Watumishi wa Umma njooni tukubaliane

Ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni,ni kweli Magufuli anafaa ila amekuja wakati mbaya,watu wanataka mabadiliko nje ya CCM,na kwa sasa UKAWA ndio mpango mzima.

MAGUFULI nimtendaji mzuri ila alipo kaa ndio pachafu yaani CCM.
LOWASSA ni mtendaji mbovu na hafai ila alipokaa ndio pasafi yaani CDM.
Wengi wanamchagua LOWASSA kwasababu ya cdm cuf na nccr lakini siyo kwa uzri wa kazi zake lowassa
MAGUFULI anasimama yeye kama yeye kwa uzuri na usimamizi wake mzuri wa kazi nasio chama chake
 
Mkuu umekuja na hoja yenye mashiko kwelikweli. Shida kubwa ni kuwa huyo anayetegemea kuleta mabadiliko ametoka hukohuko na kuna msemo kuwa jasiri haachi asili. Laiti tungepata mtu ambaye hatokani na system ikiyotufikisha hapa ningekuwa wa kwanza kuunga mkono hoja. Lakini huyu ni kati ya waliojenga hii system inayotudhulumu sisi watumishi wa umma. I wish angesimama hata Jussa au Mdee ningeelewa.
 
Hakuna deni la Mwl ambalo halija lipwa..

Una hakika au unanukuu kilichosemwa na wasemaji wa mazoea? Angalia sifa zisikuongoze kutenda dhambi. Walimu wana madai, tena mazito. Maneno yanayosemwa kwenye vyombo vya habari na uhalisia vinapishana maili 350 juu ya usawa wa bahari.

Nikukumbushe waziri wa kazi alitoaga agizo la siku 28 kuhusu jambo fulani kuhusu makampuni ya nje, kiko wapi? Kwa msingi huu ndio wananchi sasa wameamua kupeleka OIL CHAFU ikulu ikatuulie mchwa, pombe kunyweni nyinyi mlioshiba tayari
 
Nimepitia salary slip yangu kwa kweli tunahitaji Rais ambaye atatutetea watumishi wa umma. Kodi 94000 kila mwezi jamani huu uonevu utaisha lini. Hapo bado hujalipa kodi kupitia kununua umeme, kodi ya nyumba kweli watumishi wa umma tunadhulumiwa na hawa CCM.
 
tulikuwa na imani kubwa kupita mlima kilimanjaro wakati KIKWETE anaingia madarakani lakini alichokifanya ,IMANI hii haipo tena, hakuna ndani ya CCM ANAYEWEZA KULETA MABADILIKO hayo wanayoyaimba kwa takribani miaka 60
Tuna imani na Magufuli atashughulikia maswala hayo yote usijali mtumishi we mpe kura tuu yule mtendaji
 
Matumishi ya umma tumba.ff zetu, mara ngapi tumekuwa tukiwabeba ccm kwa kusaidia wizi wa kura? Wacha tupigike labda tutatia akili!
 
Lowassa atosha. Magufuli Pole sana,
na kwa taarifa , hata hapa jimboni kwa magufuli, Ubunge ni Ukawa.
 
Unachotaka kusema ni kuwa wizara ya magufuli wana schemes zao tofauti za mishahara tofauti na watumishi wengine wa umma?????

MAGUFULI katika wizara yake wafanyakazi wanalipwa mishahara mizuli na wanafanya kazi vizuri kwa mda mwafaka nakasema akiwa raisi atapandisha mishahara ila watu wafanye kazi haswa

Mmmmmmmmh
 
Walimu wanaidhalilisha sana utumishi wa umma.wanatoa taarifa za uongo ili kuiibia serikali.
ngoja nikupe darasa unaonekana hujui kitu.taarifa za madai ya walimu hutumwa na halmashauri kwenda wizarani kama List tu bila viambatanisho,hila linafanyika baada ya idara ya elimu halmashauri kuhakiki kwa kina kwa ushirikiano na CWT,hivyo kwa madai yasiyostahili hukataliwa kabla list haijaenda wizarani.Sasa hao waliosema madai ni famba wanapata wapi ujasiri huo wakati wanapokea list tu?kwa nini hawajarudisha taarifa halmashauri kujiridhisha kwa documents za maombi?walimu huu mwaka wenu chinja hawa c.c
Evelyn Salt,kamanda nifah
 
Last edited by a moderator:
Mimi sio mtumishi wa umma wala nini, ila kwa uchungu mkubwa nilionao juu ya u jobless wangu huu hakika nitaipa kura ya ndio Chadema kupitia UKAWA.
Sioni jipya katika serikali iliyochoka ya CCM.
 
Mimi sio mtumishi wa umma wala nini, ila kwa uchungu mkubwa nilionao juu ya u jobless wangu huu hakika nitaipa kura ya ndio Chadema kupitia UKAWA.
Sioni jipya katika serikali iliyochoka ya CCM.

Ndo maana kila saa upo mtandaoni
 
Back
Top Bottom