Watu 87 wakamatwa kwa tuhuma za mauaji katika mikoa 4 wakiwemo waganga wa jadi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,508
9,293
JESHI la polisi Mkoani Mbeya likishirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe, Rukwa pamoja na Katavi wamekamata watu 87 kwa tuhuma za makosa ya mauaji wakiwemo waganga wa kienyeji wanaopiga ramli chonganishi.

Kutokana na taarifa ambayo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la polisi Ulrich Matei, amesema Mikoa hiyo imeanza msako maalumu wa kupambana na mauaji yanayotokea katika ukanda huo kwa lengo la kutokomeza vitendo hivyo.

Kamanda Matei amesema Jeshi la Polisi pia linamshikilia mfanyabiashara pamoja na mganga mmoja wa jadi wakazi wa jiji la Mbeya kwa tuhuma za mauaji, huku akikemea vikali tabia ya vitendo vya kishirikina.
 
kwani serikali siaiamini ushirikina mbona wanashikiria sasa haowaganga wajandi na kukemea hivyo vitendo wakati wanasema hawaamini wao?
 
Back
Top Bottom