Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,194
- 10,929
Kundi kubwa la watu wako hatarini kufa huko jimbo la Nevada nchini Marekani baada ya kuzingirwa na matope mazito kwenye eneo walilokwenda kushiriki sherehe za kila mwaka za kumchoma mtu "Burning man".
Eneo kikawaida huwa ni vumbi kali lakini mwaka huu wakati watu wako katikati ya sherehe hizo mvua kubwa zimenyesha na kusababisha matope mazito yaliyowazuia watu hao kutoka kurudi makwao na huku shughuli za sherehe hiyo kusitishwa mara moja.
Mamlaka ya jimbo hilo limewataka watu hao wasijaribu kuondoka na hakuna ruhusu ya mtu yoyote kuingia eneo hilo..Pia wametakiwa wahifadhi chakula na maji walivyobakisha katika hakiba zoa.Katika hali ya taharuki hiyo utabiri wa hali ya hewa unaonesha mvua kubwa inatarajiwa kunyesha katika siku chache zijazo.
View: https://www.youtube.com/watch?v=6UxcX7_QNnU