Watu wanazidi kujionea matunda ya ushirikiano wa kibiashara kati ya China na Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111350897178.jpg


Parachichi kutoka Kenya, korosho kutoka Tanzania, kahawa kutoka Ethiopia... katika miaka ya hivi karibuni, bidhaa bora zaidi za Afrika zinazidi kupendwa na wachina wa kawaida; huku barani Afrika, vijana wakiweza kununua bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa China kwenye jukwaa la biashara ya mtandaoni nyumbani kwao. Watu wa China na Afrika wamejionea matunda halisi ya ushirikiano wa kibiashara kati ya China na Afrika.

"Ni watu wa China na Afrika ndio wenye haki ya kusema kama ushirikiano kati ya China na Afrika ni mzuri au la." Katika Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika Beijing mwaka 2018, Rais Xi Jinping wa China alitangaza kuanzishwa kwa Maonyesho ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika kwa lengo la kujenga jukwaa kwa ajili ya pande mbili kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara. Baada ya awamu mbili za Maonyesho hayo kufanyika kwa mafanikio, maonyesho ya tatu ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika yatafunguliwa Alhamisi hii huko Changsha, Mkoa wa Hunan, chini ya kauli mbiu ya "kutafuta maendeleo kwa pamoja na kunufaika na mustakabali mzuri kwa pamoja". Nchi 53 za Afrika zenye uhusiano wa kibalozi na China na mashirika 8 ya kimataifa yatashiriki katika maonyesho hayo, na kuzidisha uhusiano wa kibiashara kati ya China na Afrika.

Katika miaka ya hivi karibuni, thamani ya biashara kati ya China na Afrika imezidi kuongezeka, na China imekuwa ikishika hadhi yake kama mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika. Katika mchakato huu, China imekuwa ikijitahidi kukuza uwiano wa maendeleo ya biashara kati ya China na Afrika, na kukaribisha Afrika kunufaika moja kwa moja na maendeleo ya China. Kilimo ni moja ya nguzo kuu za kiuchumi za nchi nyingi za Afrika, na kinachangia zaidi ya 30% katika Pato la Taifa, na 70% ya watu wanajishughulisha na sekta ya kilimo. Mwaka 2021, mradi wa kukuza biashara, ukiwa moja ya "Miradi Tisa" iliyotangazwa kwenye Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa FOCAC umedhihirisha kuwa China itaanzisha "njia ya kijani" kwa ajili ya mazao ya kilimo ya Afrika ya kuuzwa China, na zaidi kupanua bidhaa za Afrika zinazouzwa China bila ya kutozwa ushuru. Hadi sasa, aina 16 za mazao ya kilimo kutoka nchi 11 za Afrika zinasafirishwa nchini China kupitia "njia ya kijani", na nchi 21 za Afrika zimefurahia kutotozwa ushuru kwa 98% ya bidhaa zao zinazouzwa China. Katika Mkutano wa Kilele wa Beijing wa FOCAC wa mwaka 2018 na Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa FOCAC wa mwaka 2021, China pia iliweka mgao wa ufadhili wa dola za Marekani bilioni 5 na bilioni 10 mtawalia, ili kuunga mkono Afrika kuuza bidhaa zake nje. Kwa mujibu wa takwimu, China imekuwa nchi ya pili kwa soko kubwa la bidhaa za kilimo za Afrika.

Wakati huo huo, kufuatia kuongezeka kwa hamu za watu wa Afrika kuhusu teknolojia mpya katika enzi mpya, ushirikiano wa kibiashara kati ya China na Afrika unapanuka kutoka katika sekta za kawaida kama biashara ya jadi na uhandisi hadi kwenye nyanja zinazoibukia kama vile digitali na kijani. Makampuni ya China yanashiriki katika ujenzi wa miundombinu ya kidijitali barani Afrika, na kuzisaidia nchi za Afrika kujiunga na wimbi la digitali na kuondokana na pengo la kidigitali. Baada ya mwaka 2019, kampuni ya Afrika Kusini ya Rain ikawa kampuni ya kwanza ya mawasiliano ya simu barani Afrika kutumia 5G ya kampuni ya China ya Huawei, mwaka jana, kampuni nyingine mbili za simu nchini Afrika Kusini na Kenya mtawalia zilizindua mitandao ya 5G inayoendeshwa na Huawei. Nchi nyingi zaidi za Afrika zimetambua kwamba teknolojia na bidhaa zinazotolewa na kampuni za China zina ubora na za bei nafuu zaidi kuliko za kimagharibi. Katika miaka ya hivi karibuni, hali ya hewa kali kama vile joto kali, ukame, na mafuriko imetokea mara kwa mara, pamoja na athari za mzozo kati ya Russia na Ukraine, uzalishaji wa chakula barani Afrika unakabiliwa na changamoto kubwa. Jinsi ya kuongeza uzalishaji wa kilimo na kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi kwa njia endelevu zaidi ni suala la kawaida linalokabili China na Afrika. Siku hizi, China na Afrika zinaharakisha uvumbuzi wa teknolojia ya kijani na mageuzi kuhusu mbinu za uzalishaji, na kutoa ufumbuzi wa kilimo cha kisasa kinachoweza kuvumilia changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka kumi tangu Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja BRI kutangazwa. Ikiwa ni moja ya maeneo muhimu ambapo pendekezo hilo linatekelezwa, Afrika inajitahidi kufuata mwingiliano wa kiuchumi, ambao unaendana kikamilifu na moyo wa manufaa ya pande zote na lengo la kutafuta maendeleo ya pamoja yaliyomo katika Pendekezo la BRI. Kwa hiyo, China ikiwa nchi kubwa zaidi inayoendelea na Afrika likiwa bara lenye nchi nyingi zinazoendelea, zinapaswa kuzidi kujenga mfano katika kuongoza "ushirikiano wa Kusini na Kusini", kufanya ushirikiano wa kibiashara uwanufaishe watu wa China na Afrika bilioni 2.7, na kutoa mchango mpya katika ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika
 
WaTz na waAfrika kwa ujumla kazi tunayo! Huku waarabu kule wachina, sijui tutasalimika aje hapa!
 
Back
Top Bottom