Watumiaji wa Telegram tumia bot hii kupata taarifa punde zinapotokea

IrDA

JF-Expert Member
Aug 26, 2010
743
350
Habari zenu wakuu,
Kwa wale watumaji wa mtandao wa Telegram mnafahamu kwamba ndani ya telegram kuna 'bots' ambazo zinaweza kufanya kazi mbalimbali kama; kukutumia habari mbalimbali, kuconvert mafile kutoka format moja kwenda nyingine,kusearch directly google, kudownload video za youtube,kucheza games kama tic-tac toe n.k

Nimetengeneza bot inayoitwa Habari motomoto. Bot hii inakupa taarifa kwa ufupi punde zinapotokea hasahasa Tanzania na duniani kwa ujumla.Habari za uhakika.

Habari hizi zinaingia kama message kwenye telegram, na unaweza ukaMute ukawa unasoma pale unapataka.

Source ya habari hizi ni millardayo.com ,bbcnews na Jamiiforums twitter updates

Kuijaribu bonyeza hapa; Habari_motomoto

Uzuri wake huitaji kudownload app nyingine yoyote zaidi ya kuwa na telegram kwenye simu yako au computer .Hivyo inapunguza kuwa na utitiri wa apps

Angalia hizo screenshots uone ilivyo;
photo_2017-10-23_12-15-01.jpg photo_2017-10-23_12-15-05.jpg photo_2017-10-23_12-15-10.jpg
 
bado halijakaa vizuri linarudiarudia tu kukaribisha
next time tengeneza from scratch izo platform za many bot na chatfuel huwa naona zinazingua
 
Back
Top Bottom