Watu wa uswahilini sio wa kuwazoea kabisa

co fm

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
1,415
2,141
Wadau, kuna watu wanasema ooh ukiwa unaishi uswahilini ujichanganye na watu,ilo kwa sasa nalikataa kabisa.
Miezi kama miwili iliyopita hivi kulikuwa na kisherehe hapa mtaani ambapo ni uswazi kidogo,sherehe ilikuwa inafanyika nje tu hapo ya nyumba yetu ambapo mimi nimepanga so kuna sometimes nilikuwa natoka nje kidogo kuchekicheki then narudi ndani.

Sasa kuna mdada mmoja mkubwa kidogo yaani ni kama mke wa mtu hivi na ana mtoto mkubwa tu saizi ya 14+ akawa anajiongelesha ongelesha pale ooh mara kaniomba nimnunulie bia,mimi ndo ile usionekane haujichanganyi na wenzio basi nikampa 5k nikasema sio kitu.

Basi tokea siku hiyo kila akiniona anataka kuleta mazoea zoea kwangu na mara aniombe hela au bia,sasa mimi ninakuwa na mbania.Kimbembe ni leo nimeenda dukani nikamkuta anakunywa bia, si akaanza kuniomba nimuongeze bia nikamwambia hapa sina hela labda siki nyingine ila asikii hadi akamwambia mwenye duka ampe halafu mimi ntamlipia buku mimi nikakataa.

Baada ya kukataa akaondoka pale na kuniambia itanicost!!! Mpaka now najiuliza nini maana yake, kwamba yeye anahaki ya kutumia hela yangu bila ridhaa yangu.

Yaanu hapa nataka nimfate nimuulize vizuri itanicost nini? Yaani unitishe kisa hela yangu?
 
Back
Top Bottom