA bila kura za wafanyakazi wa UMMA
Wafanyakazi wa UMMA ni asilimia ndogo sana ya wapiga kura. There is no way wakaathiri matokeo
 
Dawa ya deni ni kulipa kanuni hiyo ianze kwa serikali ilipe madeni ya watumishi wake kwanza ili mfano huo uigwe kwa watumishi inawezekana hupendi kufikiri nje ya box lkn jaribu kuangalia uwiano huo jaribu pia kuangalia watumishi hawa wamekubali kuvumilia kusitishwa kwa nyongeza zote nk.na hoja hapa ni kulipa stahiki za watumishi wote ambazo zilikwisha pitishwa mf.Uhamisho,kulipwa kulingana na vyeo vyao nk.
Stahiki ya mtumishi wa umma ni mshahara wake tu. Hayo maposho mengine, sijui posho ya disturbance allowance, leave allowance, housing allowance, maternity allowance, electricity & telephone allowance etc etc siyo stahiki ya mtumishi bali ni previledges zinazotolewa na waziri wa utumishi kupitia standing orders ambazo anaweza kuzibadili au kuzifuta anytime.
 
ungeelewa alicho kiandika usinge jisumbua kuandika haya yote. Ni hivi katika mambo mengi anayo lalamikia mleta mada hili la mkopo (ambalo hujamwelewa) anasema hakatai kulipa bali anapinga kulipa kinyume na makubaliano aliyo ingia wakati anakopa.
Wengi walingia i kulipa hii mikopo baada ya kumaliza masomo yao na hivyo kusababisha gharama ya kuwasaka. Hivyo wao wenyewe walivunja huo mkataba uliowataka kuanza kulipa deni after 1 year ya kumaliza masomo bila kujari umepata ajira serikalini au la. Hivyo kuwakata 15% au zaidi ni halali yao.
 
Kwa hiyo ww akili zako na ufahamu wako na usomi wako kama ni msomi ilifikiria kiwanda ni kitu gani? ama kweli watz tulikuwa tumechoka sana kifikra-ulitegemea madude makubwa makubwa-ila kinachotengeza juice na mikate kwako si kiwanda.
Nasikitika kwa akili zako ufahamu wako na usomi wako umeshindwa kuelewa nn namaanisha..rudia kusoma comment yangu
 
Zama zimebadilika bhana, usituletee paukwa pakawa hapa, blaaa blaa tupu hauna haya.

Vaa magome ya miti au jinja basi na ukasubirie sukari kilo moja mwezi mzima kwenye duka la ushirika. Na hizo Enzi zako tupa kuleee ndo mana hatukukulia enzi hizo

Mawazo mgando kabisa . Na mfumuko wa bei ulikuwaje hizo enzi? Non sense. Usishindane na Wakati utaumbuka.
Sawa zana zimebadilika. Enzi zile kijana akipata degree moja (Bachelor degree) alionekana msomi kweli kweli. Alipata kazi kubwa serikalini na mshahara mnene. Na hata urais aliweza kupata. Maana hakukuwa na wasomi wengi.

Sasa hivi tumeendelea. Tumesomesha vijana wengi. Leo hii degree moja is nothing. Tunao kibao na ni wachache sana wanaweza pata ajira serikalini na wakiipata si yenye madaraka makubwa kama enzi zile. Wengi wako tu mitaani wakisaga lami au wako kwenye ajira binafsi. Kwa mfano sasa hivi tuna vijana wenye LLB (Bachelor of Laws) zaidi ya laki moja wako mitaani wakisaga lami. Tuna zaidi ya vijana 10,000 wenye degree ya kwanza ya medicine ( MD or MBCHB) wako mitaani wakisaga lami. Degree hizi enzi zile zilikuwa ni hot cakes.

Wewe unayejiita NUCLEAR BOMB inavyoelekea haya mambo huyafahamu. Nadhani wala si kati ya hao watumishi wa umma unaowatetea. Hata hako ka degree kamoja sidhani kama unako. Vijana waliomaliza masomo yao ya degree ya kwanza na wakabahatika kupata ajira serikalini kamwe hawatalalamika hako kamkato ka 15% cha mshahara wao kurejesha mkopo wa masomo yao. They are very happy. Wanaoweza kulalamika sana sana ni wale ambao bado wanasaga lami au wale walio kwenye ajira binafsi maana wote wanatakiwa kurudisha mkopo aidha wao wenyewe au hao waliowadhamini kupata huo mkopo.

Hata huko ulaya kijana aliyemaliza degree moja na kupata ajira hawezi kumiliki nyumba na gari ndani ya kipindi cha mwaka mmoja hadi 10. Never on earth. Sasa vijana wakitanzania wanataka iwe hivyo. Kwa hiyo inabidi wajiingize kwenye ubadhilifu na ufisadi wa mali za umma ili kutimiza ndoto yao. Kwani kwa kipato (mshahara) wanaopata hata kama hautakatwa hiyo 15% hauwawezeshi kupata vitu hivyo (gari na nyumba) ndani ya miaka kumi baada ya kupata ajira. Sasa wewe Nuclear Bomb sijui unaweweseka kipi hapa? We are talking of realities and you are bringing politics of oppositions. It is very childish behaviour.
 
Back
Top Bottom