Watu wanane wafariki dunia jijini dar baada ya kunywa gongo.

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Watu wanane wafariki dunia kigogo buyuni wilayani ilala jijini dar baada ya kunywa gongo inayosadikiwa kuchanganywa na spirit pamoja na JIKI ili kuiongezea ukali.source:STAR TV HABARI.
 
Aisee hatareeeee,hayo ndio madhara ya serikali kutegemea walevi kuendesha nchi,wamepandisha bei ya biereee watu wanahamia kwenye machozi ya simba aka chang'aa aka kingwendu aka maji makali aka kachaso
 
Bia zimepanda bei, gongo na pombe nyingine za asili ni dili MAPATO YATASHUKA KWA KUKOSA KODI, KAMPUNI ZA BIA ZITAYUMBA...
Kwa taarifa yako: Gongo na uchuuzaji wa madawa ya kulevya ndio kitega uchumi kikuu cha wakazi wa Bonde la Mpunga na maeneo mengine yaliyoathirika na mafuriko, ndio maana wale watu waligoma kuhamia Mabwepande.
 
K.O.N.Y.A.G.I- Kunywa Ongeza Nguvu Yafaa Angalia Gongo Inaua

S.A.F.A.R.I L.A.G.E.R--Sasa Angalia Fa.la Anaagiza Round Ingine Lakini Angalia Gharama Ewe Rafiki
 
Inasemekana pia hua wanatumia matambara ya madonda toka Muhimbili ili kupikia hiyo kitu ili kuongeza ukali.
 
Mbona asubui Mganga Mkuu wa Amana alisema amepokea jumla ya watu8 waliokunya hiyo gongo yenye sumu kati yao 2 ndio waliofariki dunia, watatu wamelazwa wodini na watatu wameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kupatiwa matibabu
 
Back
Top Bottom